Tuliowahi kukaa gerezani tupeane uzoefu wa mateso, msoto na vimbwanga

Hapo kuvua nguo ni mkiwa mnakaguliwa kabla ya kwenda vyumba vyenu huko ni case za Marekani ambako jela Zina facilities nyingi na vitanda, huku bongo land sijui Ila baada ya kuchekiwa mnavaa nguo zenu kawaida
Mkuu mm sijafika marekani na ulaya ila kwa kuangalia muvi za kihalifu wanapofikishwa jela naonaga hawavuliwi nguo kama huku ila wanakalishwa kwenye kiti wenyewe wanaita boss chair kinachitumika kuscan kama umeingia na kitu matakoni.
 
Waafrika wanasurvive jela sababu maisha yenyewe tu ni jela tosha,
Thus weupe upewa semina fanya uwezavyo ikibidi rushwa usiingie jela za afrika,pia nchi zao fasta huwa zinapambana kuhakikisha awakai Sana jela.
Kuna jela ziko friendly sana Tanzania zina wafungwa watano, saba au hata wawili na zingine hazina kabisa.

Na wafungwa wake wana namba ndogondogo tu.
 
Mkuu mm sijafika marekani na ulaya ila kwa kuangalia muvi za kihalifu wanapofikishwa jela naonaga hawavuliwi nguo kama huku ila wanakalishwa kwenye kiti wenyewe wanaita boss chair kinachitumika kuscan kama umeingia na kitu matakoni.
Huwa wanavuliwa nguo fatilia series inayohusu jela za Marekani national geographic huonyesha pamoja na treatment zao, kuvua ni must pamoja na hzo scan nyingine, bila kusahau kunyoa upara
 
Mkuu mm sijafika marekani na ulaya ila kwa kuangalia muvi za kihalifu wanapofikishwa jela naonaga hawavuliwi nguo kama huku ila wanakalishwa kwenye kiti wenyewe wanaita boss chair kinachitumika kuscan kama umeingia na kitu matakoni.
Kuna documentaries nimewahi kuangalia za magereza ya marekani huwa wanavuliwa
 
Hizo ni za VIP anapowekwa mbowe,Lisu sio unapowekwa mwizi wa kuku
Sir kama hujui kitu unauliza.
Hizo jela friendly nilizozitaja ziko vijijini kabisa.

Jela wanazowekwa kina Tundu Lisu na Mbowe as you've said (japo nimekutukana tusi konki sana) huwa zina wafungwa watano, saba, watatu au huwa hazina kabisa? 😏
 
Chooni nyapara anajifanya anaenda kujisaidia kumbe kashamtanguliza mtu wake wakienda kule mnajuajua mtu anajisaidia kumbe anapumuliwa... or wakati mwingine mchana kbsa chooni kuna vyoo havitumiki mchana so Nyapara anaweza mchukua demu wake akamwambia WEWE TWENDE UKADEKI HUKU hapo wanakua washakubaliana so wakienda kule ni tukio la chap kwa haraka, sazingine hata usiku wakati wa kulala...Si wanajifunika Shuka moja ndani mambo yananendelea kimya kimya.

Hiyo ishu inategemea tu na makubaliano yenu na mazingira mtayoona yanawafaaa nyie wawili ndio mana nkasema ni tendo ambalo hulazimishwi Unaridhia kabisaaa halafu sazngine Mpumuliwaji ndio anatoa location wapi pazuri ambapo hawatoonekana.
Daaaah, unasikitisha sana hii aisee. Mwanaume unaingia jela ukiwa mzima ila unatoka ukiwa huna rinda hata moja. Ee Mola tuepushe na kadhia hii.
 
ACHENI IITWE MAGEREZA ISIKIENI TU KWENYE MARADIO NA ISOMENI KWENYE MAGAZETI ILA USIOMBE KUINGIA.

Ilikua kama utani bwana niliingia na kesi 1 hivi,nikajua nitatoka kesho kutwa maana si unajua wazazi maisha si haba,ndugu wako njema halafu nilidakwa mfukoni nikiwa na kama 1m alafu kilichonipa moyo ni GEREZANI ni mkoa huo huo na nyumbani kwetu so nikajua hata iweje mimi ndani simalizi 24hrs ntakua Nshatoka.

Utani utani masaa 24 yakaisha,wiki ikaisha, mara mwezi ukakata Maisha yakaanza hapo nipo gerezani kama MAHABUSU naendelea kwenda mahakamani na kurudishwa,taarifa zikafika kwa ndugu,wazazi,marafiki,wanafunzi wenzangu chuo kizima wakajua LAKINI nilichoambulia ni kuja kuonwa VISITORS DAY j.mosi na j.pili nahiyo ni kwa miezi ya mwanzo tu ambayo badae walikata mguu nikawa naishi kibishi.

Ki ukweli maisha yyake ni mabaya na hatari sana nakumbuka day 1 naingia Nilinyolewa AFRO langu nikawa paraaaaa nikaona fresh tu,usiku wakati wakulala kuna CELL ya RECEPTION/MAPOKEZI huko ndio wageni wote lazima mpite siku ya kwanza kwa ajili ya kufundishwa sheria za JELA na jinsi ya kuishi JELA..na sharti lao ni kila unachoambiwa unatakiwa ujibu NDIO BWANA MKUBWA

wakati wakufundishwa sheria sheria kuna muda nikaulizwa swali nikajibu NDIO
ALITOKEA nyapara mmoja sijui alitokea wapi alikua mbavu vibaya mno alafu alikua anaharufu ya kilevi Alinizaba KOFI moja hatari sana niliskia sikio linalia ng'wiiiiiiiiiiiii kisha akaniuliza tena swali...Nilijibu NDIO BWANA MKUBWAAAAAAAAA. (akasema safi sana)

Baada ya kujua sheria ukafika muda wakulala,style ya kulala inaitwa MCHONGOMA EEEh bwana eeeeh mfano wa mchongoma wenyewe kwa msio jua ni JINSI biskuti zinavyopangwa kwenye kibox chake halafu ni kwa ubavu mnalala basi nikaambiwa haya lala hapa nikapangwa na Jamaa mmoja ananuka,mchafu,ana damu raia walimpiga huko nnje yani full Kinyaa ila siku na jinsi nilijibanza.(kusema ukweli first day hadi week inakata sikuweza kulala) nilikua nakaa macho then tukiamka asubuhi naenda kulala nnje sakafuni maana mkitoka ndani hamna mtu anaebaki wote mnaenda MESSi.

basi asubuhi palivyOkucha siku ya kwanza Wageni wote tukaitwa kwa bwana jela Kuandikisha URITHI..hapa bwana sikua najua urithi ni nini? mimi nikawa najiuliza URITHI gani mimi naenda kuandikisha wakati sina nyumba,gari,wala baiskeli? basi tukaenda kwa bwana jela Kumbe bwana urithi unaoongelewa ni MWILI WAKO UKIFARIKI AKABIDHIWE NANI?? basi nikasema nikaulizwa kabila,elimu,nk nk. Kisha tukatoka.

Akili yangu inawaza sasa nimeandikishwa urithi ina mana humu ndani kufa ni muda wowote? asee nilikua na maswali mengi sana...Baada ya kutoka kwa bwana jela Wageni tukaitwa woteee KWENDA kuchambua marage,wakati tunachambua marage alikuja kiherehere (kiherehere ni cheo kama ilivyo unyapara) akatupoint watu kama 6 hivi kwa ajili ya kwenda kudeki mtaro ule mtaro ambao watu wanaswakia huko,wanatema makohozi,wanatema mate huo mtaro kwa jina lingine kule wanauita kile kiungo cha hawa wadada zetu kinachotumika sana kama TUSI (Ku....) haya tukapewa madekio tukadumbukizwa jaman jaman jaman acheni kabsaaaaa sio kwa kinyaaa kile nakumbuka siku ya kwanza nili tapika.

Basi tukadeki badae kazi zingine za kawaida zikaja KWA ufupi wageni mlioingia JANA siku ya leo huwa mtafanya kazi hadi mkione cha mtema kuniiiii..pona yenu ni wageni wataokuja LEO,maisha yaliendelea na nikiwa naendelea kwenda mahakamani,SIKU MOJA Nikiwa magereza Nikaumwa sana sana ikafikia hatua ya kulazwa basi ikabidi nipelekwe hospitali kulazwa na askari wa magereza so nikawa natibiwa kule nimepgwa dripu huku nina pingu yangu mkononi, askari wanabadilishana zamu tu...nikaendelea kukaa hospitali kama siku 3 siku ya nne kuamka nilikua mzima kabisa kabisa.

Sasa wazo la kutoroka likanijia nikasema leo iwe iwavyo sirudi magereza,,,,nakumbuka hiyo siku nilijitapisha nilijitapisha uongo,nikawa naomba kwenda choooni wakinipeleka wakati wakurudi Najidondosha najifanya nimezimia wananibeba nawaskia wanasema (huyu bado anaumwa sana sana) basi kuna muda nilijizimisha uongo wakanieka kitandani askari akasahau nifunga PINGU...nikawa nimejifanya nimelala sasa nkasubiri usiku uingie kwa kua wodini hospitali taa hazizimwi usiku nikasema usiku ukifika leo naamsha.

Usiku ukafika akapangwa zamu askari mmoja hivi mlokole mlokole nikamuita nikamwomba anipeleke chooni Akanipeleka akaniacha NIKAINGIA nikajifungia ndani..nikapanda juu ya ndoooo nikatokea dirishani NDUKIIIIIIIIIIII....mzeee nilikimbia nikafanikiwa kutoka nnje ya hospitali...Sina hata sh kumi mfukoni nikaita boda boda Nikamwambia nipeleke sehemu flani...Akawasha chombo akanipeleka kufika yale maeneo nikamwambia nisubiri nichukue hela nije tuondoke jamaa akawa ananisubiri pale nnje Eeeh bwana niliingia njia moja nikatokea mtaa wapili NDUKIIIIIIIIII....

Sasa nilivyo mjinga mjinga wakutupa Unakumbuka nilisema mwanzo gereza lipo mkoa ambao ndio nyumbani so usiku mida ya saa nane hivi nikaanza kujirudisha nyumbani mdogo mdogo nikiamini hamna atakae niona,kumbe wakati huo narudi nyumbani Kule hospitali walishajua nimetoroka na kwakua mshua wangu ni famous Walishajua huyu ng'ombe lazima karudi kwao,askari kama 20 hivi waliokua off wakatumwa home wakaulizia hadi wakafika..

Kufika wakamkuta bi mkubwa akawambia Huyu mtu hayupo huku wala hajafika,basi wakawa wanataka kuingia ndani wakanyimwa maana geti lilifungwa so wakawa pale nnje wanasubiri pakuche wafanye utaratbu wa kuingia ndani kunitafuta soo nyumba yetu nzima ilizungukwa na askari.

Mimi huku sina hili wala lile najikongoja peku peku narudi nyumbani usiku mida ya saa tisa inaenda sasa nikasema sipiti mbele ya geti acha nizungukie huku nyuma niruke ukuta nichome ndani eeeh bwana nilisikia nimedakwa alafu mtu anasema (oyaaaa mtu wetu huyu hukuuu) aseee nilichangiwa na wale askari wakunipiga kofi alinipiga,wakunipga teke alinipiga,bwana nilipigwa kisawa sawa BAHATI NZURI ilikua usiku so mtaani hawakuniuzisha sura sana ila nilichapika aseee.

Nikafikishwa magereza nikakuta mkuu wa magereza kaja akakuta natoa damu, akaanza wagombeza askari kwanini wamenipiga basi nikaskia wameambiwa waandike maelezo mimi nikaingizwa ndani kupewa first AID kisha nikaambiwa bwana saivi hata uuumwe mpk unye hospitali hupelekwi.

kesho yake pakakucha Bila kulaza DAMU nikapelekwa mahakamani kwa kosa la KUJARIBU KUTOROKA nikahukumiwa MIEZI MI 3 so nikarudi magereza nikavaa RASMI GWANDA la rangi ya CARROT na sare yangu ikashonewa kkwa nyuma kitambaa chekundu kuonyesha mimi ni Mfungwa mtoro so askari wakae makini na mimi. Basi bwana lile bata lakukaa ndani kama mahabusu likaisha nikaanza kupangiwa MAGENGE ya kkwenda kazini.

Siku ya kwanza kazini tulienda kulima bustani...(Bwana usisikie bustani ukafkiri ni bustani za nyumbani) mzeee hzo bustani ni kiboko unalima hadi unasema eheeeeeeeeeee kumekuchaaa....siku yakwanza ikaisha ikaja siku nyingine nikapangwa shambani Kaaaaaah jamn magereza Shkamooooo nililima hadi mikono ikawa na malenge lenge ya maji Nikasema kimoyo moyo MIMI BORA NIFEEEEE siwezi kukubali hizi kazi.

Siku nyingine tukapangwa kwenda kupasua kuni Nikasema LEO NATOROKA kama risasi nipigwe ila mimi leo Nasepaaaa..Tukapewa mashoka kazi ikaaanza pasua kuni pasua huku nachora ramani askari kakaaaje na nyapara kakaa wapi,basi kuna muda nyapara alitumwa na askari akatuacha wenyewe na kihere here wetu...Alafu kihere here alikua anavuta sigara kimya kimya so akili yake yote ilikua kwenye GOZO lake...aseeee NILIKURUPUKA KURUPUUUUU nikaingia poriniii kimbiaaaa mbeleee nikatokea barabarani kila boda boda hanitaki maana nina jezi Nikaona isiwe kesi Nikavua shati nkatupa huko nikabaki kifua wazi.

Huku nyuma niliwaacha distance sana maana sikuwaskia tena kwa mbio nilizochomoka hata DREAM LINER isingenipata kwa muda ule..basi huko barabarani nikawa najaribu bahati ya lift ila bahati yangu ilivyo mbaya tena asee mbele nilikutana na watu kibao wakawa wanasema MFUNGWA YULEE KATOROKAAA wakaniungia wakawa wananfukuza RAIA shaziiiii fukuzwaaaa aseee niliona kifo hiki hapa bahati nzuri ikapita gari ya magereza nikaisimamisha nikarukia ndani ili kuokoka kwa wale raia...askari akawa ananiuliza wewe UMETOROKA si ndio nikamjibu NDIO (akanipa kofiiiiii) akanambia leo tunaenda kuvunja hiyo miguuuu.

Asee hakunipeleka magereza alinipeleka kwa askari wengine walinipiga runguuuu,pigwaaa hadi miguuu ilivimba hadi nikaona sasa leo habari yangu kwishaa..Nikarudishwa magereza nimebebwa kama nmekufa askari wengine wakawa wanashangaa vipi huyo kibaka anaumwa?? wakasema hapana alikua ametoroka tena ndo tumemdaka basi Pona yangu ni mkuu wa magereza alikua pale akasema msimpige tena huyu mtoto atakua huyuko sawa kiakili,wala msimpeleke mahakamani HUYU AFANYE KAZI ZA NDANI TUUU MSIMTOE NNJE.

hiyo ndio ikawa pona yangu kuanzia siku hiyo mpk kifungo kinaisha na kesi yangu ikaja kuisha mwenzi wa 12 ambapo ni baada ya habari zangu kufika nyumbani kwamba mtoto wenu huko magereza atakufa basi ndio wazee imani ikawajia wakaingilia kati wakatoa mpunga kidogo HAKIMU akaja nihukumu miezi 6 kifungo cha nnje...

Ila ni moja ya kumbukumbu MBAYA SANA KATIKA MAISHA YANGU ambayo sitokaa niisahau...ku spend MWAKA MZIMA magereza ASEEE.

Sikuwahi kujua wanaume wanatongozwaje ila NILITONGOZWA na niliona huwa inakuaje..Sikuwahi kujua na kuona watu wakigombania mwanaume ila niliona.

HAYA NI MAJINA YA WANAUME LIVE ambao wakija uraiani WADADA MTAWAKIMBILIA NA KUTAKA MUWE NAO ila kule ndani ni mashoga...Nilikuta mtu anaitwa RAY C..BI KIDUDE, JAY DEE,CHA WOTE,nk nk

KWA MSIO JUA JELA MSIOGOPE MAANA kugeuzwa mwanamke ni wewe mwenyewe utataka ila hulazimishwi na mtu yeyote na wala nyapara hawezi kukulazimisha umpe TIGO ni wewe mwenyewe na roho yako ya huruma..

INAKUAJE MTU ANALIWA TIGO

Ukifika ukiwa mgeni kuna kitu wanaita KULEGEZA,,,kulegeza ni ile style wanayofanya manyapara ukifika tu akishatuthaminisha unafaaa,akikuona yeeesss hili toto zuri Anachofanya ni kukulegeza kwa style ya kukupa kazi..ebwana wee utafanyishwa kaziiii,utafanya kaziii yani hiyo haina kupumzika...tangu uamke hadi mnaenda kulala ni anakupa kazi.

muda wakulala ukifika anakupanga godoro lenye chawa kama woteeee..anakupanga sehemu ambazo ni mara 100 ulale jalalani ila sio ulale na hao watu ndio anapokupanga..Halafu sasa baada ya misoto yote hiyo Kuna siku utakua unamuona anakua mwema kwako..Mchana muda wakula anakwambia mdogo angu njoo ule..akikuta unafanyishwa kazi anakwambia ACHA KAPUMZIKE..wakati wakulala anakupanga kuzuriiiiiii.


Ukijifanya ukijifanya mzuri wa kupokea OFFER shauri yako ila raha ya MAGEREZA NI KWAMBA sio kama huku uraiani huku mdada akila vyako alafu hataki kutoa mzigo unaweza mfanya lolote,tofauti na magereza mtu ukila vya mtu Wakati wakutoa mzigo ukigoma HANA CHA KUKUFANYA ZAIDI TU atakua adui ako mileleeee.

So kama utajitia muoga muoga unataka kulipa fadhila watu wanazamisha PENSELI....

(msiogope magereza ila ukweli ni kwamba ili usiogope ni lazima ujue maisha ya kule ndani yakoje) SEMA KULE SOMETIME pamoja na mabaya ila kuna muda unasahau shida unaweka miguu juuu HASA ukishakua SHINDIKANA kama mimi nilivyokua basiiiii ugali unakula wakinyapara,harage la kuunga,maziwa kule ni daily yani daily kwa ajili ya watu wa TB so ukishakua mndewa UNAVUTA TU MAZIWA KILA DAY.

kasoro ya kule isiyozoeleka ni UHURU. ILA mengine yote yanazoeleka na yana muda hayadumu milele hata mateso ni ya muda tuuuu sema ndio tumetofautiana..

NOTE: SIO lazima kila anae ingia magereza apitie msoto,kuna wale wanaingia wanakuta ndugu zao,marafiki so shida hawapati na kingine kama hutaki shida ukiingia mule ndani hata kama huna ndugu wala rafiki basi Uwe na visitors kila jmos na jpili yani uwe unaletewa mavitu ya uraiani kama masabuni,machakula,masukari (hii ndio ilinifanya nisijue mateso ya magereza)

PAMOJA NA YOTE HAYO KAMA UPO URAIANI EPUKENI UGOMVI,SHIDA NA MTU,CHUKI,MANENO MABAYA YANI KAMA UNAWEZA KUISHI MAISHA YA KUEPUKA MAGEREZA BASI YAISHI HAYO MAISHA NA ISITOKEE UKAKUBALI KUINGIA.

