Tume ya kuchunguza Mafuriko Dar es Salaam

Tume ya kuchunguza Mafuriko Dar es Salaam

Igabiro

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
242
Reaction score
27
Kama ilivyo kawaida yetu Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inajiaandaa kuunda tume huru ya kuchunguza chanzo na athari za mafuriko yaliyotokea jijini dar es salaam ndani ya hizi siku mbili.
 
Awamu ya Kwanza, Awamu ya Pili, Awamu ya Tatu na sasa Awamu ya Nne

Kila jiwe ligeuzwe hapa.
 
Kama ilivyo kawaida yetu Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inajiaandaa kuunda tume huru ya kuchunguza chanzo na athari za mafuriko yaliyotokea jijini dar es salaam ndani ya hizi siku mbili.
Tume ya nini wakati wanaovunja sheria kwa wazi wanajulikana? Wabunge wanajigawia open-space na kujenga vituo vya mafuta, open-space wanajenga ofisi za CCM, Tibaijuka akibomoa kuta zao leo kesho anapelekwa mahakamani. Hakuna haja ya tume ni kupoteza mali za umma bure waharifu wanajulikana.
 
Tume ya kuchunguza mafuriko..kweli bongo raha.....mafuriko wanayachunguzia nini au wanachunguza kwa nini mvua imenyesha?
 
Tume ya nini wakati wanaovunja sheria kwa wazi wanajulikana? Wabunge wanajigawia open-space na kujenga vituo vya mafuta, open-space wanajenga ofisi za CCM, Tibaijuka akibomoa kuta zao leo kesho anapelekwa mahakamani. Hakuna haja ya tume ni kupoteza mali za umma bure waharifu wanajulikana.
mkui hiyo tume itakuwa haina kazi yoyote. kama ulivyosema viwanja vya wazi pamoja na mapito ya maji wanajigawia na kujenga mikita mikubwa kuzuia maji na matokeo yake maji yanaenda kujizolea vijimba vya walala hoi! pia kuna ijenzi holela dar wizara ya ardhi imeshindwa kupima viwanja dar. hata vikipimwa wale waliokwapua maeneo ya wazi ndio wanaojimegea mapande! Nadhani serikali sasa ina kila sababu ya kuvitwaa viwanja vyote vya wazi.na kuvirudisha mikononi mwetu.
 
Watu wanapata madhara (kupoteza mali, kufa, kushindwa kwenda kwenye shughuli zao au kurudi majumbani kwao, nk) halafu wengine wanatafuta namna ya kujitengenezea ulaji. Hii nchi, mhh!!
 
mkui hiyo tume itakuwa haina kazi yoyote. kama ulivyosema viwanja vya wazi pamoja na mapito ya maji wanajigawia na kujenga mikita mikubwa kuzuia maji na matokeo yake maji yanaenda kujizolea vijimba vya walala hoi! pia kuna ijenzi holela dar wizara ya ardhi imeshindwa kupima viwanja dar. hata vikipimwa wale waliokwapua maeneo ya wazi ndio wanaojimegea mapande! Nadhani serikali sasa ina kila sababu ya kuvitwaa viwanja vyote vya wazi.na kuvirudisha mikononi mwetu.

Uokoaji wao tu mie ndo unanisikitisha, na hizo helkopta zinazopitapita sioni kazi yake ya maana! Najaribu kufikiria mvua zikizidi zaidi ya ilivyo sasa, sijui tutapoteza watu wangapi wapendwa.......Mungu atunusuru!!!
 
Tatizo la Bongo kila maafa inaguezwa kuwa mkao wa kula! Tume hiyo itasaidia nini na mafuriko yamekwishatokea? Ni bora hizo hela walipe Architect kwa ajili ramani :A S-coffee:ya drainage system ya jiji!
 
Mkuu ni kweli serikali wameunda hiyo tume? Ni nani asiyejua chanzo ni mvua? Na huku tukiwa na mitaro iliyoziba. Jk endelea kufanya matatizo yetu kuwa mtaji kwako tu Mungu ndiye atakae kuumbua
 
Kanuni za emergency preparedness and response ziko 4 tu!
1 Pre-disaster preparation: hapa unaangalia kitu gani chaweza kutokea (risk analysis), watu gani wataathirika na watasaidiwaje?
2 disaster preparation: kitu gani kitahitajika kwa ajili ya kuhakikisha minimum damage. Kutakuwa na mafunzo, ukusanyaji na vifaa na assembly points
3 disaster response: hapa emergency imetokea na ni wakati wa kukamilisha mipango iliyopangwa kabla. Pale ambapo kitu hakijapangiwa mpango maamuzi ya haraka yanafanyika. Hii ndo stage tulipo na mafuriko yetu leo.
4 post disaster response: disaster imeshaisha, kuna wahanga watakaohitaji matibabu, ushauri wa kisaikolojia na misaada ya mali. Muhimu tunaangalia mchakato mzima uliendaje, wapi tulikosea, wapi tulipotea, uwajibikaji wetu na kama kuna ziada tunayohitaji. From this point tunarudisha vifaa vyetu tayari kwa dharura ijayo.

My take: hata kama interest yetu ni tume tu, sio neno. Tuna opportunity ya kuunda tume katika kila stage na kula hela huku tunafanya kazi na wahudumiwa wasilalamike! Inaudhi kuliko maudhi yenyewe!
 
Back
Top Bottom