Tuliowahi ku disco chuo tukutane hapa tushee historia zetu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,723
Usipmbe udisco chuo hasa kama wewe ndio kiongozi wa familia
Kiufupi sijawahi kua na historia ya kufeli toka primary ila kufaulu tena kwa daraja la kwanza O level&A level.Baada ya kujiunga chuo mlimani 2010/11 kwa kozi ya B.A.Economics nilifurah na kua proud of kwa kujiunga na kozi niliyoipenda na chuo kinachopendwa na wengi
Harakati za masomo zikaanza na upande mwingine siasa zilipamba moto miaka hiyo chuoni,akina Shonza,Hapi,Al shababu na wengine wengi.Kila uchaguzi wa daruso au mambo ya boom kulikua na kambi mbili za uvccm na bavicha zinashindana revo.square.Nikawa trapped na kupenda sana siasa hadi mala ya mwisho tulisotea sana na kesi kule central baada ya police kutukamata pale survey kwenye maandamano.Hayo ni baadhi tu ya matukio mengi ya kisiasa yaliyokua yanafanyika miaka hiyo 2010-2012,Kawambwa akiwa waziri wa elimu anajua vizuri
Nikaanza kuyumba kwenye matokeo makalai na Sapp zikawa zinaninyemelea,mbaya zaidi ukiacha kushiriki matukio ya kisiasa ndani na nje ya chuo nilikuja kushuka sana molari ya kusoma na kuichukia kozi ya ndoto zangu,sababu nilikua nikisoma magazeti library sioni ajira zinazohusiana na kozi ya uchumi nikawa nahisi nimepotea.Mwisho wa siku nikajikuta nabipu kusoma huku mda mwingi kwenye matukio ya kisiasa,magazeti ya siasa hasa mawio,na nikaanza kunyemelea mafunzo ya motivational speaker wa biashara hasa za mtandao.Slogan yangu mpya ikawa ni GPA haiwezi kunitoa.
Nikiwa Field ofisi za ESRF kijitonyama kucheki Aris second semester mwaka wa pili nimedisco kwa gpa ya 0.7,nilipata shoku lakini nikawa resilient fast nikawa nikawa nafikiria nini Cha kufanya huko nikisema ntaanzaje kumueleza mzee,nikaondoka field bila kumaliza
Nikaondoka kwenda Swax japo sio kwetu ila kuanza maisha,nikakaa wiki nikamweleza bro akamweleza mdingi aisee ilikua kasheshe,hapo ndo nikajua uchungu wa mwana aujuae mzazi.Nikatulia naunga unga kazi za zege swax Kama mwezi wakacool down nikarudi home,baada ya hapo wakanitafutia chuo Cha diploma ya civil engineering mwanza nikapiga miaka 2 by 2014 nikamaliza
Bahati nzuri nikapata kazi ya serikali 2016 baada ya kuunga unga kwa wakandarasi,after two yrs nikaona bachelor tena ya Building Economics Ardhi ndo naendelea nayo hadi sasa,bado napenda Uchumi thus why username yangu ni ChoiceVariable
Nimejifunza kwamba ukiwa chuo achana na hadithi nyingine focus kwa ishu uliyoendea na Jenga tu network na wenzako.
 
Mkuu utakuwa tulisoma pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaa haaa sherehe zilifanyaj mkuu
Mkuu kama unavyojua maisha ya chuo, boom linasoma, home wanatuma pesa za ziada Mungu akupe nini tena...

Nikaanza kukata maji hasa mix mademu, shule kwangu ikawa last option maana nilikuwa nasoma kwa ku beep sana kumbe shule yangu haihitaji kulemba inahitaji kusoma hasa...

Muda wa test ukafika zikawa zinafululiza, matokeo kurudi ni below za 20 na 30, wacha kichwa kipanick hapo kwenda darasa lingine lazima uwe na point 16 na average ya 50 tofouti na hapo una disco...

Ue nikakomaa kibishi ila matokeo kuja kutoka semester 1 na point 7.5 na karai za kutosha hapo nadaiwa almost point 8.5 ili mimi kuwa safe, halafu story zinapamba huko semester two ndio kiboko semester one cha mtoto...

Siku nasikia matokeo yametoka kuna disco 8, na supp za kutosha, machozi yakaanza kunilenga maana nilijua kwenye hao 8 mwanaune nimo, nilikuja kuangalia matokeo usiku wa saa 6 ndani ya shuka, sikuamini aisee semester two nilichomoa but ndio hivyo kwa karai za kutosha mzee baba, yaani kwa ile course ukiingiza kozi 4 umekwenda na maji maana kila somo lina credit hour 2.5....

Sitokaa nisahau ule mwaka aisee....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GPA ya 0.7? kwamba hata first semistar hukuona dalili tu hata u stopishe mwaka ujipange tena?
 
Sikuwah fikiri kwamba naweza disco maana kupata gpa ya 1.8 ili kupiga sapu ilikua simpo ila ndo hivyo ikaja kana ajali afu sikuwa na hili wazo
 
pole mkuu
Mkuu kama unavyojua maisha ya chuo, boom linasoma, home wanatuma pesa za ziada Mungu akupe nini tena...

Nikaanza kukata maji hasa mix mademu, shule kwangu ikawa last option maana nilikuwa nasoma kwa ku beep sana kumbe shule yangu haihitaji kulemba inahitaji kusoma hasa...

Muda wa test ukafika zikawa zinafululiza, matokeo kurudi ni below za 20 na 30, wacha kichwa kipanick hapo kwenda darasa lingine lazima uwe na point 16 na average ya 50 tofouti na hapo una disco...

Ue nikakomaa kibishi ila matokeo kuja kutoka semester 1 na point 7.5 na karai za kutosha hapo nadaiwa almost point 8.5 ili mimi kuwa safe, halafu story zinapamba huko semester two ndio kiboko semester one cha mtoto...

Siku nasikia matokeo yametoka kuna disco 8, na supp za kutosha, machozi yakaanza kunilenga maana nilijua kwenye hao 8 mwanaune nimo, nilikuja kuangalia matokeo usiku wa saa 6 ndani ya shuka, sikuamini aisee semester two nilichomoa but ndio hivyo kwa karai za kutosha mzee baba, yaani kwa ile course ukiingiza kozi 4 umekwenda na maji maana kila somo lina credit hour 2.5....

Sitokaa nisahau ule mwaka aisee....

Sent using Jamii Forums mobile app
.
 
Back
Top Bottom