Tume maadili: Viongozi wa serikali kukaripiana ama kuitana kama mbwa ni dalili mbaya

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,221
Tume ya maadili tunaomba mkae na na viongozi wakuu wa kitaifa na muwape darasa jinsi yakuongea tone yakuongea either na wananchi au wenyewe kwa wenyewe.
Sijuwi tabia hii wameipata wapi lakini hata Rais hana tone inatumika na wasaidizi wake.
Mfano mzuri ni hata jana mkuu wa mkoa aliongea tone kali na ya hisia kiasi kama watu walisinyaa. Lakini ukimsikiliza yule katibu ofisi ya rais alionga tone ya unyenyekevu sana na ndivyo wanapaswa kuwa.
Ukiacha hilo angalia mawaziri na wakuu wengine wamikoa kiukweli wanaongea tone za ajabu kali na misuli inawatoka wakifikiri ndio njia yakifikisha ujumbe but unaweza kuona wala hawafikishi ujumbe ila wanaleta hofu zisizo za msingi.
Nilazima wakuu wa mikoa,mawazir,wakuu wa wilaya kuongea tone za viongozi na sio kama wanaongea na wafungwa ama wahalifu. Nilazima wakumbuke wanaongea na wananchi walio waweka madarakani na wawapende na kuongea nao kwa upendo.

Hivi majuzuz kumetokea tukio la spika kumuita CAG kama anaita mbwa au kitu gan ile sio sawa hata kama alikuwa na hasira nilazima akumbuke cag ni mkubwa kuliko yeye na anastaili heshima na utu. Nimemsikiliza cag hakuongea kwa jaziba kama spika alivyo ongea ila ukweli utabaki kuwa ukweli sio spika tu hata viongoz wengine wanaita wenzao kwa masauti ya kama wanaita Mbwa.
Serikali nilazima iwe maana ya umoja wetu mkiruhusu watu kutwezana na kudharauliana ni hatari na kitisho kwa usalama wa nchi.
Tutafaka kama mkuu angewaita wakuu wa majeshi kwa tone wao wanatumia kuitana sijuwi ingekuwaje.
Nilazima viongoz waheshimiane na kupendana kuleta umoja wa kitaifa.
Asante
 
Sasa umuhimu wa semina elekezi unaonekana, wakati wa Mh Kikwete tuliona kama uhalinifu wa fedha lakini semina hizi muhimu, pili umuhimu wa kuteua watu wenye uzoefu na utumishi unaonekana sawa MF. katika utumishi Wakurugenzi wa Halmashauri (DED) sharti awe amewahi kuwa Mkuu wa idara katika utumishi, kkwa sasa tuna watu wametoka katika makampuni ya kikaburu, bila maelekezo hali itakuwa mbaya zaidi ya hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni maoni yako (uonavyo) na hivyo unayaelekeza kwa Tume ya Maadili ya viongozi wayafanyie kazi au haya yamesemwa na Tume yenyewe?

All in all, ulichokiandika bila kujali ni maoni yako ama yamesemwa na Tume, kwa kweli hii ndiyo hali halisi tunayokabiliana nayo toka kwa viongozi wetu karibu 80%.....

Yaani muda wote wanapoongea ama kutoa maelekezo kwa walio chini yao ama hata kwa wananchi, ni full hasira tu....

Wengi hawajiamini na muda wote hudhani wanadharauliwa

Na ili kuonesha kuwa wao siyo wa kudharauliwa, ni amri mbele kwa mbele.....

Na ukizubaa na kukaa vibaya tu, sheria ya 48hrs mahabusu ya polisi inakukumba palepale.....!!

Awamu hii kuna pepo mbaya sana anasumbua na anaielekeza nchi kwenye kibri
 
Ni maoni yako (uonavyo) na hivyo unayaelekeza kwa Tume ya Maadili ya viongozi wayafanyie kazi au haya yamesemwa na Tume yenyewe?

All in all, ulichokiandika bila kujali ni maoni yako ama yamesemwa na Tume, kwa kweli hii ndiyo hali halisi tunayokabiliana nayo toka kwa viongozi wetu karibu 80%.....

Yaani muda wote wanapoongea ama kutoa maelekezo kwa walio chini yao ama hata kwa wananchi, ni full hasira tu....

Wengi hawajiamini na muda wote hudhani wanadharauliwa

Na ili kuonesha kuwa wao siyo wa kudharauliwa, ni amri mbele kwa mbele.....

Na ukizubaa na kukaa vibaya tu, sheria ya 48hrs mahabusu ya polisi inakukumba palepale.....!!

Awamu hii kuna pepo mbaya sana anasumbua na anaielekeza nchi kwenye kibri
Kuanzia makatibu tarafa wanatembea kwenye misafara yake na Polisi,tena Inspector. Anampa Amri tu bila kujali kuwa amemzidi elimu cheo hata umri. NCHI HII BHANA!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa amri za hovyohovyo viongozi wa awamu ya tano wanajiweza.Ila akili za kuwaletea wananchi maendeleo ni ziro kabisa.
 
Umeandika vizuri lakini umekosea sehemu moja tu. Rais ndie mwasisi wa hiyo kitu. Hata yeye anaependa hivyo. Amini nakuambia atadumu sana yule anaeonesha ukali katika utawala huu. Ili udumu au upandishwe cheo awamu hii Fanya
1. Hakikisha upinzani hawapumui hata kwa kuwaonea makusudi.
2. Uwe jifanye mkali hata kwa kufeki ndio maana hata wale unaowajua walikuwa Wapole na adabu now ni makelele tu.
3. Jitangaze lakini usimzidi boss wako.
4. Mwaga sifa za kutosha kwa Boss hata kwenye mambo madogo tena hapo ita kameras wakati ukisifia.
Nakuhakikishia atadumu na kama kunakiongozi yupo humu anasoma hii comment yangu nakuambia Usihangaike kuroga Fanya hayo tu umefanikiwa.

Boss mwenyewe ndivyo anavyofanya kwani mtoa mada ni kipofu au kiziwi???
 
Wale jamaa ambao msemaji wao aliwahi kusema "sadism is inevitable when situation is alarming , atakuja kuwahadithia kitakachompata" ndio peeke wanaotakiwa kubaki na kauli kali wengine weka pembeni kule.
 
Back
Top Bottom