commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,954
Wadau JF,
Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha kuwa Hai na kuuona mwaka 2016. Pia Namshukuru kwa kuwaweka Hai wote mlio Hai kama mimi.
Naomba kuyatoa machache ninayoyaona kwa kiwango changu kama Changa moto kubwa iliyoko mbele yetu kama watanzania, bila kujali tofauti zetu za kielimu, kimapato,wala kisiasa.
Tanzania ya kabla ya Uchaguzi mkuu wa October mwaka 2015 na Tanzania baada ya October 2015 ni nchi ile ile lakini watu Hakika naona kama si walewale.
Nadiriki kusema haya kwa sababu, wakati kabla ya tar.25 ya mwezi October 2015, kila mtu aliimba mabadiliko na hii
iliongezeka hamasa zaidi pale kada na Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa alipojiengua toka CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chadema.
Kaulimbiu yake ikawa mabadiliko huku wapambe na wafuasi wake wakijibu mabadiliko Lowassa!
Wale waliojaribu kusema hata upande wa CCM una mabadiliko waliaminishwa kwamba ile ni system na haibadiliki na kama mtu angejikuta anapinga hayo mabadiliko ya Lowassa mbele ya wafuasi wake ilikuwa ni nadra kuachwa salama bila shambulio la aibu au hata mkongoto.
Yote haya yalikuwa yanaashiria kuwa watu nchini walikuwa wamechoshwa na hali halisi ya utawala wa awamu ya nne chini ya CCM. Na hawakuwa na Imani nayo Tena kuweza kuwapatia kiongozi mahili mwenye uzalendo na nchi yetu.
Lakini pia MUNGU ana maajabu yake kwani aliweza kuzuia mafuriko kwa mikono na hatimae mwisho wa yote watanzania walimchagua mgombea wa CCM mheshimiwa Dk John pombe magufuli kuwa Rais wao.
Ameingia madarakani na kuanza kazi Rasmi huku akitimiza alichoahidi wakati wa kampeni yake. Ya hapa ni kazi tu.
Ameanza kwa kusafisha uozo wa ufisadi katika sekta muhimu za mapato nchini kama Bandari, Tra, reli na bado vita ndio inaendelea tukiwa sasa sekta ya utumishi wa umma hasa ajira za raia wa kigeni na wahamiaji haramu sambamba na uboreshaji makazi hususan uhamishaji wa makazi hatarishi hasa mabondeni.
Nina Imani zoezi hili muhimu litafuata haki bila upendeleo na kuwachukulia hatua watumishi wa umma watakaobainika kukiuka maadili ya utumishi na kutoa vibali bandia vya ujenzi holela. Na ikibidi kutoa fidia kwa wahanga.
Baada ya hayo Nina hitimisha kwa swali muhimu.
Kama watanzania tulitaka mabadiliko kwa kuchoshwa na matendo ya serikali kufanya kazi kwa mazoea,
Kwa serikali kufumbia macho ufisadi na ubadhilifu wa Mali ya umma, kwa serikali kuwa ya uswahiba nk.
Kwa serikali kutokusanya kodi na hivyo kutoweza kukidhi huduma za muhimu kijamii kama elimu bure, uboreshaji wa ma hospitali yetu.
Sasa tingatinga la kweli linafanya kazi ya usafishaji wa yote haya Tena kwa kasi ya rapid, tumeanza kulalamika kulikoni???
Mbona sasa tunaanza kulalamika??
Mbona wale walio kuwa Mbele kutafuta mabadiliko sasa wamekuwa wa mwisho kuyapongeza mabadiliko??
Kulikoni kauli hizi za watafuta mabadiliko
Je tulitaka mabadiliko wakati hatujawa tayari kuyaishi mabadiliko? au mabadiliko yalikuwa ya kutafuta nafasi mpya za ulaji kupitia chama mbadala?
Ahsanteni na karibuni tuchangie bila mihemko