Samahani
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 237
- 355
Baada ya tu ya kupata ajira, nilipata neema ya kukaa nyumba za serikali, wenyewe tulikua tunaziita “kotaz”. Miaka hiyo nyumba hizi zilikuwa zinamilikiwa na serikali hasa, ingawa siku hizi zimeshaanza kuwa za kina “bwana Fulani”.
"Wakati huo", watumishi wa serikali walikaa nyumba za serikali kutegemeana na ofisi wanazofanyia kazi. Nyumba hizi zilifanana sana, na mara nyingi katika nyumba moja zingekaa familia mbili. Kipato chenyewe kilikuwa kinafanana, hivyo maisha nayo yalifanana kwa kiasi kikubwa ukiondoa tofauti ndogo ndogo tu.
Huku tuliishi kama ndugu. Cha mwenzako ungeweza kukitumia kwa uhuru, naye asingesita kutumia cha kwako pia (kasoro mke au mume, tafadhali msinitafutie kes). Nakumbuka hata bibi yenu wakati ule angeweza kubandika nyama jikoni na akamuachia jirani yake ili ahakikishe haziungui. Naye angezitazama kama za familia yake, na kama angepata muda, angemalizia mapishi kabisa. Hizi zilikuwa familia hasa. Nakumbua siku moja nilinyoosha koti langu pekee la heshima nililonalo pasi ili nipeleke posa ya kijana wangu. Wakati nikimalizia maandalizi mengine muhimu, jirani alipita akajivalia na kujiondokea.
Ikala kwangu, ila nikaishia kutabasamu tu.
Maisha yalibadilika baada ya kustaafu. Hapo nikaachia nyumba ya serikali na nikahamia nyumba ya kupanga, tena uswazi kati. Hapo ndipo nilipojua chungu ya maisha. Nyumba yenyewe ingawa ilikuwa na ukubwa wa kiasi tu, ilikuwa na zidi ya wapangaji kumi, tena wote wakiwa familia.
Kuonesha msisitizo, watoto wa kiume wa nyumba ile (na wakwangu wakiwemo) walianzisha timu ya mpira wakaita Nyumbani F.C! Tulikuwa wengi kwelikweli. Kama ungetokea msiba ama sherehe, tungeweza kutengeneza kamati zote muhimu sisi kwa sisi. Asubuhi ingekulazimu ubebe nguo na taulo ukaogee ofisini au kwa jirani. Changamoto ingekuwa ngumu wakati wa kwenda choo.
Huko awali sikuwa naifahamu vizuri maana ya chuki, lakini hapa nikaielewa kwa vitendo nadharia hii. Kina mama walichukina kuliko kawaida. Wakatengeneza “SACCOS” ndogo mdogo za kushambuliana wao kwa wao. Hawa wangeungana wawili au watatu wakawashambulia wengine. Asubuhi huyu angempiga kikumbo mwenzake makusudi ili akijibu wapashe kidogo kwa ngumi nyepesi.
Huyu angenunua kanga yenye maneno “UMEBAKI KUKONDA KWA KUCHUNGUZA YASIYOKUHUSU” na mwenzake angejibu kwa kwenda kununua “WEMBAMBA WA RELI TRENI INAPITA”. Huyu angeweka taarabu ya Shakira Saidi, na mwenzake angejibu na ya Ashura Mwinyiseiph. Chuki ikahamia hadi kwa wanaume na watoto. Nasikia siku moja hata ile Nyumbani F.C walijikuta wakianza kumfunga kipa wao kwa vile jana yake kwao walikula wali mchana na usiku.
Maisha ya nyumba ile yalikuwa magumu kweli. Haikuwa ajabu asubuhi kukuta lundo la kinyesi mlangoni huku mlangoni kukiwa na maandishi “Hii bado ni rasharasha, mvua bado”. Siku moja nilitembelewa na mama mkwe, tena mfukoni nikiwa na mia saba tu. Ikabidi nikope kilo moja ya mchele dukani ili mkono uende kinywani. Wakati wife anashughulikia madikodiko, tukawa ndani tukipiga hadithi mbili tatu na mama mkwe, na baada ya muda naye akaingia ndani akiacha wali uive. Loh! Huko nje si akaja nyang’au mmoja hamnazo? Kimyakimya akamwagia zaidi ya lita moja ya mafuta ya taa (labda ilizidi pia maana......) kwenye wali ule.
Ilibidi tulale tukiingoja kesho yake.
CHUKI ni mojawapo kati ya matatizo makubwa ambayo yanazikabili jamii zetu leo. Wapo watu wanaochukiana kuliko Maelezo. Kuna mtu hayuko tayari kumwona mwenzake akifanikiwa kwa namna yoyote ile. Yupo ambaye yuko tayari hata kupoteza laki mbili kwenye jitihada za kuhakikisha kuwa jirani yake hapati elfu tano, tena akawa na furaha kabisa. Kuna mtu anaweza kutumia siku nzima akieneza chuki juu ya wengine. Kuna mtu anaweza hata achelewe usaili muhimu kwa ajili ya kazi ili tu ahakikishe jirani yake anapata matatizo.
Jamii zinazofanikiwa kupiga hatua kwenye maendeleo zina mengi ya kutufundisha.
Katika upendo tunaweza kufanikiwa kwa mengi. Upendo unaleta ushirikiano. Upendo unadumisha mahusiano. Upendo unapunguza uchungu moyoni. Wanaopendana hawatakiani mabaya. Wanaopendana wanatakian heri na Baraka katika yote. Daima wanayafanya mambo yao kwa ushiriano na wanapiga hatua za maendeleo kwa haraka zaidi. Kitaalamu, uwapo na upendo, daima unadumu furahani, nahii inaongeza hata siku za kuishi.
Kwa kuwapenda wengine, unajiweka hazina ambayo hujui utaitumia lini, na wakati wa kuitumia ufikapo; itakufaa kuliko hata ulivyowahi kutegemea. Unayempenda leo akiwa juani hatasita kukukumbuuka kesho akiwa kivulini. Na ndio maana wahenga tulisema (Hata mimi ni mhenga bwana); “tenda wema nenda zako, usingoje shukrani”. Mtendee mtu wema hata pale anapokuudhi, akikumbuka sawa, asipokukumbuka sawa, lakini hata moyoni mwake hatausahau upendo na wema wako.
Baada ya kusali, kuomba na kufunga sana, siku moja, bwana mmoja aliyekuwa na matatizo chungu nzima alitokewa na Malaika kutoka kwa Mungu. (Niko serious). Ndiyo, malaika Yule alitoka kwa Mungu. Basi bwana, Yule mlalahoi akampokea kwa upendo na bashasha kubwa. Malaika akamwambia;
“Mungu ameisikia dua yako. Omba chochote utakacho utapewa kwa kadiri ya utakavyo, lakini maadui zako wote watapata mara mbili zaidi yako”.
Jamaa roho ikamshtuka pah!
Yani kweli adui zake wapate mara mbili? Yeye akipewa shekeli tatu wenzake wanapata sita. Akipewa nyumba moja wenzake wanapewa mbili. Akipewa msiba mmoja wenzake wanapata miwili. Akiomba gari mbili wenzake wanapewa mbili. Ghafla wazo likamjia, na kwa kujiamini kabisa akamwambia mjumbe yule wa mwenyezi Mungu;
“NITOE JICHO MOJA” ...
Wasalaam..
TIMOTHY PETER KIRAKA MSUYA
timothyzone10@gmail.com
+255 763 305 605 | +255 674 656 539