Tulitaka mabadiliko Mbona tunaogopa kubadilika?

Mkuu, mabadiliko tuliyokuwa tunayataka siyo haya mabadiliko yetu ni yale ya kuzungusha mikono.
 
E

Huu upuuzi haukubaliki kwa hiyo serikali ijitoe kwenye lawama ya wananchi kushinda njaa eti kwa sababu yenyewe hausababishi mvua basi ingekuwa ivi nchi ya jangwani Kama Israel au Libya; misri ingekuwa balsa basi.
endelea kuzungusha mikono eheeeeeeee
 
Hi

Suala hapa si ujinga, kama ni janga la njaa serikali ingelaumiwa kama imepata taarifa halafu ikakaa kimya, lakini sivyo Na hata wewe taarifa ndio zimetolewa Jana halafu Leo uko mtandaoni kutukana watu kwamba ujinga.
Nani mjinga hapa, wewe unaeilaumu serikali ya CCM chini ya JPM na kuisifia Israel, wakati hujui kwamba watu kama wewe kule Israel kuishi tu siku moja ni bahati
Je wewe ulitaka JPM awe Malaika na kuota ndoto kabla ya janga husika au?
Je baada ya taarifa hiyo kuripotiwa umesikia ikirudiwa kwamba bado serikali haijawafikia au?

Umaskini upo hadi USA kule pia wana Masikini ombaomba kama unabisha jaribu tu ku Google homeless in America na utajua namaanisha nini... Tuendelee
 
Last edited:
endelea kuzungusha mikono eheeeeeeee
Hata sijui ulichoandika unamaanisha nini mm sikubaliani na jamaa alivyoadai kwamba serikali isipewe lawama kwa sababu yenyewe haisababishi mvua kunyesha au isinyeshe. Haya ni mawazo ya kipuuzi serikali lazima itafute solutions juu ya matatizo yote yanayowakumba wananchi na sikukimbilia kudai wao co mungu kwa mujibu wa mtoa mada alivyodai.
 
Suala sio hapo kwenye janga suala liko kwenye hoja yangu inasema

*tulitaka mabadiliko Mbona tunaogopa kubadilika *

Sasa wachangiaji wengine hamtaki kusoma na kujibu thread kulingana na maudhui yake na badala yake mtu analeta jibu la mkato kwamba ma CCM waache usanii Bali wakawalishe watu wanaokufa na njaa, wakati akijua ndio kwanza taarifa zimetolewa Jana na pia hakuna mtu kafa kule Bali wana mahitaji ya dharula sasa hii inaendana vipi na hoja yangu ya msingi?

Ni bora mtu kama hujaelewa ukasoma na kupita bila matusi na ukawaachia wachangiaji serious waendelee au sio?
 
Suala hapa si ujinga, kama ni janga la njaa serikali ingelaumiwa kama imepata taarifa halafu ikakaa kimya, lakini sivyo Na hata wewe taarifa ndio zimetolewa Jana halafu Leo uko mtandaoni kutukana watu kwamba ujinga.
Nani mjinga hapa, wewe unaeilaumu serikali ya CCM chini ya JPM na kuisifia Israel, wakati hujui kwamba watu kama wewe kule Israel kuishi tu siku moja ni bahati
Je wewe ulitaka JPM awe Malaika na kuota ndoto kabla ya janga husika au?
Je baada ya taarifa hiyo kuripotiwa umesikia ikirudiwa kwamba bado serikali haijawafikia au?

Umaskini upo hadi USA kule pia wana Masikini ombaomba kama unabisha jaribu tu ku Google homeless in America and na utajua namaanisha nini... Tuendelee

Sijui Kama nimeilaumu serikali ya ccm mi nipo kinyume na hoja yako uliyotoa kwamba serikali sio mungu hivyo haisababishi mvua haya ni mawazo ya kipuuzi umepewa ubongo wa nini sasa. Serikali inawajibu kutafuta solutions ya matatizo yanayowakumba wananchi.matatizo ya njaa si ya Jana wala leo.
 
Suala sio hapo kwenye janga suala liko kwenye hoja yangu inasema

*tulitaka mabadiliko Mbona tunaogopa kubadilika *

Sasa wachangiaji wengine hamtaki kusoma na kujibu thread kulingana na maudhui yake na badala yake mtu analeta jibu la mkato kwamba ma CCM waache usanii Bali wakawalishe watu wanaokufa na njaa, wakati akijua ndio kwanza taarifa zimetolewa Jana na pia hakuna mtu kafa kule Bali wana mahitaji ya dharula sasa hii inaendana vipi na hoja yangu ya msingi?

Ni bora mtu kama hujaelewa ukasoma na kupita bila matusi na ukawaachia wachangiaji serious waendelee au sio?

Kwani mabadiliko yanapatikana kwa mieZi miwili?
 
Sijui Kama nimeilaumu serikali ya ccm mi nipo kinyume na hoja yako uliyotoa kwamba serikali sio mungu hivyo haisababishi mvua haya ni mawazo ya kipuuzi umepewa ubongo wa nini sasa. Serikali inawajibu kutafuta solutions ya matatizo yanayowakumba wananchi.matatizo ya njaa si ya Jana wala leo.
kabla ya serikali,mtu binafsi unawajibu wa kutafuta solution ya matatizo yanayokukumba.
 
Sijui Kama nimeilaumu serikali ya ccm mi nipo kinyume na hoja yako uliyotoa kwamba serikali sio mungu hivyo haisababishi mvua haya ni mawazo ya kipuuzi umepewa ubongo wa nini sasa. Serikali inawajibu kutafuta solutions ya matatizo yanayowakumba wananchi.matatizo ya njaa si ya Jana wala leo.
Usinitowe kwenye Mada yangu tafadhali kuna thread humu kuhusu wala viwavi wa dodoma, Unaweza kuingia huko ukachangia unavyoona wewe ni sahihi na hata mimi nikitaka nitaenda huko lakini hapa ni hii hapa heading yangu

*tulitaka mabadiliko Mbona tunaogopa kubadilika? *

Ukipenda isome vizuri na u comment kwa niliyoyasema na hili la majanga si hoja yangu kwa thread yangu karibu Tuendelee ukishaisoma thread.... Sio namba.
 
Kwa ujumla inabidi watanzania tujitambuwe,
Tuliposema mabadiliko tulimaanisha tuache ubadhirifu, tuache mazoea na tufuate sharia, pia tuisaidie serikali kubadilika. (endapo Nia ya mabadiliko ni thabiti).

Sasa tukiongelea kuishi kwa kufuata sheria ndio mfano mmoja huu wa bomoa bomoa inavyowashinda hata wale waliotuaminisha kama wapenda mageuzi na mabadiliko, lakini sasa wako busy kuhamisha hela kupeleka nje huku wakisema CCM inafuata sera zao.
Je huu si unafiki wa kisiasa
 
Usinitowe kwenye Mada yangu tafadhali kuna thread humu kuhusu wala viwavi wa dodoma, Unaweza kuingia huko ukachangia unavyoona wewe ni sahihi na hata mimi nikitaka nitaenda huko lakini hapa ni hii hapa heading yangu

*tulitaka mabadiliko Mbona tunaogopa kubadilika? *

Ukipenda isome vizuri na u comment kwa niliyoyasema na hili la majanga si hoja yangu kwa thread yangu karibu Tuendelee ukishaisoma thread.... Sio namba.
Asilimia kubwa ya mabadiliko yaliyofanywa na serikali ya Magufuli yamepokewa vizuri sana. Ni kwenye hili la bomoa bomoa tu limeleta kasoro. Hata hivyo wananchi hawajapinga bomoa bomoa ila wanataka lifanywe kwa busara zaidi bila kuleta maumivu makubwa kwao. Hivyo kwa ujumla wananchi wanafurahia mabadiliko yanayofanywa. Kuna wachache watakaopinga hilo lipo popote duniani katika utawala wa kidemokrasia
 
Mabadiliko waliyoyasema wagombea na wanaoyaamini ni tofauti kabisa na mabadiliko wananchi engi wanayoyataka. Mfano, Wananchi walio wengi wanataka kuona bei ya sukari na vyakula inashuka, au inakua affordable, wanataka kuona huduma za afya zinapatikana kirahisi, na sio dar tu kila kona ya nchi hii, kodi inapungua, elimu inayoeleweka na iliyoborra inapatikana n.k ndio maana siwaelewi watu wanaompongeza raisi kwa muda huu mchache wakati effect mitaan haijaonekana. Waliposema kuhusu mahakama ya mafisadi kumbuka wanaichi wanalist yao, ila utashangaa watakaohukumuwa kwenye hizo mahakama, watakuwa walimu wakuu, wakurugenzi, polisi, n.k hakutakuwa na waziri hata mmoja, au wale wananchi waliowatarajia. Na hivyo ndivyo tunavyopishana kuhusu mabadiliko
 
Sukari itashukaje WAKATI kuna wahujumu uchumi ,hudama za afya zitaborekaje wakati wakuwepaji kodi ni wengi ,ndo kuanza tunaanza kazi huduma ishuke kwa wananchi
 
Haya ni mabadiliko au maigizo!? Huko Dodoma wananchi wanakufa kwa njaa iambie serikali yako ikafanye mabadiliko ili wananchi wasife njaa
Pole sana! wewe utakuwa ni moja wa wale walioamini mabadililko ya kuzungusha mikono... mkiimaanisha kuzidisha ufisadi... namba utaisoma sana tena kwa kirumi!
 
Sawa mkuu, wanaoisoma namba tushaanza kuwaona huenda na mimi nimo, kwa mjibu wa akili yako
 
Safari za nje zisizo na tija kwa taifa zimefutwa, sherehe ambazo watu wanapiga hela na zenyewe zinatazamwa kikamilifu, mirija yote ya ulaji fedha inakatwa. Hakuna tena michakato uundaji wa tume. Hakuna tena urasimu katika ufanyaji kazi wa serikali. Hayo yote ni mabadiliko ambayo huambatana na maisha magumu kwa wale waliozoea kula bila ya kutoka jasho. Mabadiliko duniani huwa hayatokei bila sura za watu kununa, ukiona mabadiliko yanatokea halafu bado watu wanatabasamu kama kawaida, basi hayo ni kitu kingine wala sio mabadiliko.
 
Huo ndio UKWELI bwana bukililo mimi nilitoka kidogo na sasa nimerudi na nitamjibu kila mmoja wetu humu kadri ya mchango wake na ninaomba tuendekee, ahsante
 
Mabadiliko waliyoyasema wagombea na wanaoyaamini ni tofauti kabisa na mabadiliko wananchi engi wanayoyataka. Mfano, Wananchi walio wengi wanataka kuona bei ya sukari na vyakula inashuka, au inakua affordable, wanataka kuona huduma za afya zinapatikana kirahisi, na sio dar tu kila kona ya nchi hii, kodi inapungua, elimu inayoeleweka na iliyoborra inapatikana n.k ndio maana siwaelewi watu wanaompongeza raisi kwa muda huu mchache wakati effect mitaan haijaonekana. Waliposema kuhusu mahakama ya mafisadi kumbuka wanaichi wanalist yao, ila utashangaa watakaohukumuwa kwenye hizo mahakama, watakuwa walimu wakuu, wakurugenzi, polisi, n.k hakutakuwa na waziri hata mmoja, au wale wananchi waliowatarajia. Na hivyo ndivyo tunavyopishana kuhusu mabadiliko
Ndugu yangu, safari ya mabadiliko si safari ya mwezi mmoja tu, Bali ni suala la muda na gharama kubwa sana za kifedha, Mali kama majumba (yanayovunjwa sasa) na pia hata saa nyingine uhai pia.

Sio suala la kufumba na kufumbua kwa hiyo list yako yote ni miongoni mwa mikakati mahsusi ya serikali ya JPM, chini ya CCM.

Kwa Hali halisi ni lazima kuwe na mpangilio wa utendaji. Ukihusisha bunge, mahakama, na serikali yenyewe na pia wadau mbali mbali wapenda mabadiliko ya kweli, tukiwemo pia sisi wananchi wenyewe kuwa wazalendo na kutimiza wajibu wetu kama itupasavyo.
Na tujitume pale tunapopata nafasi ya kuitumikia Taifa katika nafasi yoyote inayopatikana bila wizi.. Nina Imani kila mtu akitimiza wajibu wake tutakuwa nchi ya mfano ifikapo 2020.
 
Back
Top Bottom