KAMA UMEPATA TATIZO HATA KAMA UMESINGIZIWA KAMA UNAWEZA JISHUSHA JISHUSHE ILA USIINGIE MAGEREZA NA ENYI WAZAZI WENZANGU MSIJE MKAJIDANGANYA MAGEREZA INABADILI WATOTO TABIA SO MUWAPELEKE athubutuuuu KAMA MNATAKA WATOTO WENU WAWE MARA 20 YA HAPO WALIPO WAPELEKENI MAGEREZA WAKAKUTANE NA MAJAMBAZI WAPEWE TECHNIQUE ZA KAZI..KULE WATU WAPO SOCIAL KABISA YANI KUNA MUDA WATU WANAPIGA STORY NA WANAELEKEZANA JINSI YA KWENDA KUIBA BILA KUDAKWA..JINSI YA KUBAKA BILA KUACHA ALAMA,JINSI YA KU UA BILA KUACHA ALAMA...JAMANI MSIPELEKE MTU MNAEMPENDA MAGEREZA.

ENYI AKINA DADA MSIPELEKE WAUME ZENU MAGEREZA MAANA WAKITOKA HUKO WAKIJA NI WATAKUA KATILI KULIKO MWANZO MALIZANENI URAIANI ILA USIJE UKAFKIRI AU KUMTISHIA MTU KUMPELEKA MAGEREZA MAANA AKITOKA HUKO ATAKUA SIMBA MARA NNE.

ENYI MNAOWADAI WATU EPUKENI KUPELEKA WENZENU MAGEREZA MAANA WAKITOKA KUNA MAWILI AWE MPOLE AU AWE SIMBA AKUPOTEZE NA KIZAZI CHAKO..

KABLA YA KUINGIA MAGEREZA NILIKUA MUOGA HATA WAKU UA MMBU LAKINI SASA HIVI ADUI ZANGU HUWA NAWAZIKA MWNYEWE..SIKUSHTAKI POPOTE WALA SIKUPELEKI MAGEREZA WALA SIENDI POLISI KUKUTAFUTA NINACHOFANYA NI NAKUTAFUTA MWENYEWE NAKUZIKA KIMYA KIMYA SIKUWAHI KUWA NA HII ROHO ILA SASA HIVI NIMEKUA MBOGO + LION GOMBANA NA WOTE ILA SIO MIMI.

TUISHI HAPA URAIANI KAMA WAJINGA YANI ISHI KAMA MBUMBUMBU ILA ENJOY YOUR FREEDOM MAGEREZA NI PABAYA JAMANI...ISHI KAMA MJINGA ILA USIKUBALI WAKUCHOKONOE HADI MACHONI WANAPOZIDISHA..WAZIKE.

POLISI,MAGEREZA,NK HAMNA HAKI ANAEKUKERA AU KUKU UDHI KAMA HUWEZI MSAMEHE BASI USIMPELEKE MAGEREZA WALA HUKO POLISI MTAFUTE KIMYA KIMYA kata shingo mzike mahali TULIA.

nachukia mapolisi,nachukia watu wote wanaoPELEKA WATU magereza nawachukia mno.

(mliosoma yote mnajitahidi ki ukweli)
 
Mkuu mm sijafika marekani na ulaya ila kwa kuangalia muvi za kihalifu wanapofikishwa jela naonaga hawavuliwi nguo kama huku ila wanakalishwa kwenye kiti wenyewe wanaita boss chair kinachitumika kuscan kama umeingia na kitu matakoni.
Marekani labda ila Ulaya hakuna kitu kama hicho!

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom