Tume ya kada Mwinchande na CCM kama ile ya Jaji Zuberi 1995. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya kada Mwinchande na CCM kama ile ya Jaji Zuberi 1995.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, May 24, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  NA JABIR IDRISSA
  Rais Amani Abeid Karume alipounda tume mpya ya kusimamia uchaguzi mkuu wa 2010, alimtaja Mwinchande mwenyekiti. Makada wenzake katika Tume hiyo ni pamoja na Said Bakari Jecha, waziri katika serikali zilizopita za CCM na mtu ambaye rekodi yake ya utumishi ya tangu serikali ya kwanza baada ya mapinduzi ya 12 Januari 1964, ingali vichwani mwa watu.
  Lakini hebu wasomaji kwanza mjueni huyu Mwinchande ni nani hasa na ametoka wapi.
  Ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa mtumishi serikalini kwa muda mrefu. Aliteuliwa na rais baada ya kupendekezwa jina lake na CCM, kama mmoja wa makamishna wawili wa Tume kutoka CCM kwa ajili ya kusimamia uchaguzi mkuu wa 2005.
  Tume hiyo, chini ya Mwenyekiti Masauni Yussuf Masauni, ofisa mstaafu wa Idara ya Uhamiaji ilishutumiwa kwa kutenda kwa maelekezo ya CCM na serikali yake na ilithibitisha hilo kwa kulalamika katika ripoti yake baada ya uchaguzi, kwamba pamoja na matatizo mengine, iliingiliwa kiutendaji na serikali na taasisi zake nyakati tofauti za mchakato wa uchaguzi.
  Hivyo, Mwinchande, kada mzuri wa CCM, anaongoza tume inayotakiwa kufuata sheria na taratibu. Lakini hii ni tume ambayo inaendeleza watendaji wa kiutawala waliopo tangu 1995. Nasema Mwinchande, kada mzuri wa CCM, anaongoza tume ambayo rekodi yake ya utendaji ni mbaya.

  Tangu uchaguzi wa 1995 wakati Mwenyekiti alipokuwa Zuberi Juma Mzee,(nimepata habari kutoka zanzibar kuwa huyu jamaa saivi anaokota makopo) msomi wa stashahada (diploma) ya sheria ya Chuo cha Mzumbe, hadi uchaguzi uliopita, tume ilikumbwa na tuhuma na shutuma nyingi za utendaji mbovu na uliojaa udanganyifu na upendeleo kwa Chama cha Mapinduzi.
  Lazima niseme, Tume hii haijatenda kosa lolote kwa mtazamo wa CCM, chama ambacho kiongozi wake mwandamizi mwaka 1995, alikataa matokeo ya uchaguzi wa rais, wakati tukisubiri yatangazwe na Mwenyekiti Zuberi, lakini yalipotangazwa tu yakionyesha kuwa wameshinda, aliyakubali, na haraka akatimikia ofisini Kisiwandui ambako alipofuatwa, alijitetea; “hata angekuwa nani angebadilika.”
  Duru za kiusalama wakati ule wa kusubiriwa matokeo ya urais, zilisema matokeo halisi yaliyokusanywa kwenye vituo vya uchaguzi yalionyesha CCM imeshindwa. Haya ndiyo matokeo yaliyotangazwa na kituo cha televisheni cha Dar es Salaam (DTV) ambayo yalikuja kukanushwa na Tume na serikali na hatimaye kituo hicho kuadhibiwa

  N.B
  hii ni sehemu ya makala ya mwandishi Jabir Idrissa kutoka zanzibar, katika gazeti la Mwanahalisi katika toleo lililopita.
  Msisitizo ni wangu.
   
 2. C

  Calipso JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wazenji wanamjua vizuri huyo muheshimiwa kwa ukada wake wa ccm... bora moto kwake lkn ccm iwe juu..
   
Loading...