Tulipokwama kama Taifa; tutajinasua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulipokwama kama Taifa; tutajinasua?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jmushi1, Mar 26, 2010.

 1. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Waungwana wa JF mabibi na mabwana nawasalimu na kutumaini mko fine.

  Wakati tukielekea kwenye uchaguzi mkuu ambao binafsi naamini ni wa muhimu pengine kuliko chaguzi zote zilizopita,ni budi tukatafakari kwa umakini wa hali ya juu....Certainly sisi wenye opportunity ya kukutana hapa na kubadilishana mawazo,ni wakati wa kuwa chachu ya ukombozi wa Taifa letu.

  Ndugu wana JF;

  Nimeshtushwa na mambo kadhaa ambayo yametokea miaka na hata siku za hivi karibuni,ni mshtuko mbaya ambao kamakweli unajali hauwezi kupata usingizi vyema.

  Kwanza kabla ya kwenda mbele,kuna jambo jingine ambalo nalo pia limenishangaza na kuanza kujiuliza maswali mengi sana kama vile;are we making any progress? ama bado tu tuna mawazo ya kwamba hapa ni kijiweni pa kupiga soga basi?

  Mh mbunge Dr Slaa ambaye pia ni member mwenzetu hapa JF amesema kwamba katika uchunguzi wao kuhusiana na mawazo ya wananchi ya kuwa ni kwa vipi wanaichukulia rushwa,na wananchi hao kudai kuwa viongozi wanawapa rushwa kwasababu wanawapenda ni jambo la kushangaza,certainly mojawapo ya sababu za kukwama kwetu kama Taifa!Nionavyo mimi,tumekwama kwenye uongozi,na pia kijamii!

  Tumekwama kwenye uongozi:

  Ndugu wana JF,nirudi basi kwenye hoja ya msingi kuhusiana na yale yaliyotokea chini ya utawala wa awamu hii ya kwanza ya Mh JK inayoelekea ukingoni. Nazungumzia awamu hii kwasababu ni mwendelezo tu wa yale ya awamu zilizopita na ndio maana wanasemea kuwa "acha apumzike" nk....Na wengine kama Mh Mwinyi kuanza kujichanganya kwa kusema eti hakuliua AD,mwenzake anayetakiwa "apumzike" na huyu wa sasa,alishawahi kudai kuwa "Eti mbona sijazomewa?" Ni vituko tu....!Sina haja ya kuwa kama kasuku na kurudia kashfa zote kuanzia Buzwagi,EPA hadi RICHMOND na DOWANS,na pia siku za hivi karibuni kusaini sheria kwa mbwembwe nyingi wakati hakuna umakini,ni utendaji wa wengi wa viongozi wetu wakuu kuanzia tupate uhuru,sina haja ya kuorodhesha tena,hata hivyo ni ukweli kwamba wananchi wamepata nafasi ya kujua mengi yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo ni kinyume kabisa na maslahi ya Taifa na yale wanayotakiwa kuyafanya wao kama viongozi kwa niaba yetu na vizazi vijavyo!

  Sasa hapo kwasababu thread hii ni kwaajili ya kuangalia ni wapi tulipokwama na pia solutions za how to move on if possible,then nirudi na kugusia kijamii...

  Tumekwama kijamii;

  Ndg wana JF: Awali ya yote,tujiulize swali moja kwanza; kama ni kweli kuwa wananchi wanaamini kuwa wanapopewa rushwa basi wanapendwa na hivyo wanawachagua viongozi hao wanaotoa rushwa,je mafisadi watashindwa vipi uchaguzi kwa mentality kama hiyo kutoka kwa wapiga kura?

  Ni wazi kuwa si wananchi wote wenye kufikiri hivyo,hata hivyo asilimia ya wanaofikiri hivyo ni kubwa maana asilimia ya viongozi mafisadi ni kubwa,hilo pia linapelekea asilimia kubwa ya maamuzi ya kifisadi,maslahi ya Taifa kuwekwa nyuma,na maendeleo ya nchi kudorora huku umasikini wa kupindukia miongoni mwa wananchi walio wengi vikiwa ni viashiria ama hali halisi ya kwamba tumukwama kwenye dimbwi zito.

