Tulipotezana miaka tisa, tumeonana anataka kunioa

Tulipotezana miaka tisa, tumeonana anataka kunioa

safaributi

New Member
Joined
Feb 8, 2015
Posts
1
Reaction score
0
Wanajamii wenzangu kuna huyu jamaa ananitatiza nisaidieni please.Huyu mwanaume tulipendana kama miaka tisa ya nyuma tukapotezana kwa muda tulopokutana akasema anahitaji kunioa.

Mimi kwakuwa nilikuwa nampenda nikamwambia anipe muda niweze kusitisha mahusiano niliyonayo na jamaa anayenisumbuasana.

Maajabu yakaanza mara aniambie kaoa anioneshe na picha, kesho aseme hajaoa huu ukawa kama mchezo nimejaribu kupeleleza sipati jibu. Jamaa anajua kutunga uongo sana anaweza kusema hata alikufa lakini anaishi.

Sasa nipo njia panda msaada .
:shocked::shocked:
 
Hilo nalo ni suala la kuomba watu ushauri? Huna akili zako mwenyewe za kuweza kupembua pumba na mchele?

Wa wapi wewe.?
 
Hivi wew ni safaributi au buti la safari hebu tuanzie hapo kwanza na jina lako, au wewe ni buti lile la Timberland unga wa mbao
 
Ukiona hivyo ujue hakuna ndoa hapo frankly speaking! Alafu ilikuwaje mtu mmeachana mda then mnakutana tena anadai kutaka kukuoa nawe unakubali haraka na unastisha hadi mahusiano yako kwa ajili ya mtu ambae hujawa nae kwa miaka sasa na hujui mienendo yake? Ungemchunguza kwanza
 
Una miaka ngap wew mana kam ungekuwa above 18.

Ungejiongeza kidogo ungepata jibu.Anyway neno moja tu,mapenzi yasikupelekeshe kama umekatwa kichwa kuna msemo unasema undaa undaaa as wew akikupiga sound piga fix usikubali kupelekwa pelekwa ovyo
 
Hyo Gia 2.Mpanulie Ili Asaini.Halaf Ndo Utapat Jb
 
Khaa!! Ajabu sana. Labda kama ulikutana naye ukiwa 2yrs old na sasa una 11yrs hapo nitakushauri umuonjeshe kidogo kisha msikilizie
 
Achana nae, anataka kukuharibia tu,mambo mengine wala hayahitaji kuuliza JF
 
[QUOTE anaweza kusema hata alikufa lakini anaishi .:shocked::shocked:[/QUOTE]

Aisee huyo ni first class liar.
 
Mbona Binti unapenda mtu akuone upeo wako wa kufikiri ni mdogo? jibu uko nalo na still unauliza jibu?
Au unataka uwambiwe mpe mda atabadilika? au hujui nini unataka? unata yote eeh vya bara na vya pwani?
 
Hatimaye sasa Bwana ametenda, njoo kwangu ninyi nyote msumbukao na mapenzi kama wewe, kuna pumziko pale Edenpark luguruni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom