Tume ya Katiba au Tume ya Muungano-Warioba atia aibu Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,593
8,734
Heshima niliyoweka kwa Warioba imetoka kabisa baada ya kusoma maoni ya katiba kwani Warioba ameweka zaidi mawazo yake badala ya Tanzania mbele.

1. Muungano: Warioba alikuwa mwenyekiti wa tume ya muungano 1995 tume hiyo ilipendekeza muundo wa serikali tatu kitu ambacho ametumia katiba kuhakikisha agenda yake pekee ndiyo inakuwepo kwenye katiba hakuna kitu kingine cha maana kinachobadilika.
2. Land: Pamoja na kuwa na matatizo mengi ya viwanja ambako vibali vinachukua hadi miaka mitano tume ya katiba haijaweka wala kuongelea kuhusu hili. Uchumi wote wa Tanzania unategemea Land sasa tutakuwaje na katiba ambayo haiongelei haki ya land wakati sasa sio wakati wa mkoloni.
3. Uraia: Kuna Watanzania wengi sana wapo na watakwenda nchi mbalimbali kutafuta maisha nchi za jirani na mabara mengine. Hakuna kipengele chochote kinachowaongelea hawa. Kenya kwa mfano wameweka kwenye katiba yao kwamba Kama mtu amezaliwa Kenya au ni Mkenya hawazi kuchukuliwa uraia wake kwasababu ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Watanzania wana mila kama wakenya swala la uraia linahusisha urithi, vifo na maziko tutakuwa watu wa ajabu kumzuia Matanzania kwenda kuangalia Makaburi ya ndugu zao kwasababu ya uraia na pasipo faida yeyote ya maana.
4. Uwekezaji: Hakuna sehemu yeyote ya uwekezaji kwenye katiba mfano katiba ingeweza kusema mikataba yote ya serikali ni lazima itangazwe kwa bunge na wananchi wote waione. Hii ingepunguza mikataba ya siri ya rushwa. Hizo kampuni zinazokuja kuwekeza mfano za ulaya ma marekani mikataba kwao iko wazi sasa ni kwanini mikataba kwetu ni ya siri.

Katiba vilevile ingetakiwa kusema kwa uhakiki kwamba Tanzania sio nchi ya kijamaa kwani bila kusema ukweli kwamba nchi yetu kwasasa ni nchi ya namna gani hatutapata maendeleo.
 
mkuu una hoja nzur, lakni hil la kutia aibu... halna msing, ungelifuta kaka.... sasa hilo la serkal tatu naona limekuuma xana..... we ulitakaje? muda bado upo!
 
Pole Mtanzania, ni maoni yako ingawa title ya thread ipo kama jamaa kaongoza tume ambayo imeleta rasimu isiyo na maana kabisa. Kumbe ni vipengele na mtazamo tofauti kwa wanaoguswa ndio katia aibu! We may need to be careful not to personalize when addressing issues that we also have a room to reverse their direction.
 
Hiyo ni rasimu tuu sio katiba bado hatua tatu muhimu ili iwe katiba kwanza kujadiliwa na mabaraza ya katiba, kujadiliwa na bunge la katiba na kupigiwa kura ya maoni, hayo mambo yaliyosahaulika bado yana nafasi ya kuingizwa pia vitu kama madaraka makubwa ya rais yanahitaji kupunguzwa zaidi!hii ni hatua ya awali tuu!!
 
Ile rasimu kaka...bado inahitaji nyama na marekebisho mengi tuu.....kama kwenye madraka ya raisi pia ...wakuu wa mikoa wilaya..vyeo kama katibu kata..tarafa..shina nk....haijaongelea pia mambo ya tume ya kupambana na rushwa itaundajwe ili iweze kuwa na meno(mm naona ni muhimu)...bado inahitaji kufanyiwa kazi ili iwe katiba nzuri
 
Hiyo ni rasimu tuu sio katiba bado hatua tatu muhimu ili iwe katiba kwanza kujadiliwa na mabaraza ya katiba, kujadiliwa na bunge la katiba na kupigiwa kura ya maoni, hayo mambo yaliyosahaulika bado yana nafasi ya kuingizwa pia vitu kama madaraka makubwa ya rais yanahitaji kupunguzwa zaidi!hii ni hatua ya awali tuu!!
Ni rasimu sawa. Lakini wasiwasi wangu ni kwamba kama the majority ya hao wanaopiga kura ni wa cham kimoja tutapata katiba kweli? Tunategemea rasimu ngapi kabla ya kupata the real thing?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hivi ile tume ya 1995 ilikuwa ya warioba au ya nyalali?
 
Heshima niliyoweka kwa Warioba imetoka kabisa baada ya kusoma maoni ya katiba kwani Warioba ameweka zaidi mawazo yake badala ya Tanzania mbele.

1. Muungano: Warioba alikuwa mwenyekiti wa tume ya muungano 1995 tume hiyo ilipendekeza muundo wa serikali tatu kitu ambacho ametumia katiba kuhakikisha agenda yake pekee ndiyo inakuwepo kwenye katiba hakuna kitu kingine cha maana kinachobadilika.
2. Land: Pamoja na kuwa na matatizo mengi ya viwanja ambako vibali vinachukua hadi miaka mitano tume ya katiba haijaweka wala kuongelea kuhusu hili. Uchumi wote wa Tanzania unategemea Land sasa tutakuwaje na katiba ambayo haiongelei haki ya land wakati sasa sio wakati wa mkoloni.
3. Uraia: Kuna Watanzania wengi sana wapo na watakwenda nchi mbalimbali kutafuta maisha nchi za jirani na mabara mengine. Hakuna kipengele chochote kinachowaongelea hawa. Kenya kwa mfano wameweka kwenye katiba yao kwamba Kama mtu amezaliwa Kenya au ni Mkenya hawazi kuchukuliwa uraia wake kwasababu ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Watanzania wana mila kama wakenya swala la uraia linahusisha urithi, vifo na maziko tutakuwa watu wa ajabu kumzuia Matanzania kwenda kuangalia Makaburi ya ndugu zao kwasababu ya uraia na pasipo faida yeyote ya maana.
4. Uwekezaji: Hakuna sehemu yeyote ya uwekezaji kwenye katiba mfano katiba ingeweza kusema mikataba yote ya serikali ni lazima itangazwe kwa bunge na wananchi wote waione. Hii ingepunguza mikataba ya siri ya rushwa. Hizo kampuni zinazokuja kuwekeza mfano za ulaya ma marekani mikataba kwao iko wazi sasa ni kwanini mikataba kwetu ni ya siri.

Katiba vilevile ingetakiwa kusema kwa uhakiki kwamba Tanzania sio nchi ya kijamaa kwani bila kusema ukweli kwamba nchi yetu kwasasa ni nchi ya namna gani hatutapata maendeleo.

Duo citizenship? No thank you! You are either a citizen of Tanganyika or something else.... no schizophrenic citizenship.
 
Ni rasimu sawa. Lakini wasiwasi wangu ni kwamba kama the majority ya hao wanaopiga kura ni wa cham kimoja tutapata katiba kweli? Tunategemea rasimu ngapi kabla ya kupata the real thing?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Baada ya mjadala wa mabaraza ya katiba tume ya Warioba itaandika rasimu nyingine itakayoegemea mawazo ya mabaraza ya katiba na hiyo ndio itaenda kwenye bunge la katiba! Baada ya mjadala wa Bunge la katiba Tume ya Warioba itaandika rasimu nyingine itokanayo na mjadala wa bunge la katiba itakayoenda kupigiwa kura ya maoni kama ikikubalika na zaidi ya 50% ya watanzania then inakuwa katiba!!Watanzania kwenye hili tuweke vyama kando ni swala la kitaifa linagusa maisha yetu bila kujali ccm chadema Libreral au DP tuige majirani zetu walivosuka katiba yao bila itikadi za vyama!!
 
1. Muungano: Warioba alikuwa mwenyekiti wa tume ya muungano 1995 tume hiyo ilipendekeza muundo wa serikali tatu kitu ambacho ametumia katiba kuhakikisha agenda yake pekee ndiyo inakuwepo kwenye katiba hakuna kitu kingine cha maana kinachobadilika.