  Mimi nimezaliwa kwenye familia ya Kikiristo,lakini nimesoma na pia kuwa na marafiki wa dini nyingine kuanzia waislam,Hindu nk,nimesoma boarding school na kuishi na watu wa makabila mengi na ya tofauti,lakini katika pita pita yangu huwa najiuliza kama mwalimu alifanikiwa "Kiukweli" kutuunganisha kama tunavyoamini.Ni kweli tunaimba tu kila siku kwamba tuna umoja,lakini hatujajiuliza umoja huo ni upi na malengo yake ni yapi?Tuliona faiulure ya AD,kwamba ilikuwepo lakini haikutekelezwa ipasavyo na mabadilko yapasayo hayakufanywa,tulikuwa tukiimba kuwa tuko strong!Lakini matokeo yake si kweli! Ni wazi kwamba hatuna umoja kwasababu watu wenye umoja wana malengo sawa,sisi na viongozi wetu ni wazi kuwa hatuna malengo sawa na hivyo ni wazi hatuna umoja wa "Kweli" pengine wengi wetu tunajua kabisa,lakini kama binadamu,tuna tabia ya kutaka kuamini hata uongo,kila mtu ana situation ambayo unajua kabisa something ni uongo,lakini huwezi kuuzuia uongo huo kuingia akilini mwako,kwa mfano kama uongo huo ni jambo la kufurahisha,basi ubongo wako utakuwa ukiufikiria uongo huo mara kwa mara kwasababu ya stimulation ama euphoria inayopelekewa na uongo huo,na ndio maana ahadi kama maisha bora kwa kila mtanzania zililkuwa za uongo na hata matokeo yake yako wazi,lakini bado watu wanataka kuamini uongo tu,na hapo kudanganyika kunatokea na wengine j
  kudai ni taifa la "Wadanganyika" ....cha muhimu ni usije kujikuta unauamini uongo huo kwasababu uongo ukirudiwa mara nyingi huwa "Justified" kuwa ukweli,sisi kama wanadamu kufanya maamuzi mengi ya muhimu ni lazima tuende beyond our normal way of thinking and doing things! Wamarekani wasingefika mwezini kama wangekuwa wanataka tu mambo normal na marahisi marahisi,ama wanasayansi na viongozi wenye kuchukua maamuzi magumu,na wananchi wenye kudare to change.

  Umoja tulio nao tujiulize kwanza ni wa aina gani ?kwani jamii yetu haina maendeleo,ufisadi umeshamiri na umasikini umekithiri!

  Je tuna uwezo wa kumchagua kiongozi bila kujali tofauti zetu tulizo nazo?Je tofauti zetu za kijamii ndizo zinapelekea tofauti zetu za kisiasa?Je si wakati wa kurudi kwenye basics ili tupate viongozi wa kweli?

  Sasa hivi as a grown up,binafsi, naamini Mungu yupo,ila simchagulii mtu kuamini kama yupo ama hayupo,ama kuamini Jesus Christ,Muhamad ama mtume yeyote!

  Wakati nikijiuliza maswali ya wapi tumekwama,hili huwa likinijia kichwani kwasababu wananchi wanafanya maamuzi mengi kwenye maisha yao depending na imani yao,certainly maamuzi hayo yalipokuwa yakiingia kwenye siasa,tunaweza kuona mwalimu alijaribu na kuwekeza nguvu nyingi sana ili udini usienee. Na hapo pia ndipo tunaweza kuona jitihada hizo haswa pale alipoweka wazi kuwa serikali haina dini

  Hata hivyo wananchi wana dini,na wengine hawana dini kabisa...However wote hao wanaunganishwa na maslahi ya Taifa huru la Tanzania,kinyume cha hayo ni ufisadi,ambao huo hauangalii ni dini gani uliyopo,mafisadi ni tabaka la wahujumu uchumi ambalo linastahili kushughulikiwa swiftly and promptly.

  Pia bila ya kujali uko kwenye dini gani,jambo moja la wazi ni kwamba kuna positive and negative forces hapa duniani,kwa wenye kumwamini Mungu kama mimi,mtakubaliana na mimi kwamba Mungu huwa anaonyesha dalili za wapi tuelekee,na wapi tusielekee,lakini kwa maajabu,watanzania huwa wanafuata yale ambayo Mungu anatuonyesha wazi kabisa kuwa tusielekee yani yale negative ama ya kishetani shetani na ushirikina!

  Hivyo basi kama ni directions unapewa,na unaashiriwa kwamba uende east wewe badala yake unaenda west!

  Viashiria vyote vya tulipokwama vinaonyesha wazi kabisa tuko in a wrong direction,yani fikiria Taifa linaloongozwa kwa utabiri wa Sheick Yayha!

  Hata hivyo Taifa hilo hilo pia linaongozwa na Rais aliyedaiwa na viongozi wa dini kuwa ni "Chaguo la Mungu"

  Kwa kifupi matumaini kwamba sasa tumepata viongozi wapya yalijitokeza kwa wengi wetu,lakini mara baada ya matukio ya kuliangamiza Taifa kutokea,basi nilishangazwa ni kivipi Mungu akatuchagulia kiongozi anayekaa kimya ama kama inavyosemekana kuwa na connection na mambo ya kuliangamiza Taifa?Binafsi naamini Mungu atatupa dalili za direction ni wapi pa kuelekea lakini siamini kuwa anatuchagulia,uchaguzi ni wetu kwenye sanduku la kura,Mungu certainly kwa wanaomwani huwapa hekima ya kufanya maamuzi ya busara.

  Ni kweli wengi wetu tuliamini kuwa maybe JK atayashughulikia yale yaliyofanywa kwenye awamu ya tatu,lakini wenye busara walituambia hapa kuwa na yeye maamuzi mengi aliyafanya wakati akiwa waziri chini ya awamu ya tatu,lakini kwasababu ya hitaji kubwa tulilonalo la uongozi makini,tukajikuta tukimpa a benefiti of doubt na kua assume atafanya mambo kwa kuzingatia maslahi ya Taifa kama alivyokuwa akifanya JK Nyerere....Matokea yake ni kinyume kabaisa na matarajio,ni kwasababu bado tunaamini kuna tofauti chini ya tabaka moja,tabaka la ccm,tabaka la kifisadi....

  We should start Afresh;

  Ndg wana JF,ni kwanini hatufanyi hivyo?Ni kwanini hakuna mabadilio licha ya yote hayo?Ni kwanini kama Mungu anatuonyesha kabisa kuwa we're in a wrong direction lakini utabiri wa Yahya unalazimishiwa?Mijadala imeenda back and forward hapa JF,na wengine ku conclude kuwa eti "Ndivyo tulivyo" Kwa hiyo kama ndivyo tulivyo then why bother?Ama nyie ndio mnaochukulia hapa kuwa ni kijiwe?Ni kweli wakati mwingine huwa tunakuja hapa kujifurahisha lakini kuna majukwaa ya tofauti kama burudani nk,hapa ni kukata issues,kama hukati issue na unakubaliana ndivyo ulivyo basi endelea na buradani,kwasababu ndivyo walivyo wabongo wengi!"Ku mix business and pleasure" etc

  Ndg wana Jf ni lazima tuanzie hapa kujiamini;

  Pia tusia assume kuwa level yetu ya uelewa ndiyo ya wananchi walio wengi...First you have to believe in yourself and what you do before you can even attempt to achievieng anything or believing in someone else,certainly kusema ndivyo tulivyo siyo solution na pia hautaweza kubelieve in what you're doing and towards bringing any changes if you're well satisfied that thats just the way it is!

  Watanzania tunapenda pia kunyenyekewa hata kama unyenyekevu huo ni wa malengo mabaya ama usio na manufaa,na kwa unyeyekevu wengi wetu tumekuwa tukiitikia yeea...Ndivyo tulivyo!And then what? Kwa kuamini ndivyo tulivyo huwezi kufanya mabadiliko kwenye sanduku la kura kwasababu unaamini kuwa hakuna atakayekuja ambaye sivyo tulivyo?

  Kama kuna wananchi wanaona rushwa ni ishara ya upendo,basi we should do something to educate them na si kusema tu ndivyo tulivyo,same thing wananchi wanapo wasikiliza watabiri,ama viongozi wa dini wasiotumia hemika ya Mungu na badala yake kuropoka tu na maslahi binafsi,mimi naamini pia uongozi as a whole hata wa madhehebu hayo ya dini ni wa kutupiwa macho maana tunaona tabaka la mafisadi ni kubwa!

  Kama tunaamini kwamba JF ni chachu ya mabadiliko ya kifikra ni budi tuanze sisi kubadilika,kama tuna viongozi wengine kama Dr Slaa na wengineo,basi tuna hazina tayari,uamuzi ni wetu sisi,kama ilivyo kwa wengineo,Dr Slaa ana opportunity ya both ground ideas na pia ideas za hapa jamvini.

  Mambo yanayotokea hapa miaka na siku za karibuni especially kulekea uchaguzi mkuu,ni wazi kwa kila mtu kwa imani yake,kwamba huku siko Mungu anakotaka tuelekee,kwenye ufisadi na umasikini uliopindukia,Mungu anayetaka tuelekee huko tuna haja gani ya kumwamini?Ama mtabiri mwenye kutaka the same?

  Uongozi ni lazima ushiriki kwenye mabadiliko:

  Ndugu wana JF,tunasikia tu juu juu kuwa rumours za kikao kilichoitishwa na kiongozi mkuu wa nchi Mh JK,wengi wetu tunaamini hakuna la ziada litakaloleta mabadilko ya kweli,hilo linaweza kuwa kweli kwasababu the president himself has either knowingly or unknowingly been dealt with specific cards,so huwezi kuona ni kivipi he will go beyond those cards,aki proove wrong then mabadiliko yatakuwepo na uongozi utakuwa umeshiriki,vitendo pia ni muhimu,mikataba ambayo wameshaingia ya kimataifa ina kasumba ya kuwa very easy to get in and almost impossible to get out,cha kushangaza ni kwamba hakuna mabadiliko yeyote hilo limedhibitishwa na Mh Rais nasikia amefura "Kwasababu ya Dr. Slaa"

  Ina maana umakini bado haupo na hivyo hakuna jipya unlesss he's going to be dealt with absoultely new cards and something to back it up!

  Uwezekano wa kupata mabadiliko kama kiongozi aliyeko madarakani inavyoonekana anashindwa kuyaleta yanawezekana mwaka huu wakati wa uchaguzi mkuu hao december kama sijakosea.....

  Ni uchaguzi wa muhimu;

  Ndg wana JF,naomba basi niwakaribishe kwenye mjadala,kwasababu ya "Spring break"nitapata nafasi ya kushiriki mijadala inayoendelea hapa huu ukiwemo,nawaombeni basi kila mwenye kupata nafasi atueleze kuwa ni wapi tumekwama kama Taifa,na kama ukiweza(si lazima) uweke solutions kwamba what we should do to get out of this mess!

  Hapo juu nimeorodhesha sababu ambayo kuu kuliko zote na ya msingi ni uongozi na jamii,sababu manazoweza kutoa nyinginezo zinaweza kuangukia kwenye either or category,reasons zinaweza kuwa za kijamii na kisiasa,lakini ni wazi ziko interconnected,ni lazima tuzijadili kiunaga ubaga ili kusort out hizi kamba zilizotufunga na kushindwa kumove forward...hata hivyo having said that; wale wanaoamini kuwa sisi ndivyo tulivyo basi na wao wanahitajika mawazo yao,unless wanaamini kwamba kama ukiwa "ndivyo ulivyo" basi you can never change.

  Na pia kwasababu wananchi huwa na tabia ya kuwasikiliza viongozi flani flani ama watu flani flani mashuhuri,hili nalo haliwezi kuwa sababu inayotukwamisha kama viongozi hao ndiyo watoa rushwa na wanaopendwa?how can we change that mentality amongst the people?Where should we start?
  Tunajua kulekea uchaguzi muu tunahitaji viongozi kama kina Dr. Slaa,how do we achieve that?

  Nilikuwa nikishangazwa na wale waliokuwa wakidai kuwa JK anapeta uchaguzi ujao,lakini niligundua hayo ni mawazo yangu ya hapa mtandaoni.....lakini JF being blessed with people on the ground from almost every party,every religion,affiliations and beliefs....na wengine wetu wa hapa mtandaoni wenye tru passion...United as Tanzanians,first and foremost;Lets bring our ideas together as one Nation under one agenda,tuanzie na wapi tulipokwama as a Nation,and lets believe that we can,if we want it,we should get down on it
  Mnakaribishwa.
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Thank you for useful post..
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mushi, mtu huvuna alichopanda. Mwanzoni kabisa katika safari yetu kama taifa tulianza vizuri kwa kuamua kurutubisha utu wa Mtanzania kwa kuyapa kipaumbele mambo matatu ya msingi - afya, elimu na umoja. Hii misingi pamoja na kutupa heshima haikuwa rahisi kuiendeleza kwani ilihitaji uvumilivu, ustahimilivu na nidhamu ya hali ya juu. LAKINI njiani wakatokea walafi wakatafuta njia walizofikiria ni nyepesi za kufikia malengo yetu na za mkato ambazo hazikuhitaji kuzitolea jasho. Wakadai walihitaji colgate, wakadai walichoka kulishwa unga wa yanga, wakadai heri wakati wa mkoloni kuliko AD na hadi leo baada ya miaka 25 bado wanamlaumu Mwalimu. Mali, tamaa na utengano zikaota mizizi na matunda yake tunayashuhudia hadi leo kwa kukosekana misingi ya uadilifu, uaminifu na ustaarabu na badala yake kujengeka vitendo vya rushwa, ufisadi na uroho wa madaraka. Mkuu Mushi hapa tulipo all hell has broken loose and it will take nothing less than a revolution to fix it - a desperate and unfortunate action to take but sadly necessary.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  quote me: "Tulipoacha kulijenga taifa ndipo tulipoanza kulibomoa".. matokeo yake leo tunafurahia mitumba hadi ya kandambili wakati tunabeza uwepo wa kiwanda cha viatu cha BORA; leo tunafurahia mazuria toka Uarabuni wakati tulikuwa tujengeneza ya kwetu wenyewe; mablanketi yetu kutoka kiwanda cha mablanketi yanatumiwa sijui na nani (sijui kama kile kiwanda kipo anyway).. Tumefikia mahali hadi tunawaweezaji wanaotujengea vyoo kama mamlaka ya maji taka ya mbeya ilivyodokeza hivi juzi tu..
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Baada ya kubomoka limekuwa vipande, watu wanakula wanavyotaka, mpaka atokee mtu aseme; hey! wacha!

  solution...   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka kanga za Mwatex, Urafiki na Mutex, nakumbuka betri za National, nakumbuka nyama za kusindika za Tanganyika packers, nakumbuka dawa za mbu za Expel, nakumbuka baiskeli zetu, nakumbuka kiwanda cha kuunganisha redio, nakumbuka sabuni zetu za kufulia na kuogea, pombe zetu za kienyeji, nakumbuka --- n.k. n.k.(nostalgia kali !)
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tulipo kosea ni upkezi wa madaraka toka awamu ya kwanza kwenda awamu ya pili. We did not set enough precedent. The only precedent we set was on presidential terms of office na kama mnavyo ona mpaka leo hii hamna anaye thubutu kujaribu kuikiuka na ambae ana jaribu tunaona yanayo mkuta. If we had set enough precedent today "Kawaida ingekua kama sheria".
   
 8. K

  Kinnega Member

  #8
  Mar 26, 2010
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili neno la uzima limetulia kweli kweli, isipokuwa tu haliko kwenye jamvi lake.

  Sijui kama taratibu zimebadilika, lakini ilikuwa unawatumia wahusika ujumbe binafsi wakuwie ruksa kubandika mawaidha yako mawili matatu kwenye jukwa husika. Sio jamvi la siasa. Enenda na amani ya Bwana, na tazama, atakutangulia.
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Haya yote ilikuwa tunayaendesha kwa hasara, yaani behind a hoax ideology, mashirika ya umma yalikua a big lie Tanzania tukawa nchi ya kwanza duniani kuwa na kampuni za bia na sigara zinazoendeshwa kwa hasara, leo hizi kampuni mbili ndio tegemeo letu nationally katika hela za matumizi ya serikali maana kodi kubwa inakusanywa na serikali toka hapa, lakini sio enzi zile tunazoambiwa tulikuwa paradise, as if hatukuwepo vile,

  - Leo hakirushwi kitu tena, hakuna bia ya kuruka, mchele wa kuruka, sabuni imperial ya kuruka, raba za mtoni, wala ugali wa yanga hakuna tena na zile foelni za ungwa wa njano na sukari hakuna tena, labda tunamkumbuka kiongozi aliyekua serious na uongozi na maadili binafsi ya uongozi, lakini otherwise wengine tunakumbuka petroli ya kuruka na haiuzwi Jumapili, that was a very sad situation, cement ya kuruka, I mean ulikuwa ni mwendo wa kuruka kila kona ya maisha, I mean tulikwua wadogo kiumri, lakini tulijuionea mengi ya ajabu ambayo tukiwaambia vijuana wetu wa kisasa hawaamini kabisa kama ni kweli!

  - Hatuwezi kujinasua kwa sababu hatujui hata tuliponasia ni wapi na tumenasa na nini, tutaendelea kuzunguka tu bila kusonga mbele kwa sababu mifano hakuna!

  Respect.


  FMEs!
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Alipokufa Sokoine naona hakukuwa na mtu mbadala wa kupokea kijiti kutoka kwa Nyerere. Waliofuatia walileta hadithi ambazo uzuri zimeanza kuwasuta wangali bado hai kwamba walivurunda.
  Sokoine ndiye aliyetaka tujifunze kutumia vichwa vyetu kutafuta maendeleo. Hakulea lea huu upuuzi wa mtu kuhutubia hotuba ndefu akijisifia kuruhusu watu kuvaa mitumba, akasahau viwanda vya ndani vya nguo vinakufa.
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280

  Tumejipa likizo ya kutotumia vichwa vyetu na kwa kweli hatujajua tatizo liko wapi.
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Tunawaheshimu Sokoine na Mwalimu only kwa sababu hawakuwa mafisadi, lakini kwa hali tuliyonayo ya kuvuna walichopanda hakuna cha kuonyesha, hili taifa hatujawahi kuwa na viongozi wenye uwezo wa kuongoza, tizama kina George Washington, waliyoyapanda mpaka leo yapo, sisi imekwua exuses tu kila siku tufike mahali tukubali ukweli tu kwamba we never had it!

  - Viongozi wenye uwezo hujenga institutions na policies imara ambazo hata wakifa au kuondoka hapahitajiki watu mbadala wa kupokea vijiti vyao, Rais mbovu kama Carter huondolewa kwa kura after one term, lakini sisi alimaliza term zote mbili, sasa tutaendelea kulaumiana tu ni wewe ni yule sio mimi, yaliyopita si ndwele sasa tutafute yajayo!

  Respect.


  FMEs!
   
 13. m

  miner Member

  #13
  Mar 27, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumekwama kama Taifa kutokana na mambo makuu 4.
  1. Siasa
  2..Mipango
  3.Usimamizi
  4. Utekelezaji
  Mwl. Nyerere alipata kusema ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi na siasa safi.Watu wapo na ardhi pia tatizo ni siasa mbaya kama leo TIC wanatagaza kugawa ardhi yetu kwa wakoloni walewale kulikua na sababu gani ya kudai uhuru na kujitawala Watanzania ni lazima tukatae tena kwa kijitoa hadharani na silaha zetu za jadi kama walivyofanya wananchi waliodai ardhi yao waliyopewa Nafco.
  Tutaendelea vipi kama hatuna mipango. Mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka 5 ulikua 1965 hadi 1970 nawa pili 1970-75 baada ya hapo nchi imepelekwa wanavyotaka watawala hebu angalia awamu hii tu miaka ya uongozi wa Lowasa ilikua Elimu na kipindi kilichobakia katika awamu hii chini ya uongozi wa Pinda ni kilimo hakuna tena ujenzi wa madarasa kwa kasi ile sasa halmashauri zinashindana kununua power tillers.
  Tutaendelea vipi kama hatuwezi kutekeleza yale tulioamua na kuyasimamia ipasavyo ni wajibu wetu sote kuchukua hatua sasa.Nabii Mussa aliwatoa wana wa israeli misri akatangatanga nao jangwani na hakuwafikisha katika nchi ya ahadi ya maziwa na asali na CCM wametutoa katika ukoloni leo miaka 48 tunatangatanga na umskini , shida na taabu kamwe hawatatufikisha kwenye neema tele ni lazima tuchukue hatua..NDIO TUNAWEZA ; PAMOJA TUNAWEZA.
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Well said mkuu,wananchi nao pia wanachoshindwa kuelewa ni kwamba hata nabii Musa mwenyewe hakuiona kanani ama nchi yenye maziwa na asali,waliopata bahati hivyo kwa mujibu wa maandiko matakatifu ya kitabu cha biblia ni Joshua mwana wa nuni na Khaleb "mwenye imani"

  kwahivyo ni kweli kwamba ccm imetuondoa Misri lakini si lazima itufikishe kanani kwenye nchi yenye maziwa na asali,hapo ni mojawapo ya sehemu tuliyokwama,mwalimu mwenyewe ambaye kuna waliothubutu kumwita "Mussa" na hata hivyo kama ilivyokuwa kwa Mussa,ametutoka kabla ya kuiona hiyo nchi yenye maziwa na asali,tutapata wakina Joshua wetu na nuni kama tukiamini kwamba mabadiliko ni lazima na pia kuachana na yale ya kale...Pamoja tunaweza kufika kama tukichukua hatua!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa umenifanya nifikirie sana; inawezekana uko sahihi kuliko unavyowezea kujua maana kama unayosema ni kweli basi yawezekana matatizo yetu baada ya uhuru hadi alipokuja Mwinyi hayakuwa makosa ya Mwalimu! Hakukuwa na watu wa kutekeleza zile njozi zetu za taifa. Ingekuwa vigumu sana kwa Nyerere kufanya kila kitu yeye mwenyewe; kiongozi ni lazima awe na watu anaowategemea.

  Leo hii mojawapo ya mambo tunayogongana nayo katika uongozi wetu ni kama abebe lawama Kikwete au wasaidizi wake. Kwa kiasi kikubwa tunaambiwa ni wasaidizi wake ndio wanamuangusha, lakini upande mwingine tunasema "the buck stop with the president".

  Je Rais yeyote anaweza kufanikiwa bila ya kuwa na watu anaoweza kuwaamini kutekeleza sera na maagizo yake?

  Je, wale wanaodhaminiwa nafasi mbalimbali wanatakiwa wasimamiwe na Rais kwa kila kitu ili wakifanikishe?

  Kwa kweli inawezekana tatizo letu la uongozi ni kubwa zaidi kuliko ni Rais gani yuko madarakani.
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Tunaweza kusema tatizo kubwa la kufa kwa nchi hii lilikuwa ni upungufu wa wasomi katika kila fani, Nyerere alifanikwa kuanzisha viwanda vingi na vya maana, lakini ilikuwa nani wa kuvisimamia?, huwezi kiwanda kikubwa kama Urafiki Accountant awe la nne la zamamni au kada mzuri wa TANU ndio awe meneja,

  mimi mpaka sasa nikiwa nafatilia na kutafakari sera na miongozo mbalimbali ya Mwalimu naona mpaka kwa karne hii tuliyopo bado inatufaa sana, ni kiasi cha kujitwist kidogo na turudi kwenye basics, tuchukue yale Mazuri ya mwalimu na tuyafanyie kazi

  kwenye hiyo point ya ili "tuendelee tunahitaji mambo manne" hapo ndio msingi mkuu wa nchi yetu na maendeleo ulipo

  1:WATU, Huwezi kuendelea bila kuwa na watu, lakini si watu tu mwalimu anakwambia
  mtu lazima apate CHAKULA, MAVAZI NA MALAZI, NA PIA APATE ELIMU NA AELIMIKE (kwa hili mwalimu alijitahidi)

  2;ARDHI, Miongoni mwa mambo ambayo mwalimu alifanikwa kwa asilimia kubwa ni kuitunza Ardhi ya Tanzania na rasilimali zake na alikuwa anafanya kwa Maslahi ya Watu wote walikuwa kipindi chake na kwa faida ya vizazi vijavyo

  3: SIASA SAFI, Hapa ndio labda kunakuwa na tatizo kidogo kutokana na misimamo na miono ya watu tofauti, lakini kwa mtazamo wangu, by that time ile siasa ya Mwalimu ya ujamaa na kujitegemea ilkuwa ni SIASA SAFI, kwa maana kuwa; kwanza nchi ilikuwa hiko kwenye majimbo ambayo mengi yalikuwa yanasimama kwa misingi ya Ukabila au Udini, Kama sio ile siasa yake ya ujamaa basi sidhani watu kama Mwalimu (Mzanaki), Mwinyi (Mndengereko)Mkapa (Myao), Kikwete (Mkwere) wangeweza kuwa Maraisi na kuwaongoza watu walikuwa na maendeleo ya hali ya juu mno (Wahaya, wWachaga, Wanyakyusa),
  pili nchi ilkuwa haina misingi wala njia za maana za uchumi, NANA mara nyingi tunajifafnanisha sana na Wakenya, au MAlawi, hizo nchi zilikuwa na program za kiuchumi za kimagharibi tofauti na Tanzania, YAANI NI UKWELI USIOFICHIKA NYERERE ALIKUWA NI MWAFRICA WA KWANZA KUJENGA NCHI NA VIWANDA VINGI VYA KISERIKALI NA AMBAVYO VILIFANYA KAZI YA KIMAENDELEO, na hii ilitokana na imani yake na siasa yake aliyohihubiri ya ujamaa na kujitegemea NA NDIO MAANA KWA MTAZAMO WANGU MIMI NAONA ILKUWA NI SIASA SAFI

  4: UONGOZI BORA: Hapa nadhani panaweza kuwa palikuwa na Tatizo, labda tusiweke kuwa kiongozi bora ni yule asiye kula rushwa ama kujirimbikizia mali, nadhani Tatizo hapa lilikuwa ni upeo, japo kulikuwa na viongozi walikuwa commited, lakini wengi hawakuwa bora, katika kutumia uwezo binafsi wa kusimamia na kutekeleza sera za kimaendeleo, nadhani palikuwa na Tatizo kubwa la kielimu, by that time SIASA ILIKUWA NI KWA WASIOSOMA, ILIKUWA NI SHIDA KUKUTA INJIA AU DOCTA KUWA MBUNGE

  hitimisho
  KWA MTAZAMO WANGU NDANI YA HIZI FILOSOFIA NA MIONGOZO MINGI YA MWALIMU KUNA KITU KIZURI ZA KUSOMA, LETS GO BACK TO BASICS
   
 17. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya yote uliyoyasema ni lini yalianza? Kulikuwa na mambo mengi yaliyochangia mawili yakiwa ni kupanda kwa bei ya mafuta na vita vya Kagera. kupanda kwa bei ya mafuta kwenye miaka ya 70 hadi 80(energy crisis) pipa moja la mafuta ghafi lilifikia $ 39.50 April 1980, hakukuithari Tanzania peke yake bali dunia nzima. Hilo la vita vya kagera you can build a case kwamba lengo ilikuwa kumrudisha Obote. Ila je hayo mabomu waliyopigwa huko kagera ilikuwa ni janja ya Nyerere ili ionekana tumechokozwa?
  Viwanda vyote vilivyotajwa vilikuwepo na vilikuwa vikifanya vizuri sana General tyre ilisifika kwa matairi yenye ubora wa hali ya juu. Viwanda vya nguo ndio usiseme. Msingi ulikuwepo tatizo watu wa ku-manage ndio hawakuwepo. Hawakuwa wa kwapuaji kama hawa wa sasa waliingiza hasara kwa kukosa utaalamu wa kuendesha mambo. Vitu hivi vilikuwa real huwezi kuvi-lebel as hoaxes.
  Hivyo viwanda vya bia na sigara faida yake haipo kwetu wanachukua makaburu na wajapani sisi tunatupiwa makombo. NBC hakuna kitu hapo lakini miundo mbinu ya vyote hivyo ni ileile wameongezea kidogo tu kwa bia na Sigara. Tulikuwa na reli hata kama ni ya kurithi ikifanya kazi vizuri leo yako wapi?
  Tulipokwaama ni pale tulipoaamua kuwa na upendo wa mshumaa kumulikia watu huku wenyewe unateketea. Tatizo letu ni kuchagua viongozi wabovu.
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Mkuu FMES Heshma mbele!
  Je una maananisha hatujui kwamba uongozi mbovu ni sababu kuu ya kukwama na kwamba solution ya kujinasua among others,haiwezi kuwa mapinduzi?
   
 19. D

  Donrich Senior Member

  #19
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tanzania inahitaji kiongozi mwenye uchungu na Watanzania,viongozi kama Nyerere na Sokoine(R.I.P) ni vigumu kuwapata kwenye zama zetu hizi.
   
 20. m

  miner Member

  #20
  Mar 27, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana lakini sitaki kuamini hivyo. Tatizo ni mfumo si kiongozi naomba nifafanue kwa lugha nyepesi mfumo ni sawa na gari huwezi kufika unakokwenda kama gari ni bovu hata ukiwa na dereva mzuri kiasi gani (kiongozi) ili uweze kufika salama uendako una njia 2 tu za kufanya ama uuze hilo gari bovu ununue gari nyingine imara ama ulikarabati kwanza (major overhaul) sasa zama za Nyerere na sokoine gari au mfumo waliokua wanausimamia ulikua bora kiasi .Sasa mfumo huo (gari) limeoza halifai na wala hauwezi kulikarabati tena njia na suluhisho la pekee ni kunnua gari jipya (mfumo mbadala) ili tufike huko tunakotaka kubadili dereva pekee haitoshi.
   
Loading...