Tume ya Katiba au Tume ya Muungano-Warioba atia aibu Tanzania

Heshima niliyoweka kwa Warioba imetoka kabisa baada ya kusoma maoni ya katiba kwani Warioba ameweka zaidi mawazo yake badala ya Tanzania mbele.

1. Muungano: Warioba alikuwa mwenyekiti wa tume ya muungano 1995 tume hiyo ilipendekeza muundo wa serikali tatu kitu ambacho ametumia katiba kuhakikisha agenda yake pekee ndiyo inakuwepo kwenye katiba hakuna kitu kingine cha maana kinachobadilika.
2. Land: Pamoja na kuwa na matatizo mengi ya viwanja ambako vibali vinachukua hadi miaka mitano tume ya katiba haijaweka wala kuongelea kuhusu hili. Uchumi wote wa Tanzania unategemea Land sasa tutakuwaje na katiba ambayo haiongelei haki ya land wakati sasa sio wakati wa mkoloni.
3. Uraia: Kuna Watanzania wengi sana wapo na watakwenda nchi mbalimbali kutafuta maisha nchi za jirani na mabara mengine. Hakuna kipengele chochote kinachowaongelea hawa. Kenya kwa mfano wameweka kwenye katiba yao kwamba Kama mtu amezaliwa Kenya au ni Mkenya hawazi kuchukuliwa uraia wake kwasababu ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Watanzania wana mila kama wakenya swala la uraia linahusisha urithi, vifo na maziko tutakuwa watu wa ajabu kumzuia Matanzania kwenda kuangalia Makaburi ya ndugu zao kwasababu ya uraia na pasipo faida yeyote ya maana.
4. Uwekezaji: Hakuna sehemu yeyote ya uwekezaji kwenye katiba mfano katiba ingeweza kusema mikataba yote ya serikali ni lazima itangazwe kwa bunge na wananchi wote waione. Hii ingepunguza mikataba ya siri ya rushwa. Hizo kampuni zinazokuja kuwekeza mfano za ulaya ma marekani mikataba kwao iko wazi sasa ni kwanini mikataba kwetu ni ya siri.

Katiba vilevile ingetakiwa kusema kwa uhakiki kwamba Tanzania sio nchi ya kijamaa kwani bila kusema ukweli kwamba nchi yetu kwasasa ni nchi ya namna gani hatutapata maendeleo.
Sio kweli Warioba katia Aibu kwani japo ni Mwenyekiti lakini tume ipo na viongozi wengine Sidhani Kama atakuwa kawaburuza na hii bado ni rasimu tu sio katika harisi
 
Kwenye Tume ya katiba pamesheheni viongozi wengi tena toka pande zote yaani ZNZ na TZ Bara Sio rahisi Warioba apitishe mawazo binafsi kwa taaarifa yako hayo ni maoni ya Wengi tena Wazenji kwani wana ajenda za Siri juu ya Muungano Nadhani unakumbuka staili iliyotumika kule URUSI serikari Tatu ilitumika na akina Yestin kutekeleza adhima Yao .hivyo endapo Rasimu utapitia na kuikubali serikari tatu tujiandae Zanzibar kujitenga na kuipa Nafuu Bara kiuchumi kwani Bara itakuwa Nchi tajiri kulingana na rasilimali zilizopo hazitakuwa na mgao pili Raia wa Zenji watakuwa raia wa Nchi Jilani watalipia Viza na vibali vya kuishi na kufanya kazi Bara .wenye kuitaka serikari tatu wanalijua hili
 
Tanzania, the land of Wailers and mourners. Hii nchi imetengeneza raia walalamikaji tu, Rais ananung'unika, Raia wananung'unika. kazi kwelikweli!
 
Ardhi siyo suala la muungano hivyo katiba ya muungano haiitaji kulizungumzia. km ww ni Mtanganyika jiandae tudai asiyekua mtanganyika na anamiliki ardhi anyanganywe
 
Walalamishi ni wale milioni 1.5 lakini Hawa milion 45 sio Walalamishi kabsa! Kumbuka Hawa m 45 wao wana madini,mbuga za wanyama,Gesi,mazao ya biashara ,Asali,mbao na Rasilimali lukuki huku wakiwasaidia Umeme na Chakula hao M 1.5 lakini hawaliziki kabsa wanapenda kulalamika pasipo kujua jinsi wanavyosaidiwa .kumbuka wabunge wa huko m1.5 wao wanaingia Dodoma na kuvuna posho lakini hivyo hivyo kwa mawaziri Lakini wa M 45 hawana nafasi wala posho huko Kwao M1.5 kuna msemo wasema hv Changu changu na chako ni cha wote hiyo Ndio falsafa ya akina M1.5
 
Duo citizenship? Lugha ya watu jamani!

Huku ni kukinyanyapaaa Kiswahili JF wambieni wapenda kiswanglish Kuwa tukipende Kiswahili kwani ni lugha yetu ile dhana potovu ya kudhani Kingereza ni Usomi inapaswa ifutike kwani Taaluma na inapatikana kwenye lugha mbali mbali Dunia huku Kingereza kikibaki ni Lugha yaawasiliano tu wapo wasomi toka German,china,Italy ,Ufaransa,Rusia nk hawajui Kingereza?tukipende kiswahili tuachane na ulimbukeni
 
Duo citizenship? No thank you! You are either a citizen of Tanganyika or something else.... no schizophrenic citizenship.

Duo citizenship? Lugha ya watu jamani!

Huku ni kukinyanyapaaa Kiswahili JF wambieni wapenda kiswanglish Kuwa tukipende Kiswahili kwani ni lugha yetu ile dhana potovu ya kudhani Kingereza ni Usomi inapaswa ifutike kwani Taaluma na inapatikana kwenye lugha mbali mbali Dunia huku Kingereza kikibaki ni Lugha yaawasiliano tu wapo wasomi toka German,china,Italy ,Ufaransa,Rusia nk hawajui Kingereza?tukipende kiswahili tuachane na ulimbukeni

Wakuu wangu Mag3 na minyoo mie ni Mtanzania kwa sasa. Taifa hili likitawanyika kama Urusi nitakuwa Mtanganyika. Haitatokea hata siku moja nikawa kitu kingine. Najua kuzungumza Kinyakyusa, Kinyiha, Kimalila, Kiswahili, Kiingereza na ninabahatisha kidogo Kifaransa kwa mbali.

Zipo fikra ambazo huwa zinagoma kuwasilisha kwa maneno machache katika lugha mojawapo ya hizi kwa hiyo hujikuta natafuta kuchanganya kidogo. Hili ni sawa kabisa na maneo ya Kilatini kutumika katika Kiingereza kwa lengo la kutaka kueleweka-- ceteris paribus of course; au Kitumia Kiarabu kufafanua kifungu cha Qur-an Tukufu wakati unaoongea nao ni watu wanaoelewa Kiswahili na siyo Kiarabu au Kilatini.

Si kila mchanganyo wa lugha unakuwa na lengo la kujitia kujua. Mwasalipa!
 
Walalamishi ni wale milioni 1.5 lakini Hawa milion 45 sio Walalamishi kabsa! Kumbuka Hawa m 45 wao wana madini,mbuga za wanyama,Gesi,mazao ya biashara ,Asali,mbao na Rasilimali lukuki huku wakiwasaidia Umeme na Chakula hao M 1.5 lakini hawaliziki kabsa wanapenda kulalamika pasipo kujua jinsi wanavyosaidiwa .kumbuka wabunge wa huko m1.5 wao wanaingia Dodoma na kuvuna posho lakini hivyo hivyo kwa mawaziri Lakini wa M 45 hawana nafasi wala posho huko Kwao M1.5 kuna msemo wasema hv Changu changu na chako ni cha wote hiyo Ndio falsafa ya akina M1.5
wewe dog upo na akili lakini.. hao wabunge wanaingia kwenye bunge la muungani.. wewe huna nyumba tanganyika homeless wewe.. hauna makaani.. sasa anza lkazi ya kujenga bunge na kadhalika.. hilo bungeni letu sote yaani la muungano.......wacha kujisemea ulikua huyajui....tafuta nyumba na sheria zako kwanza sisi tupo na kila kitu cha kwenu huko zenj...
 
Duo citizenship? Napita tu...

Tukipende Kiswahili jamani kuendekeza ulambukeni wa lugha za wakoloni haujengi tufikiri kwa lugha mama kiswahili .na Kama watu hawakitaki Kiswahili katiba mpya Ndio jawabu
 
Ardhi siyo suala la muungano hivyo katiba ya muungano haiitaji kulizungumzia. km ww ni Mtanganyika jiandae tudai asiyekua mtanganyika na anamiliki ardhi anyanganywe

Ndio maana tunasema huyu kaenda kutengeneza katiba ya Muungano na sio Tanganyika.
Ni wakati sasa Tume nyingine iteuliwe kwa ajili ya kuandika katiba ya Tanganyika.
 
Uraia ni haki ya mzawa na si siasa na mawazo ya watu. Mzawa aliyezaliwa Tanzania na kukulia Tanzania ni Mtanzania kama tunataka au hatutaki ni haki yake kuwa Mtanzania. Kama ameenda nchi nyingine kafanya nini sisi haituhusu kwani kila mtu ajali uraia wake. Hizi siasa za watu eti kuamua nani ni Mtanzania na nani sio hasa kwa wazawa ni upuuzi usio na msingi wewe jijali mwenyewe kwanza na haki zako badala ya kufirikia uraia ni passport. Kuna passport zimeuzwa nyingi kwa watu wa Rwanda na Nigeria lakini hao si Watanzania. Hivi Watanzania wanaokufa nje na kusafirishwa sijawahi kusikia wachangiaji wakiulizwa passport zao au vibali vyao watu wanajijua kama ni Watanzania hawahitaji siasa au watu wengine kujua hilo na wanasadiana kama ndugu dunia nzima.
 
Heshima niliyoweka kwa Warioba imetoka kabisa baada ya kusoma maoni ya katiba kwani Warioba ameweka zaidi mawazo yake badala ya Tanzania mbele.

1. Muungano: Warioba alikuwa mwenyekiti wa tume ya muungano 1995 tume hiyo ilipendekeza muundo wa serikali tatu kitu ambacho ametumia katiba kuhakikisha agenda yake pekee ndiyo inakuwepo kwenye katiba hakuna kitu kingine cha maana kinachobadilika.
2. Land: Pamoja na kuwa na matatizo mengi ya viwanja ambako vibali vinachukua hadi miaka mitano tume ya katiba haijaweka wala kuongelea kuhusu hili. Uchumi wote wa Tanzania unategemea Land sasa tutakuwaje na katiba ambayo haiongelei haki ya land wakati sasa sio wakati wa mkoloni.
3. Uraia: Kuna Watanzania wengi sana wapo na watakwenda nchi mbalimbali kutafuta maisha nchi za jirani na mabara mengine. Hakuna kipengele chochote kinachowaongelea hawa. Kenya kwa mfano wameweka kwenye katiba yao kwamba Kama mtu amezaliwa Kenya au ni Mkenya hawazi kuchukuliwa uraia wake kwasababu ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Watanzania wana mila kama wakenya swala la uraia linahusisha urithi, vifo na maziko tutakuwa watu wa ajabu kumzuia Matanzania kwenda kuangalia Makaburi ya ndugu zao kwasababu ya uraia na pasipo faida yeyote ya maana.
4. Uwekezaji: Hakuna sehemu yeyote ya uwekezaji kwenye katiba mfano katiba ingeweza kusema mikataba yote ya serikali ni lazima itangazwe kwa bunge na wananchi wote waione. Hii ingepunguza mikataba ya siri ya rushwa. Hizo kampuni zinazokuja kuwekeza mfano za ulaya ma marekani mikataba kwao iko wazi sasa ni kwanini mikataba kwetu ni ya siri.

Katiba vilevile ingetakiwa kusema kwa uhakiki kwamba Tanzania sio nchi ya kijamaa kwani bila kusema ukweli kwamba nchi yetu kwasasa ni nchi ya namna gani hatutapata maendeleo.
Nadhani hapo nilipokazia ndipo kuna hoja.
Ni kweli ardhi haijaongelewa, kila ukiisoma katiba kwa umakini unaweza kuelewa jambo lilichoachwa kwa makusudi.

Ardhi imeachwa kwa makusudi kwa maana kuwa si jambo la muungano tena. Hilo litashughulikiwa na serikali za washirika.
Huu ni mwiba mwingine unaoipiga znz! niachie hapo
 
Unaleta thread bila kujishughulisha na ubongo wako japo kidogo, tena kwa jazba,hili ndio tatizo letu wa tanzania kwa miaka mingi,warioba kaeleza hii ni rasimu ya tanzania na sio tanganyika wala zanzibar, hivyo hayo yote uliyoeleza majibu yake yatajibiwa na katiba za nchi husika na sio hii ya sote.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Binafsi nimeshangaa mambo ya msingi kama madaraka mikoani kurudishwa kwenye katiba za Tanganyika na Zanzibar maana yake hii katiba ya muungano hatutaona zile impact za moja kwa moja hadi kila nchi ianze tena mchakato wa katiba yake!
10yrs tutahangaika na katiba!
 
Ulipeleka maoni yako? sasa kama hukupeleka ndio unakuja na mawazo kuwa rasimu ya katiba ni maoni ya warioba? kuwa na subira, kama hutaki fanya kazi ngoja watu wajadili kwa niaba yako....usilalamike
 
Heshima niliyoweka kwa Warioba imetoka kabisa baada ya kusoma maoni ya katiba kwani Warioba ameweka zaidi mawazo yake badala ya Tanzania mbele.

1. Muungano: Warioba alikuwa mwenyekiti wa tume ya muungano 1995 tume hiyo ilipendekeza muundo wa serikali tatu kitu ambacho ametumia katiba kuhakikisha agenda yake pekee ndiyo inakuwepo kwenye katiba hakuna kitu kingine cha maana kinachobadilika.
2. Land: Pamoja na kuwa na matatizo mengi ya viwanja ambako vibali vinachukua hadi miaka mitano tume ya katiba haijaweka wala kuongelea kuhusu hili. Uchumi wote wa Tanzania unategemea Land sasa tutakuwaje na katiba ambayo haiongelei haki ya land wakati sasa sio wakati wa mkoloni.
3. Uraia: Kuna Watanzania wengi sana wapo na watakwenda nchi mbalimbali kutafuta maisha nchi za jirani na mabara mengine. Hakuna kipengele chochote kinachowaongelea hawa. Kenya kwa mfano wameweka kwenye katiba yao kwamba Kama mtu amezaliwa Kenya au ni Mkenya hawazi kuchukuliwa uraia wake kwasababu ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Watanzania wana mila kama wakenya swala la uraia linahusisha urithi, vifo na maziko tutakuwa watu wa ajabu kumzuia Matanzania kwenda kuangalia Makaburi ya ndugu zao kwasababu ya uraia na pasipo faida yeyote ya maana.
4. Uwekezaji: Hakuna sehemu yeyote ya uwekezaji kwenye katiba mfano katiba ingeweza kusema mikataba yote ya serikali ni lazima itangazwe kwa bunge na wananchi wote waione. Hii ingepunguza mikataba ya siri ya rushwa. Hizo kampuni zinazokuja kuwekeza mfano za ulaya ma marekani mikataba kwao iko wazi sasa ni kwanini mikataba kwetu ni ya siri.

Katiba vilevile ingetakiwa kusema kwa uhakiki kwamba Tanzania sio nchi ya kijamaa kwani bila kusema ukweli kwamba nchi yetu kwasasa ni nchi ya namna gani hatutapata maendeleo.
Hii ni katiba ya Serikali ndogo ya muungano. Haya uliyoyasema hapa yatakuwa kwenye katiba za zanzibar na Tanganyika kwani siyo mambo ya muungano
 
katiba hii ni ya siasa hakuna mambo yeyote ya maendeleo ni mfumo wa siasa tu Land na mambo muhimu hakuna!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom