Heshima niliyoweka kwa Warioba imetoka kabisa baada ya kusoma maoni ya katiba kwani Warioba ameweka zaidi mawazo yake badala ya Tanzania mbele.
1. Muungano: Warioba alikuwa mwenyekiti wa tume ya muungano 1995 tume hiyo ilipendekeza muundo wa serikali tatu kitu ambacho ametumia katiba kuhakikisha agenda yake pekee ndiyo inakuwepo kwenye katiba hakuna kitu kingine cha maana kinachobadilika.
2. Land: Pamoja na kuwa na matatizo mengi ya viwanja ambako vibali vinachukua hadi miaka mitano tume ya katiba haijaweka wala kuongelea kuhusu hili. Uchumi wote wa Tanzania unategemea Land sasa tutakuwaje na katiba ambayo haiongelei haki ya land wakati sasa sio wakati wa mkoloni.
3. Uraia: Kuna Watanzania wengi sana wapo na watakwenda nchi mbalimbali kutafuta maisha nchi za jirani na mabara mengine. Hakuna kipengele chochote kinachowaongelea hawa. Kenya kwa mfano wameweka kwenye katiba yao kwamba Kama mtu amezaliwa Kenya au ni Mkenya hawazi kuchukuliwa uraia wake kwasababu ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Watanzania wana mila kama wakenya swala la uraia linahusisha urithi, vifo na maziko tutakuwa watu wa ajabu kumzuia Matanzania kwenda kuangalia Makaburi ya ndugu zao kwasababu ya uraia na pasipo faida yeyote ya maana.
4. Uwekezaji: Hakuna sehemu yeyote ya uwekezaji kwenye katiba mfano katiba ingeweza kusema mikataba yote ya serikali ni lazima itangazwe kwa bunge na wananchi wote waione. Hii ingepunguza mikataba ya siri ya rushwa. Hizo kampuni zinazokuja kuwekeza mfano za ulaya ma marekani mikataba kwao iko wazi sasa ni kwanini mikataba kwetu ni ya siri.
Katiba vilevile ingetakiwa kusema kwa uhakiki kwamba Tanzania sio nchi ya kijamaa kwani bila kusema ukweli kwamba nchi yetu kwasasa ni nchi ya namna gani hatutapata maendeleo.