Hapa nakumbuka awali tuliambiwa tusiujadili muungano. Ila maoni ya rasimu yamewakilisha mawazo ya msingi ya baadhi yetu kuhusu hili la muungano.

2. Land: Pamoja na kuwa na matatizo mengi ya viwanja ambako vibali vinachukua hadi miaka mitano tume ya katiba haijaweka wala kuongelea kuhusu hili. Uchumi wote wa Tanzania unategemea Land sasa tutakuwaje na katiba ambayo haiongelei haki ya land wakati sasa sio wakati wa mkoloni.

Ardhi ilizungumziwa sana kwenye maoni ya katiba inashangaza kuwa haipo kwenye rasmu hii. Kwa kweli mimi na wengine tungependa iwepo. Pamoja na kuwepo suala la Ardhi naamini ni pamoja na rasilimali zilizopo kwenye ardhi hiyo. Kinachonikera ni rais kuwa na madaraka ya kuwasogeza watu kwenye ardhi yao bila makubaliano; kwa kisingizio cha uwekezaji.

3. Uraia: Kuna Watanzania wengi sana wapo na watakwenda nchi mbalimbali kutafuta maisha nchi za jirani na mabara mengine. Hakuna kipengele chochote kinachowaongelea hawa. Kenya kwa mfano wameweka kwenye katiba yao kwamba Kama mtu amezaliwa Kenya au ni Mkenya hawazi kuchukuliwa uraia wake kwasababu ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Watanzania wana mila kama wakenya swala la uraia linahusisha urithi, vifo na maziko tutakuwa watu wa ajabu kumzuia Matanzania kwenda kuangalia Makaburi ya ndugu zao kwasababu ya uraia na pasipo faida yeyote ya maana.

Hii ni kero kiasi cha kutumiiwa vilivyo na wapora uraia dunia nzima kutumia pasipoti ya Tanzania (Wasomali). Sasa hivi majirani zetu wanajipachika uraia kwa udhaifu wa viongozi na serikali iliyoko madarakani.

4. Uwekezaji: Hakuna sehemu yeyote ya uwekezaji kwenye katiba mfano katiba ingeweza kusema mikataba yote ya serikali ni lazima itangazwe kwa bunge na wananchi wote waione. Hii ingepunguza mikataba ya siri ya rushwa. Hizo kampuni zinazokuja kuwekeza mfano za ulaya ma marekani mikataba kwao iko wazi sasa ni kwanini mikataba kwetu ni ya siri.

Hili neno uwekezaji ni la watawala tu, na kandamizi kwa wananchi wanyonge. Ni kwa sababu ya udhaifu wa katiba kuhusu uchumi kuwanufaisha wananchi.

Katiba vilevile ingetakiwa kusema kwa uhakiki kwamba Tanzania sio nchi ya kijamaa kwani bila kusema ukweli kwamba nchi yetu kwasasa ni nchi ya namna gani hatutapata maendeleo.

Nadhani wamefanya makusudi kutojiainisha na milengo ya kisiasa za uchumi za kimataifa. Mimi ningefurahi wangeingiza suala la Taifa kujitegemea. Ujamaa haupo, umepari unaonewa aibu lakini unafantwa kwa vitendo
 
Huo ni mtazamo wako,kila binadamu anamapungufu lakini katika hili Warioba kajitahidi sana na anastahili pongezi,kadri mchakato huu unavyoendelea nadhani tutapata katiba nzuri.
 
Mtoa uzi umenisikitisha kwa title yako inayomlenga na kumshambulia mzee warioba.Huyu ni Mwenyekiti wa Tume inayoratibu mabadiliko ya katiba,Ametangaza rasimu ya mapendekezo ya katiba na si katiba tayari.Wamefanya kazi nzuri ni mwanzo tu.'Big up' Tume ! Tutafika tu.IWE TANGANYIKA,ZANZIBAR AU IBAKI TANZANIA.Lakini bila remote ya mwl.Nyerere wakuu.
 
