Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,013
- 1,635
Habar wana jamvi ,leo naomba tutoe ushuhuda kwa wale ambao tumelewa na watu ambao sio wazazi wetu mfano Baba mdogo, Mama mdogo, Shangazi, mjomba, mama wa kambo nk ila wakatundea mema
Mimi baada ya mama yangu wa kambo kunitendea yasiyo mema ila siwezi kuýataja hapa, baada ya mama yangu mzazi kufariki nikiwa mdogo, Mke wa baba yangu mdogo alimshawishi mumewe yaani baba yangu mdogo wanichukue niishi nao, baba yangu mdogo akanichukua kutoka kwa baba yangu mzazi nikawa naishi nao, Yule mama Mungu ambariki sana, alinilea kwa upendo mpaka watu wageni na mimi walijua yule ndio mama yangu Mzazi na yule baba mdogo ndio baba yangu mzazi, ingawa Mapungufu ya kibinadamu yalikuwepo kwani huwezi kupata haki sawa na watoto aliowazaa yeye, ila mimi mapungufu yale niliyaona ni mambo yakawaida, hata kwa watoto wako mwenyewe lazima tofauti ya upendo iwepo,
Mpaka nakumbuka kuna kipindi nilipata changamoto za kimaisha, nilikua napokea simu kutòka kwa yule mama, "Baba nimekutumia kiasi kidogo wanunulie sukari wajukuu zangu, "ukija ukipeleleza unagundua kwamba aliuza sehemu ya mavuno ndio akakutumia hiyo hela, baada ya muda utasikia simu yake "Baba nenda stendi na usubiri basi fulani kuna mzigo nimekutumia "ukienda pokea unakuta vyakula vya kutosha.
Kwa sasa yule mama namchukulia ndio mama yangu mzazi kwani mama yangu alifariki nikiwa mdogo, shida yake najitahidi nianze kuitatua mimi kabla ya watoto wake.
Naomba Mungu anipe Riziki zaidi na atupe maisha marefu ili aenjoy upendo wangu