Tuliomaliza chuo tunalia na ajira mtaani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuliomaliza chuo tunalia na ajira mtaani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MWL MTZ, Oct 4, 2011.

 1. MWL MTZ

  MWL MTZ Member

  #1
  Oct 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <font size="3"><strong>tumemaliza chuo na sasa tupo mtaani lakini tunalia na ajira kila kukicha utatuona na baasha mkononi lakini wapi! mliopo chuoni na mnotalajia kujiunga na vyuo angaline course za kusoma.</strong></font>
   
 2. HOYANGA

  HOYANGA Senior Member

  #2
  Oct 5, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  usikate tamaa utafanikiwa tu bwana mdogo!!!
   
 3. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,078
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  waache wasome sociology halafu waone mziki wake!! watabadilisha bahasha mpaka watakoma!!
   
 4. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  POle Sana. hili ni tatizo la mtizamo wa elimu yetu, kwa kuwaandaa wanafunzi kuajiriwa baada ya kuwaandaa ili wajiajiri wenyewe. Kama mngekua mmeandaliwa kujiajiri wenyewe swala la kusubiri ajira usingesumbuka nalo. Ungekua tayari una Idea yako ya kujiajiri na tatizo lingekua vipi auanze na ungekuja na hiyo idea watu wangekuelekeza jinsi gani ya kupata mtaji kutokana na nini unachotaka kufanya. Kumbuka wahitimu sasa ni wengi na ofisi ni chache za kutoa ajira hivyo badili mtizamo wako katika hilo.
   
 5. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  jamani hili tatizo la ajira wasomi wakitanzania limeanza kuota sugu sana na nafikiri hii ni time bomb ya hii serikali yetu kwa kweli ndio tutaongeza matapeli wezi wa kutumia karatasi mtaani . ni kweli mtaala w a ELIMU YETU UNATUANDAA SISI WASOMI WENGI WA KITANZANIA KUFANYA KAZI ZA KUAJIRIWA(WHITE COLLAR JOBS) KULIKO KAZI ZA KUJIARI BINAFSI ,NI SAWA LAKINI PIA TULITIZAME HILI SUALA KWA KINA SIO KILA MTU ANAWEZA KUJIARI MWENYEWE KWA SABABU NYINGI (mitaji,familia anayotoka, kozi aliyosoma nk). TU KITIZAMA MATAIFA MENGI MWAJIRI MKUBWA NI SERIKALI SASA SERIKALI YETU HAINA MIKAKATI KATIKA KUTENGENEZA AJIRA KWA AJILI YA RAIA WAKE .TATIZO JINGINE AMBALO KWA KWELI HILI NAOMBA VIJANA WENZANGU NA WASOMI WENGI TUJITAHIDI KUWA ELIMISHA WADOGO ZETU UCHAGUZI WA KOZI PINDI WAWAPO SEKONDARI TUNAJUA WENGI WETU TUNATOKA FAMILIA MASKINI WASOMI NI WACHACHE UNAKUTA UNAJIONGOZA MWENYEWE MPAKA UNAFIKA A LEVEL HUJUI UTASOMA NINI CHUO SASA UKIFIKA A LEVEL UNAKUTANA NA HADITHI ZA BCOM, TELECOMUNICATION COMPUTER SCIENCE , IT , BAF ,SOCIOLOGY , LAW (kwamba hizi kozi zina makert) NA WEWE BILA KUPATA USHAURI UNAINGIA KWENYE MKUMBO YAWEZEKANA UFAHAMU HILO SIO KOSA LAKO NI KOSA LA KIMFUMO NAWEZA KUKUPA MFANO MWAKA AMBAO MIMI NILIDAHILIWA CHUO KIKUU KUNA KOZI KAMA TELECOMUNICATION ENGINEERING INAWANAFUNZI 10-15 WAMZUMBE , 10 KIBAHA, 5-10 ILBORU KWELI HAWA WOTE WANAENDA TELECOM KWA KUIFAHAMU AU KWA SABABU INA CUT OFF KUBWA ILI AKAENDELEZE UTABE WAKE HUKO CHUO BILA KUZINGATIA HATIMA YA MAISHA YAKE?
  nina mifano ya kozi kama telecom mwanzoni mwa miaka ya 2000 -2007 mwajiri mkubwa kwa wahandisi hawa walikuwa makampuni ya simu ,sasa makampuni ya simu yameamua kuOUTSOURCE karibia kazi zake nyingi za technical kwa makampuni madogo amabayo hayatumii wahandisi kwa sababu ni gharama kumlipa baadale wanatumia technician
  YAWEZEKANA BCOM, BAF BBA,TELECOM, LAW ZINALIPA ,LAKINI JE UWEZI KUSOMA KOZI KAMA PROCUREMENT, LOGISTIC, ZOOLOGY, MECHANICAL, ELECTRICAL ,CIVIL, URBAN AND RURAL, QUANTITY SURVEY EDUCATION UKATOKA KIMAISHA
  NI KWELI AJIRA NI NGUMU SANA MATATIZO HAYA KWA MTAZAMO WANGU YAPELEKEA SANA HILI TATIZO KUWA SUGU
  I. SERIKALI ISIYO NA MIKAKATI
  II. UCHAGUZI WA KOZI ZA KUSOMA VYUONI
  III. MTAALA WA ELIMU YA KITANZANIA
  MSIKATE TAMAA NDUGU ZANGU TAIFA HILI LINA WASOMI WACHACHE LAKINI WADHARAULIWA SANA JITAHIDI KUJIPANGA AMSHA AKILI JARIBUNI KUWA VENTURE MFANYE WALAU BIASHARA NDOGO TUTOKE TUTAFIKA TU MAANA MANTIKI YA KWANZA YA KWENDA SHULE NI KUKOMBOKA KIFIKRA
  NAWASILISHA
   
 6. Engager

  Engager JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hawa ndo ma-great thinkers sasa, good discription. Nimependa.
   
 7. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naifahamu hiyo challenge ndugu yangu kwani hata mimi nimewahi kukutana nayo wakati fulani, but kwa ufupi hebu nenda na CV yaho pale TAeSA watakusaidia, ila pia usiache kutembelea tovuti za ajira kama vile Tanzania Directory for Business, Entertainment & Travel Info. Usijali you will make it.
   
 8. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  jipe moyo mkuu
   
 9. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Njoo kiwanja 'upige box' babu,uta make dolari kuwashinda wale maprof wako walokuwa wanakubania.Kama vipi niPM nikupe mchongo.Lakini uwe umesoma kozi yenye akili siyo
   
 10. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  mwenzio kasoma political sciance.
   
 11. E

  Ekwilibriamu Member

  #11
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ...tell me about it ! ..nsha tuma maombi mia kidogo bila response hata moja!!
   
 12. E

  Ekwilibriamu Member

  #12
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ...thats Tz bro! wake up!! ...ther no easy way out!
   
 13. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Enhee Ndugu, Hilo Tatizo la Ajira ni kubwa sana Tanzania.

  Nguvu Kazi ya Vijana inapotea bure wakati uchumi wa Tanzania unaporomoka. Just compare our TShs with US $.

  Tatizo ni kuwa hakuna ubunifu katika serikali, Mh Mary Nagu yuko Wizara ya Uwezeshaji ila sijawahi kusikia wakiwa na mkakati wa kuwawezesha Vijana na wawekezaji WAZAWA.

  Kila muda tunataka wawekezaji tu wa nje. Kungekuwa na mkakati maalumu wa kuwapa vijana wetu elimu ya ujasiriliamali (entrepreneurship) ili na kuwawezesha katika nyanja zote kama kilimo (agriculture), usindikaji (agro processing), biashara za kimataifa (Agro export) na zaidi.

  Vijana wangezalisha, ajira zingepatikana, uchumi ungekuwa. Sina la zaidi ila soma hapa zaidi :--- https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/179176-millennium-goals-tanzania-na-shillingi-yetu-kuporomoka.html
   
 14. n

  ngwini JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakenya,waganda,wahindi,wamechukua ajira ze2...
   
 15. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Relief kasema kweli na katoa pendenkezo zuri fuata hilo, kila taaluma inahitajika kwa wingi cha muhimu waliopo makazini wakifikia kustaafu waende nyumbani wapishe wengine, wenye mvi za uzee siyo za kurithi wanaongezeka ofisini, japo sababu kubwa ni kuwa na mafao hafifu wakati wa kustaafu. Ziboreshwe packages za wastaafu ili wasitamani kubaki ofisini wawapishe watoto wao. Ila na wale watafuatao ajira angalieni vyeti vyenu isije ikawa vile vya Kibaha na wengi tunajifelisha wenyewe wakati wa usaili hatujui taaluma ya kusailiwa, poleni Mungu yupo
   
 16. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2011
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu senetor!
  kunakaukweli fulani!
  kunawatu hawatakikushauriwa! unakuta mtu unamshauri anakoma mi soshologi tu!
   
 17. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu. Wengine tumepitia hiyo balaa ya kuzunguka hapo mjini na bahasha sijui folders imejaa resumes, ajira hakuna, kujiajiri mwenyewe mtaji sina, kiatu soli ikaisha nikatembelea kandambili, nauli ya daladala ikawa sina, pa kukaa sina na njaa ndio usiseme. Karibu uje kupiga box kaka. Box halimtupi mtu
   
 18. Mhandisi Mzalendo

  Mhandisi Mzalendo JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2011
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 2,209
  Likes Received: 1,096
  Trophy Points: 280
  kaka umemaliza telecom mwaka gani pale udsm??? me nshawashauri madogo mpaka natamani kulia but hawaelewi wakishapata marks kubwa wanataka wasome TE.....ajira huku ngumu ingawa si kivile problem nw ni mshahara zaidi....my advice if upo telecom tayari jitahid kubase kwenye IT kidogo piga programming PHP, MySQL, javA web designing, na mengine mengi...kazi za site c lelemama
   
 19. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  mimi nimemaliza electrical pale mkuu ila naona my collegue wanavyosafa kitaa na hiyo course bad enough ni watu walliokuwa na uwezo mzuri darasani , usichoke kuwaelimisha madogo maana mbele ya safari watakuja kujua ukweli ni upi . unajua civil engineering, electrical engineering na mechanical na chemical engineering ni principle course kwa engineering tofauti na hizi course nyingine ambazo either zinaaanzisha kutokana na soko au mabadiliko ya kiteknolojia sasa ukiangalia nchi yetu iko static sana kwenye mabadiliko sasa wewe unaweza ukawa unatumia mtaala wa kizamani wakati dunia imeshaakuacha mfano wewe unakazana kusoma analogue telecom wakati watu wanazungumzia digital telecom au unasoma pascal programming kweli?
  kwa ujumla tujitahidi sana kubadilika kuna fursa nyingi hapa duniani tujitahidi kutumia akili zetu at maximum ..
  nawasilisha
   
 20. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana kijana usikate tamaa kazi ngumu kupata: inaelekea elimu uliyopata ilikuwa inakuandaa kuwa job hunter ok keep on hunting but this could be your prime time to think on what you can do kujiajiri: ni ngumu bila mtaji lakini ukiwa mbunifu unaweza kusahau about job hunting ukawa unafikiri jinsi ya kuboresha kile unachokisimamia
   
Loading...