Heshima niliyoweka kwa Warioba imetoka kabisa baada ya kusoma maoni ya katiba kwani Warioba ameweka zaidi mawazo yake badala ya Tanzania mbele.

1. Muungano: Warioba alikuwa mwenyekiti wa tume ya muungano 1995 tume hiyo ilipendekeza muundo wa serikali tatu kitu ambacho ametumia katiba kuhakikisha agenda yake pekee ndiyo inakuwepo kwenye katiba hakuna kitu kingine cha maana kinachobadilika.
2. Land: Pamoja na kuwa na matatizo mengi ya viwanja ambako vibali vinachukua hadi miaka mitano tume ya katiba haijaweka wala kuongelea kuhusu hili. Uchumi wote wa Tanzania unategemea Land sasa tutakuwaje na katiba ambayo haiongelei haki ya land wakati sasa sio wakati wa mkoloni.
3. Uraia: Kuna Watanzania wengi sana wapo na watakwenda nchi mbalimbali kutafuta maisha nchi za jirani na mabara mengine. Hakuna kipengele chochote kinachowaongelea hawa. Kenya kwa mfano wameweka kwenye katiba yao kwamba Kama mtu amezaliwa Kenya au ni Mkenya hawazi kuchukuliwa uraia wake kwasababu ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Watanzania wana mila kama wakenya swala la uraia linahusisha urithi, vifo na maziko tutakuwa watu wa ajabu kumzuia Matanzania kwenda kuangalia Makaburi ya ndugu zao kwasababu ya uraia na pasipo faida yeyote ya maana.
4. Uwekezaji: Hakuna sehemu yeyote ya uwekezaji kwenye katiba mfano katiba ingeweza kusema mikataba yote ya serikali ni lazima itangazwe kwa bunge na wananchi wote waione. Hii ingepunguza mikataba ya siri ya rushwa. Hizo kampuni zinazokuja kuwekeza mfano za ulaya ma marekani mikataba kwao iko wazi sasa ni kwanini mikataba kwetu ni ya siri.

Katiba vilevile ingetakiwa kusema kwa uhakiki kwamba Tanzania sio nchi ya kijamaa kwani bila kusema ukweli kwamba nchi yetu kwasasa ni nchi ya namna gani hatutapata maendeleo.

Kwa mzee kama yeye, na anavyopenda kulazimisha mambo! Aibu!
 
Katika ngazi za vijiji, sheria ziko wazi ukitaka hata kulima / kununua eneo linalozidi eka 10 / 50 (sikumbuki figure) kwa nia ya kuwekeza mkutano mkuu wa kijiji ndio wenye uwezo wa kupitisha hayo, Pia sheria zinasisitiza uwazi na ukweli kwa kila kinachofanyika kijiji na ripoti itolewe katika mikutano ya vijiji kila miezi mitatu. Hata kama una kiwanja chako ukataka kubadilisha matumizi mathalani kujenga shule n.k sheria zinalazimisha kutoa tangazo na wananchi wakubaliane na azma hiyo.
Ninashangaa inapofika huko juu wanadai kila kitu kinakuwa siri!!.
 
nadhani kuna haja ya kufafanua maana halisi ya rasimu ya katiba ndipo watu wje na hoja kama hizi
 
Jaji Warioba umefanikiwa kuweka agenda yako ya muungano lakini haujasaidia Tanzania kwenye katiba. Katiba ingetakiwa kulenga vitu vikuu vifuatavyo

1. Haki za kibinadamu: Dini, jinsia isiwe kikwazo cha maendeleo na mtu
2. Mfumo wa siasa unaoeleweka.
3. Mundo wa serikali Muungano, mikoa,bunge, madaraka.
4. Haki ya Land: Miaka mitano kwa vibali hatutaendelea
5. Uwekezaji: Kuongeza uwazi kama mikataba kuwa wazi.
6. Haki ya uraia: Mtanzania ni nani?,Permanent residence status.

Sasa tumebakia kuzungumzia muungano tu na jinsi ya kufanya serikali kuwa kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom