Tumaini letu liko wapi?

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,655
Unaweza kusema unampenda mtu kisha ukamuongoza katika njia zisizofaa? Unaweza kusema unampenda mtu kisha anapokosea unakaa kimya? Unaweza kusema unajali? Je huu ni upendo wa kweli?

Wenye upendo wa kweli wanapenda kuona mwisho mzuri wa watu wao. Wenye upendo hawataki kumuona mtu akipotea. Wanapenda kuona ukiendelea vizuri kiroho na kimwili.

Wakati mwingine watu hutuchukia kwa kusema ukweli. Wanatuona wabaya kwao. Lakini tunavumilia kwa matumaini. Tukiamini siku moja kaka zetu au Dada zetu wataona mwanga.

Sitakuwa mwamume kama nitakuwa na mpenzi wangu kisha nikamwongoza katika njia zisizofaa. Nguvu yangu itakuwa wapi? Mwanaume ni mlinzi wa mwanamke, na sio mwangamizi. Ni lazima tujifunze kulinda maisha sio kuyaangamiza.

Matumaini yetu yapo kwenye kutenda yaliyo mema. Tujenge familia zetu katika umoja na upendo. Tusamehe kaka na Dada waliotukosea. Tumaini letu limisimamia wapi? Sio kwenye familia imara? Na bila familia imara kuna taifa litakalo simama?

Unaporudi nyumbani kwenye familia yako unajisikiaje? Kuna Matumaini? Kuna upendo? familia iko moja? Uko comfortable kuwa home? We ruin every best things in our lives. Je sisi ni Wenye busara? Ni Wenye hekima kuliko Mungu? Tunaweza kushindana nae? Where do we get our strength and our hope?

Umeishawahi kujiuliza ukifa utaacha nini duniani? Kitu gani chema utakiacha ili kiwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo? Au utaacha unstable family na watoto wasio na mwelekeo. Tumaini letu liko wapi? Au ukifa ndio watoto wako wanasambaratika?

Unadhani waliosema tafuta busara kuliko Mali ni wajinga? Kwanini binadamu wanatafuta Mali kuliko busara? Hawajui kwamba busara ndio mwongozo hutusaidia kufanya maamuzi yenye faida za mbeleni?

Sio kwa kutenda yaliyo haki na sahihi tunasimika miguu yetu sehemu iliyosahihi na salama? Kwanini tusibadili njia zetu? Ni nini misingi ya Matumaini yetu?

Penda familia yako na tenda kilicho chema kwaajili ya familia yako. Penda na mke wako. Rudisha akili zako.
 
Ukimpenda mtu hautakubali kuharibu maisha take ya baadae, hautamuacha akajihusisha na mambo yanayoharibu au kuchangia kuharibu tabia njema.
Mfano, toka nilipokua shule nilidhamiria kutokujihusisha na mapenzi ya aina yeyote kabla ya ndoa, nikiamini kwamba yeyote ntakaemfanyia hivyo ni kuharibu future yake kwa vile sikua tayari kuoa kwa wakati huo.
Hautakubali kujihusisha na biashara za madawa ya kulevya kwa vile zinaharibu vijana wetu na taifa kwa ujumla.
Hautajihusisha na ufisadi na rushwa kwa sababu utawakosesha watu haki zao stahiki.
Lakini ili kuyaweza haya yote, hofu ya Mungu inahitajika sana.
Tumaini language liko kwa Mungu pekee, na nna amino kwamba nilikuja duniani bila chochote na ntaondoka nikiwa sina kitu. Haina haja ya kuchukia watu au kuwasababishia matatizo wengine.

Kuwa na Amani na watu wote ni vigumu sana, lakini inawezekana.

Tupende familia zetu na kuwajali wengine, hapo ndipo tutakapokua na Amani na furaha ya kweli na inayodumu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom