Hii obsession yako na Mwalimu imekuwekea wingu zito usoni mpaka unashindwa kabisa kuona mambo mengi tu kwa usahihi wake kamili. Hebu jaribu kutoa timeline kwa haya mambo unayoyadai ili tuweze kupima kama yalisababishwa na mapungufu ndani au nje ya Azimio. AD ilitangazwa mwaka 1967, je ilichukua muda gani kwa matatizo hayo unayoyadai kutokea na yalisababishwa na nini.
Duniani kote watu wote hawawezi kukubaliana kwa kila jambo hata likiwa zuri namna gani na hasa linapokinzana na maslahi ya kundi fulani. Hivi sasa tunashuhudia Marekani ilivyogawanyika katika swala la afya kwa wote na kuna wanaoapa kabisa eti lisifanikiwe - naam, ndivyo watu walivyo. Ni hapo mafanikio yatakapoonekana ndiyo hao wenye roho ngumu watakapoweza kusalimu amri japo shingo upande.
Lakini hali hii ipo tofauti kidogo kwa nchi masikini na changa kama yetu. Shuhudia inavyokuwa vigumu kuwashughulikia hata mafisadi - watu ambao dhahiri tungeweza kuwaita wahujumu uchumi. Ni rahisi kwa watu wenye uwezo wa kifedha kuwarubuni wananchi ambao wengi wao ni masikini wa kutupwa kuwaunga mkono. Ndio maana demokrasia kwenye nchi kama zetu siku zote hazifanikiwi au hubaki zikisuasua.
Viwanda vingi baada tu ya kutaifishwa, pamoja na kukosa wataalamu waliobobea, vilifanya kazi vizuri tu na na kwa faida kubbwa tu. Kama kuna wakati tuliweza kufanya biashara kama kuuza nje bidhaa za viwango zilizotengenezwa Tanzania ni wakati huo. Lakini kuna walioapa toka mwanzoni kuhakikisha kuwa Azimio halifanikiwi kabisa. Hebu fikiria
the Patels, the Somaiyas and the Rostamus wa wakati huo.
Uwezo wa kuvihujumu walikuwa nao na viwanda viliweza kuhujumiwa, period. Hata hivyo tuliweza kustahimili na kupambana na hizi hujuma za ndani mpaka pale matatizo yalipojitokeza nje ya uwezo wetu kama kupanda kwa bei ya mafuta duniani na vita vya Kagera. Of course kuna Watanzania ambao wanaona hivi vita havikuwa lazima na kuna wanaoenda mbali zaidi na kudai tulimwonea Idi Amin lakini kama alivyosema Mwalimu - sabau, nia na uwezo vyote tulikuwa navyo.
Je, kabla ya vita kama hali ingekuwa mbaya unavyotaka kutuaminisha, huo uwezo tungeupata wapi kwani ni kweli tulimpiga yeye, Walibya na Wapalestina waliokuja kumsaidia. Tulikuwa na uwezo wa kumtoa mvamizi wa ardhi yetu lakini leo hii hatuna hata uwezo wa kuwatoa mafisadi wanaotafuna rasilimali za taifa kama mchwa. Hivi sasa hatuna hata cha kujivunia halafu wanatokea watu kama wewe - unakuwa na jeuri ya kumkashifu Mwalimu,
shame on you.
Jemadari Mkuu akiwatembelea vijana wake wakati wanatembeza kipigo kumtoa nyoka pangoni.