TUME YA AJIRA: Mnamaanisha nini hapa???

GP

JF-Expert Member
Feb 5, 2009
2,049
160
"Applicants for entry levels currently employed in the Public Service should not apply, they have to adhere to Government Circular Na. CAC. 45/257/01/D/140 dated 30th November 2010"

AU
"Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010"
wakuu,
mara nyingi tume ya ajira katika utumishi wa umma huwa wanaweka vipengele hivyo hapo juu,
sasa sijui walikua wanamaanisha nini hapa?, na hii CIRCULAR kama kuna mtu anayo basi naomba anisaidie nijionee mwenyewe.
 
Sasa usichoelewa nini? Maana yake USIOMBE kama unaangukia hapo, na 7bu ndo hyo, katafute maelezo zaidi kwenye waraka kumbukumbu hyo hapo walokuandikia/ambatanisha.
 
Sasa usichoelewa nini? Maana yake USIOMBE kama unaangukia hapo, na 7bu ndo hyo, katafute maelezo zaidi kwenye waraka kumbukumbu hyo hapo walokuandikia/ambatanisha.
ishu ni kwamba kuna watu ambao wao wameajiriwa sehemu kama vibarua au tempo yani hawana ajira ya kudumu kwenye taasisi za serikali. kwa mfano utakuta mtu kamaliza shule na kaomba sehemu kama tfda tempo akapata na akawa anafanya kazi akilipwa kama mfanyakazi wa muda mfupi.
je mtu kama huyu kifungu hiki kinamuhusu??
 
serikali haina akili
mimi nimeajiriwwa kwa DIP ya Ualimu.......
sasa nina SHAHADA YA UHASIBU NA FEDHA......................

they are fuxxxiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiinnnnnnnnnnnnnnnnnnnggggggggggggggggggg
 
ishu ni kwamba kuna watu ambao wao wameajiriwa sehemu kama vibarua au tempo yani hawana ajira ya kudumu kwenye taasisi za serikali. kwa mfano utakuta mtu kamaliza shule na kaomba sehemu kama tfda tempo akapata na akawa anafanya kazi akilipwa kama mfanyakazi wa muda mfupi.
je mtu kama huyu kifungu hiki kinamuhusu??

huyo mtu serikali haimtambui, kwahiyo anatakiwa aombe ili apate ajira nakisha serikali imtambue.
 
huyo mtu serikali haimtambui, kwahiyo anatakiwa aombe ili apate ajira nakisha serikali imtambue.
there you are mkuu!,
ndio sasa yeye anataka kupata ajira sasa iliyo rasmi hapo hapo kwenye hiyo taasisi.
sasa hawa jamaa wa tume ya ajira kuna kipengele kingine wanaruhu mtu ambae ameajiriwa lakini anataka kubadili fani tofauti na ile aliyopo kitu ambacho naona sio sawa sana kivile.
 
ishu ni kwamba kuna watu ambao wao wameajiriwa sehemu kama vibarua au tempo yani hawana ajira ya kudumu kwenye taasisi za serikali. kwa mfano utakuta mtu kamaliza shule na kaomba sehemu kama tfda tempo akapata na akawa anafanya kazi akilipwa kama mfanyakazi wa muda mfupi.
je mtu kama huyu kifungu hiki kinamuhusu??

Kwa hiyo kiingereza hujaelewa na kiswahili hakipandi?

Kama wewe ni mwajiriwa wa serikali au idara zake, USITUME MAOMBI. Hii ni kupunguza kero ya vijitu vinavyohama hama bila msingi kwa kazi ile ile. Kama wewe ni messenger wizara ya afya unaomba u-messenger wizara ya kilimo ili iwe nini wakati kuna watu hawana ajira? Pili, unapoacha kazi kule wizara ya afya unaisumbua serikali ile ile kuajiri messenger mwingine.

Sasa kama tempo ni ajira utajua wewe na uzito wako wa kuelewa
 
ishu ni kwamba kuna watu ambao wao wameajiriwa sehemu kama vibarua au tempo yani hawana ajira ya kudumu kwenye taasisi za serikali. kwa mfano utakuta mtu kamaliza shule na kaomba sehemu kama tfda tempo akapata na akawa anafanya kazi akilipwa kama mfanyakazi wa muda mfupi.
je mtu kama huyu kifungu hiki kinamuhusu??

Ndugu yangu,
Hicho kipengele ni muhimu sana na ni msaada kwetu tusio na ajira. Nini maana ya kipengele hbicho?! Assume wewe umemaliza BCom Accoounts na ukaajiriwa kama Accountant II (Hiyo ndo Entry Level yenyewe) Halmashauri ya Misungwi. Kisha, serikali wanatangaza nafasi za kazi Accontant II Wizara ya Fedha....na wewe kwa kuona huko kuna deal, unaamua kuomba ili ukimbie Misungwi....kutokana na kipengele hicho maana yake ni kwamba hauruhusiwi kwavile huku mtaani kuna watu wanaitafuta hata hiyo ya Misungwi lakini hawajaipata!!! Alternatively, inawezekana umeajiriwa kama Mhasibu II anywhere serikalini, na mara serikali inatangaza nafasi za Wkaguzi wa Mahesabu (Auditors II)....wewe kwa kuona kwamba Auditor ni deal kuliko Mhasibu; unaamua ku-apply hiyo nafasi ya U-Auditor wakati tayari ni Mhasibu....Kwa mujibu wa kipengele hicho; hairuhusiwi!

IN addition, huyo kibarua au wa tempo, haguswi na kipengele hicho! Je, hicho kipengele ni muhimu au sio muhimu?!
 
there you are mkuu!,
ndio sasa yeye anataka kupata ajira sasa iliyo rasmi hapo hapo kwenye hiyo taasisi.
sasa hawa jamaa wa tume ya ajira kuna kipengele kingine wanaruhu mtu ambae ameajiriwa lakini anataka kubadili fani tofauti na ile aliyopo kitu ambacho naona sio sawa sana kivile.

Hata hapa ndugu yangu bado haupo sahihi!!!
Maana ya kipengele hicho ni kwamba.....Uhalisia wake ni huu.....Assume uliajiriwa kama Afisa Kilimo wakati ukiwa na Diploma in Agriculture. Lakini, ukaenda SUA na kuchukua BSc. AgroEconomics na baada ya ku-graduate na kurudi kazini kwako bado ukaendelea kutumikia kama Afisa Kilimo! Mara, Tume ya Ajira wakatangaza nafasi za Economist II, ambapo mtu wa BSc. AgroEconomics ana sifa za kuomba! Kutokana na kipengele hicho; ha;po huyo mtu ni ruksa kuomba hiyo post ya Economist II ! Lakini Say, uliajiriwa kama Afisa Kilimo (Agricultural Officer III) mwenye Diploma; kisha zikatoka nafasi za Extension Officer III....hapo, HAPANA!!! Lakini kama ni wewe ni Agricultural Officer III (ulikuwa na Diploma) kisha ukaenda kusoma na kupata degree na zikatangazwa nafasi ama za Agricultural Officer II OR Extension Officer II....HAPO, RUKSA KUOMBA!
NGOJA nikuambie kitu kimoja! Kabla ya utaratibu huu; kulikuwa na idadi kubwa tu ya wafanyakazi wa serikali ambao walikuwa wanazunguka tu kutoka idara moja hadi nyingine; au wizara moja hadi nyingine! Unakuta mtu ameajiriwa kama Economist II Wizara ya Jinsia; kisha anaona nafasi Wizara ya Fedha; basi anaamua kuomba Wizara ya Fedha wakati tayari ana ajira !!
 
there you are mkuu!,
ndio sasa yeye anataka kupata ajira sasa iliyo rasmi hapo hapo kwenye hiyo taasisi.
sasa hawa jamaa wa tume ya ajira kuna kipengele kingine wanaruhu mtu ambae ameajiriwa lakini anataka kubadili fani tofauti na ile aliyopo kitu ambacho naona sio sawa sana kivile.

jaman kwanin m2 usibadili? Mi naona sawa, mfano nlikuwa afisa maendeleo bt kazi nliobobea sana ni afisa habari na zimetoka mayb nying tu, sasa ndipo hapo napata chance ya ku apply ili nfanye kaz nliobobea zaidi.
 
................
NGOJA nikuambie kitu kimoja! Kabla ya utaratibu huu; kulikuwa na idadi kubwa tu ya wafanyakazi wa serikali ambao walikuwa wanazunguka tu kutoka idara moja hadi nyingine; au wizara moja hadi nyingine! Unakuta mtu ameajiriwa kama Economist II Wizara ya Jinsia; kisha anaona nafasi Wizara ya Fedha; basi anaamua kuomba Wizara ya Fedha wakati tayari ana ajira !!
asante sana ndugu yangu kwa kunipa shule moja nzuri kwa maelezo yako mazuri nimekupata mwanzo mwisho!.
 
Back
Top Bottom