PreGE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yaongeza siku mbili uboreshaji daftari la wapigakura Dar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
JAJI.jpg
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeongeza siku mbili (Machi 24 na 25) za uboreshaji wa daftari la mpigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi.

Taarifa ya INEC imetolewa leo Machi 23, 2025 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Jacobs Mwambegele ikiwa ni siku moja tangu Mwananchi iripoti wingi wa watu vituoni na malalamiko ya baadhi kushindwa kuboresha taarifa zao.

1742733565562.png
Soma: Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Dar es Salaam Kufanyika Machi 17-23, 2025. Wapiga Kura wapya 643,420 kuandishwa

Uboreshaji wa taarifa huo awali mkoani Dar es Salaam ulianza Machi 17 na ulitakiwa kumalizika leo Jumapili Machi 23, 2025.

"Kama mnavyofahamu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na hatua ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ambayo kwa mujibu wa ratiba ilianza Machi 17, 2025 na ilitarajiwa kukamilika Machi 23, 2025."

"Kutokana na mwitiko mkubwa Tume ilichukua hatua za kuongeza mashine za bvr kits pamoja na watumishi katika maeneo yote yaliyoonekana kuwa na watu wengi na hatua hii imewezesha shughuli hiyo kuendelea kwa utulivu katika maeneo yote. Hatua hiyo imewezesha kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi na kupunguza kwa kiasi kikubwa misongamano kwenye baadhi ya maeneo,"
imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: "Licha ya hatua zilizochukuliwa na Tume, bado katika maeneo kadhaa kuna mwitikio mkubwa wa wananchi. Hivyo basi, napenda kuwatangazia wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa Tume imeongeza siku mbili za uboreshaji wa daftari kwa Machi 24 na 25, 2025."

1742733213252.png

1742733223461.png

1742733232307.png
 
Hawa na NIDA wanapenda tu kusumbua wananchi na kusababisha kuingia kwenye nchi ambazo hazina Furaha Duniani.

Mnapangisha watu foleni wakati kura wanawapigia ninyi.

Mnashindwa nini kufanya hili zoezi kua endelevu?
 
Hii ni huru kwa kumaanisha wateule hawajachaguliwa na washindania au ?? Wateule kwa kumaanisha nini??watu wa dini au?? Kama mwenyekiti wake anachaguliwa na washindania basi hapo ni sawasawa na kuchezea pesa ya walipa kodi bila sababu huku mkifungia biashara na mitaji ya watu kwa ajili ya upumbavu .........
 
Mm mara ya kwanza nilijiandikisha ili nipate kitambulisho tuu, ila sasa hv nna nida hvy siwezi kujiandikisha kwenye huo ujinga mana ht hvy sijawahi na sion umuhimu wa Mm kupiga kura
Umuhimu upo mkubwa sn, wabunge wa upinzani ni nguzo kubwa sn, zinapitishwa sheria za hovyo hovyo hakuna hata mmoja wa kupinga
 
Hii ni huru kwa kumaanisha wateule hawajachaguliwa na washindania au ?? Wateule kwa kumaanisha nini??watu wa dini au?? Kama mwenyekiti wake anachaguliwa na washindania basi hapo ni sawasawa na kuchezea pesa ya walipa kodi bila sababu huku mkifungia biashara na mitaji ya watu kwa ajili ya upumbavu .........
Solution ni nini?
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeongeza siku mbili (Machi 24 na 25) za uboreshaji wa daftari la mpigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi.

Taarifa ya INEC imetolewa leo Machi 23, 2025 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Jacobs Mwambegele ikiwa ni siku moja tangu Mwananchi iripoti wingi wa watu vituoni na malalamiko ya baadhi kushindwa kuboresha taarifa zao.

Soma: Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Dar es Salaam Kufanyika Machi 17-23, 2025. Wapiga Kura wapya 643,420 kuandishwa

Uboreshaji wa taarifa huo awali mkoani Dar es Salaam ulianza Machi 17 na ulitakiwa kumalizika leo Jumapili Machi 23, 2025.

"Kama mnavyofahamu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na hatua ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ambayo kwa mujibu wa ratiba ilianza Machi 17, 2025 na ilitarajiwa kukamilika Machi 23, 2025."

"Kutokana na mwitiko mkubwa Tume ilichukua hatua za kuongeza mashine za bvr kits pamoja na watumishi katika maeneo yote yaliyoonekana kuwa na watu wengi na hatua hii imewezesha shughuli hiyo kuendelea kwa utulivu katika maeneo yote. Hatua hiyo imewezesha kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi na kupunguza kwa kiasi kikubwa misongamano kwenye baadhi ya maeneo,"
imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: "Licha ya hatua zilizochukuliwa na Tume, bado katika maeneo kadhaa kuna mwitikio mkubwa wa wananchi. Hivyo basi, napenda kuwatangazia wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa Tume imeongeza siku mbili za uboreshaji wa daftari kwa Machi 24 na 25, 2025."

Maigizo tu 😂😂😂. Tume huru ambayo haina uhuru
 
Back
Top Bottom