Tuliza Moyo Habiba - (Ombi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuliza Moyo Habiba - (Ombi)

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 18, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 18, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,069
  Likes Received: 5,194
  Trophy Points: 280
  Tuliza moyo habiba, moyo wako na upoe,
  Upunguzie shuruba, hofu yote iondoe,
  Penzi letu sio haba, huzuni yako itoe,
  Tuliza moyo habiba, Penzi letu limeshiba!

  Tuliza moyo habiba, ni mbali tumetokea,
  Tumeyaona ya huba, ya penzi lilokolea,
  Na mengine yenye miba, maumivu kuletea,
  Tuliza moyo habiba, Penzi letu limeshiba!

  Tuliza moyo habiba, ya zamani yamepita,
  Uchungu tusije beba, mbeleni tukaja juta,
  Tusikijaze kibaba, kwa yale yanayopita,
  Tuliza moyo habiba, Penzi letu limeshiba!

  Tuliza moyo habiba, wenye kusema waseme,
  Wanajifanya swahiba, sumu yao waiteme,
  Yarabi twalia toba, hawa ni mapaka shume,
  Tuliza moyo habiba, Penzi letu limeshiba!

  Tuliza moyo habiba, penzi letu likolee,
  Wa mbinguni yeye Baba, dua zetu apokee,
  Atujaze mara saba, penzi letu lendelee,
  Tuliza moyo habiba, Penzi letu limeshiba!

  Tuliza moyo habiba, la moyoni nimesema,
  Busu langu liwe tiba, likutakialo mema,
  Moyoni ninakubeba, u mawazoni daima,
  Tuliza moyo habiba, Penzi letu limeshiba!

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  MwaKjj hongera kwa tungo hii, kuna mdada hapa JF, nijui status yake wala yako katika mahusiano ya kimapenzi, ila naona kama mngefaana sana na ingependeza kama huu utungo ungeudedicate wake.
   
 3. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Nina wazo. Kutokana na baadhi ya wana jf kuonyesha kipaji cha kuandika mashairi, kwa nini tusianzishe kamtindo ka kuchagua mada halafu kila mpenda kuandika shairi anaandika shairi lake kuhusu hiyo mada? Nafikiri hii style itachangamsha zaidi utundu wa mashairi, zaidi ya kumsubiri mkjj atoke halafu ndio ajibiwe.

  Pengine tunaweza kutengeneza kitabu cha jf mashairi na kupeleka huko mashuleni kitumike. Who knows?

  Ni wazo tu!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Apr 18, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,069
  Likes Received: 5,194
  Trophy Points: 280
  Yeah.. I dedicate this one to her..! (I really don't know which one..)
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  nakunong'oneza na usimwambie mtu, dedicated kwa mwanadada jasiri 'Mwafrika wa Kike'.
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,417
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  ya hands are full, stop pushin ya way in like a bull,
  just like me you do, silently i act cool,
  no more school to you, in court the ball is with you,
  mkjj you rule, but careful as you eat ya gruel.

  SteveD. (Echo from the trench)
   
 7. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  habiba wangu jamani, mbona wanitesa wangu moyo
  wajua ninavyo kutamani, mbona waumiza yangu roho
  kipenzi changu cha thamani, mbona wanyanyasa pangu koo
  habiba wangu wa amani, nini nimekutenda wangu polo?

  habiba rudi kwangu jamani, haki napatwa na masimanzi
  chonde chonde tafadhali, lako tamu penzi bado nalihitaji
  usiku wapita mwenzio silali, nakuwaza wangu manzi
  habiba wangu asali, nini nifanye tafadhali?

  kumbuka mengi twafanya, tuwapo pamoja mahala
  nguruko pale tulichofanya, miili yetu tulitoa kafara
  utamu wetu ulichanganya, chini ulitaka galagala
  habiba wangu wa chanya, nini chakutia hasara?

  usiku wa harusi ya dadayo, kawe rumba tulicheza
  kisha tukafuatilia yafuatayo, pata chumba hatukuweza
  tukaishia kwenye uzio, ngoma yetu tamu tukacheza
  habiba wangu wa enzio, nini nifanye wangu pweza?

  kuendelea siwezi tena, naomba nifikirie kwa undani
  mwenzio nashindwa hema, naomba nijie kitandani
  hakika vizuri nitakutenda, naomba ikuingie kichwani
  habiba wangu nakupenda, nini wataka wangu wa ubani?
   
 8. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0


  Mkuu,


  Umetulia mwanakwetu.
   
 9. C

  Choveki JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2008
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tuliza moyo habiba, mwenziyo amekuomba
  Siye twajua ka kwiba, na sasa anajikomba
  Pia amuomba Toba, ahisi ume m-bamba!
  Bi Habiba mi nasema, uliza kwani kunani?

  Anaanza kwa upole, ahisi ushagundua
  Uhuni wake wa kale, adhani umejulia
  Mabusu hayo chelele, ni nini anafichia?
  Bi Habiba mi nasema, uliza kwani kunani?

  Anajihisi mwenziyo, ila ashindwa tamka
  Achunguza wako moyo, na yepi uta tamka
  Anayahepa machoyo, ya kwake yeshamtoka!
  Bi Habiba mi nasema, uliza kwani kunani?

  Habiba mwana fulani, fungua macho wa kwetu
  Uliza yule ni nani, nimsemaye Sikitu
  muangalie machoni, asije kuficha kitu
  Bi Habiba mi nasema, uliza kwani kunani?
   
 10. BiMkubwa

  BiMkubwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2008
  Joined: Jan 9, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Mahabuba nimeshindwa, moyo wangu kutuliza
  mazito nalemewa, iweje leo waniuliza
  uchungu nahemewa, na yako miujiza
  moyo hauwezi tulia, na penzi lisiloshibisha

  Mbali tumetokea, iweje leo ukumbuke
  kwa yale yaliyotokea, lazima ugutuke
  hofu imenienea, natafuta mahala niruke
  moyo hauwezi tulia, na penzi lisiloshibisha

  penzi lazima lishibishe, iwe kwako iwe kwangu
  nani akueleweshe, matendo yako uchungu kwangu
  kidonda usinitoneshe, ubichi bado kwangu
  moyo hauwezi tulia, na penzi lisiloshibisha

  kurudi kwako asilani, hata kwa maneno matamu
  nisijeonekana hayawani, penzi limepoteza hatamu
  penzi limepata miwani, penzi pofu sina hamu
  moyo hauwezi tulia, na penzi lisiloshibisha


   
 11. B

  Boma Senior Member

  #11
  Jul 3, 2008
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 190
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du kumbe Mwanakijiji ni hatari kwa mashairi ya mapenzi, siku hizi wanasema umebobea
   
 12. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Wakijiji umelonga,acha nami ninene
  Shairilo limekonga,limelizidi sebene
  Kidogo nataka chonga,Naomba dakika nne
  Kwa Habiba umegonga,Ninaye mwaka wa nne

  Wajificha huko shamba,Habiba wamwacha town
  wakijiji nakuomba,Mwache apate amani
  Huku alipo atamba,Ananipenda Amani
  Kwa Habiba umegonga,ninaye mwaka wa nne

  Habiba alikupenda,na wewe ukamtenda
  Ukamwacha njia panda,ukaamua kuhanda
  Ameamua kuenda,sasa watoka udenda
  Kwa Habiba umegonga,ninaye mwaka wa nne

  Pendo lake Habiba,ni tamu siwezi sema
  Kama chakula nishashiba,mpaka nashindwa kuhema
  Pendo lake kwangu tiba,Mola atupe |Uzima
  Kwa Habiba umegonga,Ninaye mwaka wa nne

  Uchungu ninaupata,Kwa mateso uliompa
  Chalinze mpaka Msata,Shambani ukamtupa
  Ulimfanya Kuruta,kwa kazi ulizompa
  Sasa kwangu amefika,Na kamwe sitamtupa

  Kadi tamati wa tama,Mimi mwisho nimefika
  Habiba ni wangu mama,Moyo wangu kaushika
  wakiji kachunge ndama,Niache mimi na 'mama'
  Kwa Habiba umegonga,ninaye mwaka wa nne
   
 13. B

  BeNoir Member

  #13
  Jul 3, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh!
  Hongera wote mlioonyesha umahiri wenu.
   
 14. b

  bonnie2_s Member

  #14
  Jul 24, 2008
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habiba habebi,haibi hububu,
  wala hatubu kwa uongo kukuhubu,
  hana haiba na mpenda misiba,
  heri yako wewe ushapata mahaba.


  mimi sijawahi kupendwa baba,
  kupata habiba mwenye kwangu huba,
  nimekulia upweke na huzuni nimeshiba,
  tuache hadithi zake mahabuba.

  miaka 18, nitafute tuonane,
  kisha tuelewane kisha tuoane,
  tukaishi saanane tukifa tuzikane,

  nakukumbusha popote ulipo,
  chambi chambicho kificho,
  chambi ukipata chambilecho,
  chambilecho ni kifo ukiwa nacho
  ,
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2008
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,155
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  MHE shairi lako zuri sema tunarudi kulekule you will develop what you practise, ebu soma michango yetu utagundua wabongo tunapenda mapenzi kuliko jambo lolote. ndio maana nchi inauzwa tukiwa tunawaza mapenzi... tutungie shairi la kuponda mafisadi bwana.. hizi za mapenzi waachie akina mr blue na banana zoro
   
 16. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Mimi nimesikia lakini usihofu simwambii mtu
   
 17. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Naunga Mikono na miguu yote
   
 18. C

  Choveki JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  SSSSSSHHHHHHHHHHH!!!!, Msiipaze sauti wakuu, wengine watasikiya.
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,282
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  hahahahahahah!tangaza zabuni tu mkuu
  We will go for the highest bidder!
   
Loading...