Tulivyotapeliwa msibani, tapeli alitumia mbinu rahisi sana kiasi kwamba kila nikifikiria nacheka tu

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,523
27,019
Wananzengo, tuendelee kujilinda na kuwaombea wenzetu.

Maisha yanavyozidi kuwa magumu kila siku watu wanafungua ubongo na kuona fursa mpya, hii yote ni ili kuweza ku-survive. Hivyo majanga kwako wewe ni fursa kwa mwingine, hakuna aliye salama.

Basi bwana, yapata wiki sasa tangu tupate msiba [RIP Mzee wetu], ni maeneo fulani ya kijanja ndani ya jiji pendwa, Bongo Dar es Salaam.

Ilikuwa hivi:

Wakati ambao wengi wa wanafamilia wapo kwenye msafara wa kuupokea mwili kutoka hospitali, na kupitia maeneo ya ibada kabla ya kufika nyumbani tayari kwa kusafirishwa mkoa, alitokea mwamba [tapeli] aliyejivika usamaria wema.

Mwamba akiwa ameshachora ramani nzima, aliibuka nyumbani ambapo aliwakuta watu kadhaa, kwa ujasiri mkubwa akahitaji kuonana na mwenyeji mmoja wa familia ile.

Alichofanya ni kumwambia achukue vijana wawili watatu waongozane naye kwenda dukani kuchukua MCHELE, kusikia neema imeshuka naye bila kusita akafanya hivyo na safari ikaanza.

Kufika dukani mwamba akasema na mangi [taarifa za msiba anazo] kuwa yuko pale kwa niaba ya familia, apime mchele kiasi cha kilo 100, naye bila ajizi akafanya hivyo.

Baada ya kupima mangi akamkabidhi, mwamba akaugawa mchele mafungu mawili, kilo 20 vijana wabebe kupeleka nyumbani na kilo 80 zitasafiri mkoa kwa ajili ya msafara wa mazishi, hivyo bodaboda ili kupeleka kunako gari kumbe ndo katokomea nazo anakojua yeye.

Ikawa imeisha hiyoo.

Baada ya siku mbili tatu za nusu mlingoti, mangi analeta bili ya kilo 100 kwenye kikao cha ndugu.

Watu ooh watu eeeh, wanapigwa na butwaa kilo mia zimetumika wapi, wakikumbuka walivyolala njaa huko malaloni.

Ndipo yule kijana mwenyeji akaelezea mkasa mzima, na kushuhudia kuwa nyumbani waliambulia kilo 20.

Bongo Dar es Salaam ni Chuo Kikuu, kila siku kuna cha kujifunza, ukizubaa tu unawapa watu faida.
 
Kama ni kwel, bas Mashtaka yake yapo mbele za Mungu yanamgonjea. Kwa kila hesabu ya matendo yako ya dhuluma hukumu huwa ipo pale pale, labda atubu mbele za mungu tena kwa damu ya yesu, maana ndiyo inayoleta patanisho, nje ya hapo hamna lolote.
 
Back
Top Bottom