Tuliokuwa tukipenda Kuangalia ' Sinema ' za Hayati Bruce Lee na kwenda ' Kuonea ' Watu mitaani na tukapigwa tujitokeze

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,922
Ikiwa leo ni Kumbukumbu ya ' Mtaalam ' wa Sanaa za ' Mapigano ' duniani ( Martial Arts ) Hayati Bruce Lee naomba wale wenzangu na Mie ambao tulikuwa tukipenda mno Kuziangalia, Kuiga na kwenda Kuwaonea Wenzetu mitaani na tukawa tunapata ' mirejesho ' ya Kupigwa / Vipigo tujitokeze ili ikibidi tuweze Kujiona jinsi tulivyokuwa Mangumbaru na Mapopoma kipindi hicho.

Binafsi nakumbuka nilikuwa nikipenda sana Kuziangalia na kwenda Kuwaonea ' Madogo ' wenzangu ' Mitaani ' na hata Watu wazima ( akina Kaka )ambao nilikuwa naona nawamudu na hasa kwa ' Mikwara ' yangu iliyotukuka ila kuna Siku moja ' niliyakanyaga ' na mpaka leo sisahau kwa nilichokipata.

Nakumbuka kuna Siku moja nikiwa mitaa fulani kwa Mkubwa mmoja ambaye Kipindi hicho alikuwa akilindwa na Wana Medani Waliotukuka ( Wanajeshi / Wajeda ) hivyo kwa Kujiamini na Sinema za Bruce Lee ambazo nilikuwa naziangalia mara kwa mara na ' Kumuiga ' katika tembea tembea yangu tena nikiwa na Mbwa wangu nikamkuta huyo Mjeda anakojoa pembeni hivi mwa barabara nikaanza kumpiga ' Mkwara ' kama kawaida yangu huku nikilia kama Bruce Lee na ile Sauti yake, mara nikiipindisha Mikono yangu na Miguu utadhani Helikopta ya Polisi inataka Kupaa yaani yote ni ' Minjonjo ' tu ili Jamaa aogope na nijione mbabe nilikuja kupokea Ngumi moja hiyo ' takatifu ' na ' tukuka ' ambayo sidhani hata akina Tyson au Cheka wanaijua inaitwaje ambayo iliniingia kisawasawa na kilichofuata hapo nilikubaliana na yule Mbwa wangu niliyekuwa nae kuwa tugawane zetu tu njia za kurudi Nyumbani japo Yeye ( yule Mbwa ) wakati ' nakandamizwa ' na lile ' Konde ' zito la Kimedani / Kijeshi alikuwa tayari ameshaianza safari yake ya Kunitangulia kurudi Nyumbani.

Ile ngumi hadi leo naikumbuka na kila nikikutana na hawa Mabondia nikiwaelezea na kuwauliza inaitwaje jibu wanalonipa tu ni kwamba ina ' Ngumi ya Kifo ' na kwamba kama ningechelewa au kuzidi kuwepo eneo lile la tukio na yule Mjeda basi kulikuwa na uwezekano mkubwa ile Siku maturubai ya Msiba yangetawala Nyumbani Kwetu.

Ndiyo maana hadi leo hii nikikuta tu Ugomvi wowote ( kwakuwa napenda sana Ugomvi ) ila nikaambiwa anayeuratibu / anayeusimamia ni Mwana Medani / Mwanajeshi Mimi huwa mpole mara moja na ikibidi huwa naanza kuziulizia mapema mno njia za Uchochoro ili ' Kikinuka ' tu basi tuanze kumwambia Mwanariadha Usain Bolt kuwa hata huku Tanzania Vipaji vya Kutoka Nduki ( Kukimbia ) mita 100 vipo lukuki tu sema bado hatujaonekana.

Hivi Wajeda / Wanajeshi zile ngumi zao nani huwa anawafundisha? Na kwanini hata akikupiga huwa zinauma hata kwa miaka 15 hadi 25 ya maisha yako yote? Haya Vijana wa sasa hivi mnaopenda sijui Kuwaangalia akina Vad Damme na Jackie Chan ole Wenu siku mkosee mkajaribu ' Kuziigiza ' kwa Wajeda ndipo mtajua kwanini hata Mimi GENTAMYCINE nawaogopa japo wengi wao ni Marafiki zangu wakubwa na wazuri tu huku hadi Ndugu zangu baadhi nao wakiwa huko ila ' nawaheshimu ' kuliko Kitu kingine chochote kile.

R.I.P Bruce Lee

Nawasilisha.
 
Dah umenikumbusha mkuu, niliwahi kufunga mtaa baada ya kupata mkanda mweupe katika karate, nikajiona mimi ndio Bruce Lee. Si nikaingia anga za vichaa ambao wao mazoezi kwao ilikuwa ni kama menu ya kila siku. Acha nichezee kichapo, nakumbuka nilikuja kuzinduka siku ya pili nikiwa hospitali...
 
Mkuu ' Shikamoo ' sana. Yaani umenifanya nicheke mno kwa hii ' post ' yako. Kumbe tuliojeruhiwa na ' Kumuigiza ' Hayati Bruce Lee tupo wengi hivi Mkuu? Ngoja waje wengine na leo naamini kadri ' Uzi ' unavyoenda tutapata ' Shuhuda ' nyingi za kuvunja mbavu kutoka kwa wale Wenzetu ambao tulikuwa tukidanganywa na ' Sinema ' zake huyo Nguli ( Legend ) wa Kimapigano.
 
Miaka ya 99 tumetoka kuangalia ile movie ya Bluce Lee na Chuck Norris tukasema ngoja tupigane ikawekwa Sh 30 chini atakayekuwa mshindi anabeba.
Mimi nikajifanya ndio Bluce Lee halafu mwenzangu Chuck Norris nilipigwa siku hiyo mpaka "liwange" puani zinatoka.

Tangu siku hiyo sijawahi kupigana katika maisha yangu.

Ile zile movie tulikuwa tunaona ndio ukweli halisi.(kipindi cha kusimuliana sasa)
 
Hizi Sinema tulikuwa tunakwenda kuangalia kwa "mwasi" pale kinondoni studio alikuwa kati ya watu wa kwanza kuwa na Tv....
Tv enzi hzo hizo lazima iwe na kadi kama ya gari

Ova
 
Naamini kilichompata hawezi hata kusimulia...

Kweli kabisa Mkuu na ndiyo maana ameogopa hata ' Kutusimulia ' ili tujue. Tena nahisi atakua alipokea ' Kichapo ' cha Kishalubela / Kikatili kuliko ambavyo tulivipata Mimi na Wewe.
 
Miaka ya 99 tumetoka kuangalia ile movie ya Bluce Lee na Chuck Norris tukasema ngoja tupigane ikawekwa Sh 30 chini atakayekuwa mshindi anabeba.
Mimi nikajifanya ndio Bluce Lee halafu mwenzangu Chuck Norris nilipigwa siku hiyo mpaka "liwange" puani zinatoka.

Tangu siku hiyo sijawahi kupigana katika maisha yangu.

Ile zile movie tulikuwa tunaona ndio ukweli halisi.(kipindi cha kusimuliana sasa)

Nilisema leo katika ' Uzi ' huu nitacheka mno na kukutana na ' Vituko ' vya kila aina.
 
Miaka ya 99 tumetoka kuangalia ile movie ya Bluce Lee na Chuck Norris tukasema ngoja tupigane ikawekwa Sh 30 chini atakayekuwa mshindi anabeba.
Mimi nikajifanya ndio Bluce Lee halafu mwenzangu Chuck Norris nilipigwa siku hiyo mpaka "liwange" puani zinatoka.

Tangu siku hiyo sijawahi kupigana katika maisha yangu.

Ile zile movie tulikuwa tunaona ndio ukweli halisi.(kipindi cha kusimuliana sasa)
Dah! Nimecheka utadhani ni jambo la kufurahisha...
 
Hizi Sinema tulikuwa tunakwenda kuangalia kwa "mwasi" pale kinondoni studio alikuwa kati ya watu wa kwanza kuwa na Tv....
Tv enzi hzo hizo lazima iwe na kadi kama ya gari

Ova
Mrangi mbona umeficha? Funguka ilikuwaje baada ya kuangalia movie ya Bruce Lee...
 
Nilicheza na kupenda zaidi Kung fu kuliko Karate. Ninachokumbuka ni kwamba sijawahi kumuangusha Bruce Lee, ila sikuwa mkorofi ingawa nilionekana mpenda ugomvi sababu ya zero tolerance kwenye matusi na matani.
 
Magereza butimba nilikuwa nachapa sana ngumi yani nikikuchapa moja lazima utoke nundu (TOCHI) mpaka sasa asili yangu haijapotea. Japo kuna migambo maeneo ya tanganyika stand walinifanyaga sio na kiburi cha baba ni m-soldier kikaanza kuisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom