Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,152
- 9,344
TUME YA MH PINDA IMETOA MAPENDEKEZO 130
Jumla ya mapendekezo 130 yametolewa na tume ya Kuchunguza Kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012. Mojawapo ni kupitiwa upya kwa mitaala ya elimu kuanzia shule za msingi hadi vyuo vya ualimu.
Hayo yamethibitishwa na mwenyekiti wa tume hiyo Prof Sifuni Mchome. Prof Mchome alisema mitaala iliyopo imeshapitisha muda wake kwani kwa kawaida mtalaa unabadilishwa baada ya kumaliza mzunguko wake mmoja, hivyo tume hiyo imependekeza kupitiwa upya kwa mitaala yote ambayo imemaliza mzunguko. Mzunguko huu ni miaka saba kwa elimu ya msingi, minne kwa sekondari na miwili kwa kidato cha tano na sita.
Pendekezo la kubadili mtaala maana yake nini?
Kama mitaala iliyopo ilishamaliza mizunguko yake siku nyingi bila kufanyiwa mabadiriko stahiki, maana yake mitaala iliyopo haiendani na hali halisi ya sasa. Kwa bahati mbaya sana, elimu isiyoendana na hali halisi katika jamii-inakuwa haina mvuto kwa wanafunzi kujifunza. Hawaoni kuhitaji kutumia maarifa wanayojifunza katika maisha yao moja kwa moja. Kukosa mvuto pia kunadumaza nia ya wanafunzi kuwa wadadisi na wabunifu. Kama ilivyowahi kuelezwa na wadau wengi miaka ya nyuma, tunapokosa mtaala unaoendana na hali yalisi ya sasa ni kwamba tunawaumiza wanafunzi na kuharibu misingi ya elimu tuliyoirithi.
Prof Mchome aliongeza: "...Mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2005 umetekelezwa bila kufanyiwa majaribio (piloting)."
TAFAKARI!
SOURCE: HAKIELIMU.