Tulitaka mabadiliko Mbona tunaogopa kubadilika?

Tulitaka mabadiliko Mbona tunaogopa kubadilika?

Asilimia kubwa ya mabadiliko yaliyofanywa na serikali ya Magufuli yamepokewa vizuri sana. Ni kwenye hili la bomoa bomoa tu limeleta kasoro. Hata hivyo wananchi hawajapinga bomoa bomoa ila wanataka lifanywe kwa busara zaidi bila kuleta maumivu makubwa kwao. Hivyo kwa ujumla wananchi wanafurahia mabadiliko yanayofanywa. Kuna wachache watakaopinga hilo lipo popote duniani katika utawala wa kidemokrasia
Well said mkuu 😀
 
Wadau JF,
Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha kuwa Hai na kuuona mwaka 2016. Pia Namshukuru kwa kuwaweka Hai wote mlio Hai kama mimi.

Naomba kuyatoa machache ninayoyaona kwa kiwango changu kama Changa moto kubwa iliyoko mbele yetu kama watanzania, bila kujali tofauti zetu za kielimu, kimapato,wala kisiasa.

Tanzania ya kabla ya Uchaguzi mkuu wa October mwaka 2015 na Tanzania baada ya October 2015 ni nchi ile ile lakini watu Hakika naona kama si walewale.
Nadiriki kusema haya kwa sababu, wakati kabla ya tar.25 ya mwezi October 2015, kila mtu aliimba mabadiliko na hii
iliongezeka hamasa zaidi pale kada na Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa alipojiengua toka CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chadema.

Kaulimbiu yake ikawa mabadiliko huku wapambe na wafuasi wake wakijibu mabadiliko Lowassa!

Wale waliojaribu kusema hata upande wa CCM una mabadiliko waliaminishwa kwamba ile ni system na haibadiliki na kama mtu angejikuta anapinga hayo mabadiliko ya Lowassa mbele ya wafuasi wake ilikuwa ni nadra kuachwa salama bila shambulio la aibu au hata mkongoto.

Yote haya yalikuwa yanaashiria kuwa watu nchini walikuwa wamechoshwa na hali halisi ya utawala wa awamu ya nne chini ya CCM. Na hawakuwa na Imani nayo Tena kuweza kuwapatia kiongozi mahili mwenye uzalendo na nchi yetu.

Lakini pia MUNGU ana maajabu yake kwani aliweza kuzuia mafuriko kwa mikono na hatimae mwisho wa yote watanzania walimchagua mgombea wa CCM mheshimiwa Dk John pombe magufuli kuwa Rais wao.
Ameingia madarakani na kuanza kazi Rasmi huku akitimiza alichoahidi wakati wa kampeni yake. Ya hapa ni kazi tu.
Ameanza kwa kusafisha uozo wa ufisadi katika sekta muhimu za mapato nchini kama Bandari, Tra, reli na bado vita ndio inaendelea tukiwa sasa sekta ya utumishi wa umma hasa ajira za raia wa kigeni na wahamiaji haramu sambamba na uboreshaji makazi hususan uhamishaji wa makazi hatarishi hasa mabondeni.
Nina Imani zoezi hili muhimu litafuata haki bila upendeleo na kuwachukulia hatua watumishi wa umma watakaobainika kukiuka maadili ya utumishi na kutoa vibali bandia vya ujenzi holela. Na ikibidi kutoa fidia kwa wahanga.

Baada ya hayo Nina hitimisha kwa swali muhimu.

Kama watanzania tulitaka mabadiliko kwa kuchoshwa na matendo ya serikali kufanya kazi kwa mazoea,
Kwa serikali kufumbia macho ufisadi na ubadhilifu wa Mali ya umma, kwa serikali kuwa ya uswahiba nk.
Kwa serikali kutokusanya kodi na hivyo kutoweza kukidhi huduma za muhimu kijamii kama elimu bure, uboreshaji wa ma hospitali yetu.
Sasa tingatinga la kweli linafanya kazi ya usafishaji wa yote haya Tena kwa kasi ya rapid, tumeanza kulalamika kulikoni???
Mbona sasa tunaanza kulalamika??
Mbona wale walio kuwa Mbele kutafuta mabadiliko sasa wamekuwa wa mwisho kuyapongeza mabadiliko??

Kulikoni kauli hizi za watafuta mabadiliko

Je tulitaka mabadiliko wakati hatujawa tayari kuyaishi mabadiliko? au mabadiliko yalikuwa ya kutafuta nafasi mpya za ulaji kupitia chama mbadala?
Ahsanteni na karibuni tuchangie bila mihemko
tulikuwa tunasema anatekeleza ilani ya ukawa mambo yamegeuka basi na sisi tumebadili mawazo. sasa hivi anatekeleza ilani ya ccm. hahahaha mabaya yote ya ccm na mazuri yote ya ukawa. hapa kazi tuu.! wananchi wajitahidi kuelewa haya ndio mabadiliko tuliyokuwa tukiyataka.ni lazima kuna wenzetu wataumia na wengine watafurahia. then mwisho wa siku tutakuwa katika mstari mmoja na tutaanza kufaidi keki ya taifa. vinginevyo kama tutaacha mafisadi wanaendelea kutafuna nchi hii hatutaweza ila keki hii vizazi na vizazi. wananchi msidanganywe na wanasiasa uchwala hawana jema lolote kwa mwananchi. kwa sasa tumuunge mkono Magufuli tuu
 
Swala la kukoa uhai wa watu siyo tuigemee serikali pekee bali ni jukumu la kila mmoja wetu hata wanasiasa wanapaswa kuwasaidia wananchi bila kujali itikadi zao za vyama, Dodoma watu kufa njaa ni swala la kila mmoja kuokoa maisha ya watu hawa, hili mkuu halina chama wala serikali kama una uwezo saidia kadri uwezavyo.
 
Wadau JF,
Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha kuwa Hai na kuuona mwaka 2016. Pia Namshukuru kwa kuwaweka Hai wote mlio Hai kama mimi.

Naomba kuyatoa machache ninayoyaona kwa kiwango changu kama Changa moto kubwa iliyoko mbele yetu kama watanzania, bila kujali tofauti zetu za kielimu, kimapato,wala kisiasa.

Tanzania ya kabla ya Uchaguzi mkuu wa October mwaka 2015 na Tanzania baada ya October 2015 ni nchi ile ile lakini watu Hakika naona kama si walewale.
Nadiriki kusema haya kwa sababu, wakati kabla ya tar.25 ya mwezi October 2015, kila mtu aliimba mabadiliko na hii
iliongezeka hamasa zaidi pale kada na Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa alipojiengua toka CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chadema.

Kaulimbiu yake ikawa mabadiliko huku wapambe na wafuasi wake wakijibu mabadiliko Lowassa!

Wale waliojaribu kusema hata upande wa CCM una mabadiliko waliaminishwa kwamba ile ni system na haibadiliki na kama mtu angejikuta anapinga hayo mabadiliko ya Lowassa mbele ya wafuasi wake ilikuwa ni nadra kuachwa salama bila shambulio la aibu au hata mkongoto.

Yote haya yalikuwa yanaashiria kuwa watu nchini walikuwa wamechoshwa na hali halisi ya utawala wa awamu ya nne chini ya CCM. Na hawakuwa na Imani nayo Tena kuweza kuwapatia kiongozi mahili mwenye uzalendo na nchi yetu.

Lakini pia MUNGU ana maajabu yake kwani aliweza kuzuia mafuriko kwa mikono na hatimae mwisho wa yote watanzania walimchagua mgombea wa CCM mheshimiwa Dk John pombe magufuli kuwa Rais wao.
Ameingia madarakani na kuanza kazi Rasmi huku akitimiza alichoahidi wakati wa kampeni yake. Ya hapa ni kazi tu.
Ameanza kwa kusafisha uozo wa ufisadi katika sekta muhimu za mapato nchini kama Bandari, Tra, reli na bado vita ndio inaendelea tukiwa sasa sekta ya utumishi wa umma hasa ajira za raia wa kigeni na wahamiaji haramu sambamba na uboreshaji makazi hususan uhamishaji wa makazi hatarishi hasa mabondeni.
Nina Imani zoezi hili muhimu litafuata haki bila upendeleo na kuwachukulia hatua watumishi wa umma watakaobainika kukiuka maadili ya utumishi na kutoa vibali bandia vya ujenzi holela. Na ikibidi kutoa fidia kwa wahanga.

Baada ya hayo Nina hitimisha kwa swali muhimu.

Kama watanzania tulitaka mabadiliko kwa kuchoshwa na matendo ya serikali kufanya kazi kwa mazoea,
Kwa serikali kufumbia macho ufisadi na ubadhilifu wa Mali ya umma, kwa serikali kuwa ya uswahiba nk.
Kwa serikali kutokusanya kodi na hivyo kutoweza kukidhi huduma za muhimu kijamii kama elimu bure, uboreshaji wa ma hospitali yetu.
Sasa tingatinga la kweli linafanya kazi ya usafishaji wa yote haya Tena kwa kasi ya rapid, tumeanza kulalamika kulikoni???
Mbona sasa tunaanza kulalamika??
Mbona wale walio kuwa Mbele kutafuta mabadiliko sasa wamekuwa wa mwisho kuyapongeza mabadiliko??

Kulikoni kauli hizi za watafuta mabadiliko

Je tulitaka mabadiliko wakati hatujawa tayari kuyaishi mabadiliko? au mabadiliko yalikuwa ya kutafuta nafasi mpya za ulaji kupitia chama mbadala?
Ahsanteni na karibuni tuchangie bila mihemko
Rubbish
 
Naona umefarijika kuniqoute kisa tumetofautiana mtazamo we unajiona una elimu sana na akili nyingi, hongera yako mama
Wapi WAHEED watu tungekuwa tunasajiliwa JF kwa elimu hata huyo unayemwambia anaona ana elimu kubwa kuliko wewe asingepata nafasi JF watu wanajidai wanajua na ukishaona umetofautina na mtu akaanza personal attacks jua huyo ni kanjanja.Wala asikupe shida mkuu
 
Hata Mimi najaribu kuwaelewa baadhi ya watu lakini nashindwa.

Wale wale waliokuwa wanaimba wanataka mabadiliko sasa WANAYAPINGA???

Magufuli alipoanza kazi walisema anatekeleza ilani ya UKAWA kwani CCM haiwezi leta mabadiliko, Leo wamegeuka!!!

Tanzania tuna safari ndefu. Mungu atusaidie.

Queen Esther
Tatizo hujui tafsiri ya neno MABADILIKO, so hata unachoongea huwezi kukitetea kwa sababu neno lililobeba mada limekuwa msamiati kwako.Unafikiri mabadiliko ni kubomoa nyumba?ni kuzuia safari za nje?Ni kufukuza na kusimamisha watu kazi?au kutisha? Google maana ya neno madadiliko linapotumiwa na wanasiasa linamanisha nini halafu rudi kuja kuchangia.
 
Ndugu yangu, safari ya mabadiliko si safari ya mwezi mmoja tu, Bali ni suala la muda na gharama kubwa sana za kifedha, Mali kama majumba (yanayovunjwa sasa) na pia hata saa nyingine uhai pia.

Sio suala la kufumba na kufumbua kwa hiyo list yako yote ni miongoni mwa mikakati mahsusi ya serikali ya JPM, chini ya CCM.

Kwa Hali halisi ni lazima kuwe na mpangilio wa utendaji. Ukihusisha bunge, mahakama, na serikali yenyewe na pia wadau mbali mbali wapenda mabadiliko ya kweli, tukiwemo pia sisi wananchi wenyewe kuwa wazalendo na kutimiza wajibu wetu kama itupasavyo.
Na tujitume pale tunapopata nafasi ya kuitumikia Taifa katika nafasi yoyote inayopatikana bila wizi.. Nina Imani kila mtu akitimiza wajibu wake tutakuwa nchi ya mfano ifikapo 2020.
Nakubaliana na wewe, Ndio maana nimesema nawashangaa watu wanaompongeza jpm ndani wa mwezi mmoja wakati hakuna positive effects yoyote iliyoonekana mitaan.
 
Nakubaliana na wewe, Ndio maana nimesema nawashangaa watu wanaompongeza jpm ndani wa mwezi mmoja wakati hakuna positive effects yoyote iliyoonekana mitaan.
Nimekuelewa vizuri ahsante
 
Huwezi kutumbua hayo ya kihistoria na bila kuzuia na kuyatumbua yaliyopo live, wakati ndio yanayoumiza kwa sasa.
Hii Richmond, escrow iptl na mengine yanafuatia kwani hayo yako kwenye mhimili mwingine kw:🙂a sasa nao ni bungeni. Ni suala la muda tu,
Pia mjiandae kisaikolojia kwani mengine yakitumbuliwa misiba inaweza kuwa mingi kuliko ya bomoa bomoa.
Tulimuona Rished Bade akiwa team Lowassa.
Tuna taarifa na uhamisho wa bilioni Tatu takriban uliofanywa kinyemela na Mbowe na kutaarifiwa na media kadhaa nchini na mhusika kukaa kimya bila kutoa ufafanuzi, wakati akituaminisha ni kamanda Safi wa angani. Nk.... Nk..... Just time will tell
....na kwa kuongezea tu, kuwashughulikia wahusika wa ufisadi huo ulioorodheshwa ktk mfumo wa sasa wanaweza still kupuruchuka.....tumeshuhudia kesi za meli ya samaki ya wachina, na pia ufisadi ktk manunuzi ya jengo la ubalozi wetu italia, pia zugazuga kwenye kesi ya ufisadi wa UDA...hapa itangulie marekebisho yakisheria yatakayoleta mahakama maalum kushughulikia kesi za ufisadi,huku takukuru ikizisimamia mashtaka ktk mahakama hizo...
 
Well said mkuu, tuko pamoja
 
Mabadiliko waliyoyasema wagombea na wanaoyaamini ni tofauti kabisa na mabadiliko wananchi engi wanayoyataka. Mfano, Wananchi walio wengi wanataka kuona bei ya sukari na vyakula inashuka, au inakua affordable, wanataka kuona huduma za afya zinapatikana kirahisi, na sio dar tu kila kona ya nchi hii, kodi inapungua, elimu inayoeleweka na iliyoborra inapatikana n.k ndio maana siwaelewi watu wanaompongeza raisi kwa muda huu mchache wakati effect mitaan haijaonekana. Waliposema kuhusu mahakama ya mafisadi kumbuka wanaichi wanalist yao, ila utashangaa watakaohukumuwa kwenye hizo mahakama, watakuwa walimu wakuu, wakurugenzi, polisi, n.k hakutakuwa na waziri hata mmoja, au wale wananchi waliowatarajia. Na hivyo ndivyo tunavyopishana kuhusu mabadiliko
waswahili tuna msemo wetu unasema Nyota njema huonekana asubuhi,kwahiyo waache watu wampongeze Raisi kwasababu asubuhi ya Tanzania imeanza kukaribia maana kinachotia moyo ni nia inayoonekana kwa Raisi,mwanzo tuliaminishwa hawezi kuleta jipya kwasababu tatizo ni mfumo lakini tunaona kumbe inawezekana kinachotakiwa tuwe na imani,uvumilivu na tumsaidie kwasababu hivyo vitu wanavyovitaka wananchi haviwezi kutokea kufumba na kufumbua lazima misingi iwekwe na turudi kwenye sheria kwamba kila mtu kwa nafasi aliyonayo afate sheria,kuwa na listi na hukumu ni vitu viwili tofauti maana sheria inasema not guilt until proven,na hawa walio juu walizijua njia za kufanya madudu huku wakijua sheria watacheza nayo vipi kuliko wenzangu namimi hii haihitaji kwenda shule kujua.
 
....na kwa kuongezea tu, kuwashughulikia wahusika wa ufisadi huo ulioorodheshwa ktk mfumo wa sasa wanaweza still kupuruchuka.....tumeshuhudia kesi za meli ya samaki ya wachina, na pia ufisadi ktk manunuzi ya jengo la ubalozi wetu italia, pia zugazuga kwenye kesi ya ufisadi wa UDA...hapa itangulie marekebisho yakisheria yatakayoleta mahakama maalum kushughulikia kesi za ufisadi,huku takukuru ikizisimamia mashtaka ktk mahakama hizo...
uko sawa kabisa
 
E

Huu upuuzi haukubaliki kwa hiyo serikali ijitoe kwenye lawama ya wananchi kushinda njaa eti kwa sababu yenyewe hausababishi mvua basi ingekuwa ivi nchi ya jangwani Kama Israel au Libya; misri ingekuwa balsa basi.
Kwanza kusema eti janga la njaa ni suala la asili huu nao ni ujuha wa aina yake,sasa inakuaje kyela dar watu wawe na chakula alafu Dodoma kuwe na njaa,serikali imeshindwa vipi kununua chakula kuwapelekea
 
Hayo yanayofanyika ni ghilba zinazotokana na utekaji wa agenda wa ccm bila kumaanisha, bila kuwa na nia wala mkakati wowote. Matokeo yake wanaishia kupapasa papasa ili kuwaonyesha watu kuna mabadiliko.

Sis hatukutaka mabadiliko njiti, mabadiliko ndebila au mabadiliko songi!!!!!!!!!!!!, ndiyo sababu tunashangazwa na sarakasi za sanaa za ccm zisizokuwa na mizizi wala uwezekano wa mwendelezo.

Tulimaanisha overhauling. Siyo hii rambaramba, na pakarangi kwenye nyufa inayofanyika. Huku wakilazimisha media ziwatangaze wao na kuzuia mikutano ya wanamabadiliko halisi wasije kuwafungua watu macho. Manipulative, superficial and malicious approaches never shall bring sustainable changes!. Changes that we desired.

Tunacho kihitaji siyo mnachojaribu kubumbabumba huku mkikimbilia media, na kutaka kujua, tunasemaje.

CCM ILIYOUA NCHI, HAIWEZI KULETA MABADILIKO SAHIHI KWA SABABU MABADILIKO HALISI NI MAUTI KWA CCM. Who wants to die?

Tafadhali sana, jitambueni.
 
Kwa kweli na mie nimeanza kuingiwa na mashaka na baadhi ya kauli,za wakati wa kampeni na ambavyo tuliaminishwa,kwamba mabadiliko yataletwa na UKAWA lakini Mungu si athumani mambo hayakuwa hivyo,ikaanza minong'ono,mara oooh anatekeleza sera,za ukawa,moyoni nikafarijika kuwa ataanza kuungwa mkono si wamedai,anatekeleza focus yao,lakini mara ooh mbona hiki na kile.Sheria ambayo ni msumeno ilipoanza,si unajua unakata kuwili,wanaanza kudai siyo mabadiliko,waswahili walisema daima,mti wenye matunda ndo hupigwa mawe.nahisi wengine waliimba tu wimbo mabadiliko lakini,hawajawahi usikia,sasa kwa taarifa yenu ndo huu,chezen,mabadiliko huwa ni gharama mfano waliojenga njiani kama hupo serious utaishia majadiliano nao badala ya kubomoa,watanzania kwa sasa ni kujua kwamba hapa kazi tu,basi.
 
Kwanza kusema eti janga la njaa ni suala la asili huu nao ni ujuha wa aina yake,sasa inakuaje kyela dar watu wawe na chakula alafu Dodoma kuwe na njaa,serikali imeshindwa vipi kununua chakula kuwapelekea
Ukishataka serikali iwanunulie wanachi chakula na iwapelekee wakati sio kazi ya selikali kulisha wananchi ujue tayari kuna tatizo ambalo sio la kawaida ambalo ndio tunaweza kuliita janga,aihitaji digrii kujua hili.
 
Back
Top Bottom