Tumbo kujaa Maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumbo kujaa Maji

Discussion in 'JF Doctor' started by Mazogola, Jun 7, 2012.

 1. Mazogola

  Mazogola Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hi Wanajamii habari za asubuhi
  jamani ninapenda kama kuna watu wanaweza kuelewa hii kitu ni kuwa kuna shemeji yangu ana jawa na maji tumboni walienda kupima wakaambiwa milija fulani hivi haifanyi kazi. Sasa nlitaka kujua tiba ya hii kitu halafu nijue chanzao chake ni nini
  Please kama kuna wataalam wanaolijua swala hili embu nijuze
  n.
   
 2. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Shemeji yako:
  1. Ni wa jinsia gani?
  2. Ana miaka mingapi?
  3. Alianza kupatwa na tatizo hilo tangu lini?
  4. Huwa anapendelea kutumia pombe?
  4. Hali yake ya sasa ipoje, amelazwa hospitali au yupo tu nyumbani?
  5. Ana uzito wa kilo ngapi?
  Jitahidi nijibu maswali hayo na nitarudi tena.
   
 3. Baba Sharon

  Baba Sharon JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mazogola thanks a lot nimekutana na hii thread hapa............Mzee wangu nae anatatizo kama hilo na limemuweka KCMC wiki ya tatu sasa..........Yeye alikuwa na Hernia na akafanyiwa operation baada ya Operation tatizo la tumbo kujaa maji likaanza likiambatana na vichomi vikali........mwanzoni tulidhani tumbo linajaa gas ila tulipompeleka KCMC wakatuambia tumbo linajaa maji..wiki ya tatu sasa hajapata nafuu na utumbo umevimba kwa sababu hali chakula.............Kesho wanamrudisha theater kwa ajili ya upasuaji sasa sijui wanairudia ile ya mwanzoni ama vipi..........maana wanasema daktar aliyemfanyia ya kwanza kuna mishipa ya maji aliikata.WENYE KUJUA WATUSAIDIE.....Mi mzee wangu anateseka sana
   
 4. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Please kama kuna wataalam wanaolijua swala hili embu nijuzen.

  Baba yako:
  1. Ana miaka mingapi?
  2. Alianza kupatwa na hernia tangu lini?
  3. Huwa anapendelea kutumia pombe?
  4. Ana uzito wa kilo ngapi?
   
 5. Mazogola

  Mazogola Member

  #5
  Jun 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  1. Ni wa kike
  2.Ana Miaka 21
  3. alianza kupatwa na tatizo hili mwaka huu ka miezi 3 nyuma
  4.Hatumii kilevi cha aina yoyote
  5. Hali yake kwa ss sio nzuri kwani moyo pia unaaanza kuuma
  6. Ana uzito wa kili 55
   
 6. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Swali la tano nilitaka kujuwa hali yake, pia endapo amelazwa hospitali au kuna dawa gani anatumia, anatembea peke yake?. Niandikie namba yake ya simu nimpigie binafsi.

  Nyumbani | maajabuyamaji.net
   
 7. k

  kisukari JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,757
  Likes Received: 1,046
  Trophy Points: 280
  kwa upande mwengine kama unajua,ungeelezea humu kidogo ili na sisi tuelimike.kwani mengine tunajifunza humu humu
   
 8. Baba Sharon

  Baba Sharon JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mkuu mzee ana miaka 58 sasa na not less than 50 kg maana amepungua kwa sababu ya haya maradhi............hatumii wala hajawahi kutumia kilevi..............Hernia ilimuanza kama mwka mmoja uliopita tunazungumzia mwaka 2010 mwishoni ndo matatizo ya Hernia yalimuanza
   
 9. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Tayari nimeku-PM mkuu, uguza pole.
   
 10. Baba Sharon

  Baba Sharon JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Thanks kaka nimeipata............naifanyia kazi
   
 11. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kaangalie moyo au ini!! cardiac failure, liverchirrosis, hali hiyo huitwa edema. pia yaweza kuwa cancer
   
 12. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,497
  Likes Received: 5,979
  Trophy Points: 280
  tatizo la kujaa maji tumbo husababishwa sana na protini kupungua kwenye damu, mfano1 maini hutengeneza protini na pombe huwa ina haribu maini kwa hiyo maini yakiharibika protini kwenye damu hupungua na kusababisha maji kutoka kwenye mirija ya damu na kujaa tumboni, mfano2 mtoto mwenye kwashakoo huwa amepungukiwa protini hivyo unakuta mtoto kakonda mbavu tupu ila tumbo kubwa mfano3 huyo ambaye babaake kafanyiwa upasuaji itakuwa mirija ya lymph imekatika ambayo husafirisha protini kwenda kwenye damu hivyo protini kupungua kwenye damu na kusababisha tumbo kujaa. kunasababu zingine pia kama mtoa mada tatizo litakuwa ni moyo yaani unashindwa kusukuma damu fresh hivyo inajaa mishipani sasa mishipa ili ijiokeo kupasuka inavujisha maji. matibabu makubwa ni kufanya tapping ya hayo maji wanakutoboa tumbo na kutoa maji. nahisi nimeeleweka.
   
Loading...