Tuliokuamini na kukutetea kwenye janga la Corona umetuangusha. Nimepoteza rafiki na ndugu kwa janga la Corona. Serikali chukueni hatua

Umeacha hoja za msingi za namna ya kujikinga na kuelimishana
Wewe umewaza lockdown tu na hiyo categorization yako
Duh...!, kumbe siku hizi humu jf kuna muongozo wa namna ya kuchangia?!, mtu akipandisha bandiko lina hoja kumi lazima uzijibu hoja zote 10?. Uki zero in kwenye eneo fulani unaulizwa kwanini hukuchangia kuhusu hili na lile?.

Bandiko lilikuwa na hoja nyingi mimi nika zero in eneo ninaloweza kuchangia, sasa kumbe nilitakiwa kuchangia kuhusu
  1. biashara kariakoo kwa kuijengea sepcials zones
  2. wilaya zote na kuwa na utaratibu maalum wa nyakayi za biashara na kupunguza sababu za kila mtu kwenda kariakoo
  3. Mass testing
  4. Case identification kupitia local authorities
  5. na namna ya kusaidiana kupitia watendaji
Asante nikitulia nitachangia tena uzi huu.
P
 
Paskal usitake nikudharau bana.
Na masikin hata awe amechoka vip mzee akiumwa lazima watu wajifunge atibiwe.
Duh...Mkuu Kitali, kama ni kunidharau kwa ku zero in nidharau tuu, ila pia asante kwa nondo kali za kushiba kwenye bandiko lako.

Corona ina kinga kwa kuizuia isikuingie ila ikikuingia haina dawa!. Pona yako ni uwezo wa kinga yako ya mwili kuproduce antigens to fight the virus, lakini kama una issues za PB, Kisukari, Aids, Heart Disease, Pneumonia, TB, au uko kwenye ugonjwa mwingiine wowote ambao uko under heavy medication kiasi cha kumaliza uwezo wa mwili wako kutengeneza antigens, hata watu wajifunge vipi kukutibia, hata ufungiwe the latest ventilators, lazima uchomoke!.
P
 
Kinachouma kwa nini hata halizungumzii.
Hii ni dalili ya dharau na majigambo kwa upande wake
 
Paskal Mayalla Mkuu ni umri ndio unaenda au basi tu.Mbona wakati mwingine unakuwa na reasoning ndogo kiasi hiki? Kenya walilifanya hilo nadhani hata Uganda. Na hili lilisemwa tangu mwanzo ukawa unaleta nyuzi zako za kutetea na na kishabiki.
Mkuu Focal ni umri, tena na Corona hii ni kutuombea tuu Mungu sisi wazee vinginevyo mtatupoteza wengi!.
P
 
Paskal usitake nikudharau bana.
Ishu niko hiv. Linapotokea jambo la dharura ni lazima njia za kidharura litumike kupambana nalo. Hii nchi ina mfuko wa dharura wa maafa.
Pili. coz hili ni janga la kimataifa zinahtajika uwaz hili usaidiwe kimataifa.
Tatu. Hakuna mtu ambae hajui tuko kwenye dharura so ukilockdown kwa mfano Dar zanzibar mwanza na Arusha. Unadeal na zile familia za wasiojiweza tu. Hawa watu wa mishahara cjui kipato cha juu wanapambana na hali zao. Mbona uganda wamefanye mzee na wamefanikiwa? Shida mimi ninayoiona ni kuwa kibur cha mamlaka ndio kinatusumbua. Tushaongea sana mambo mengi ambayo mwisho wa cku tumeshindwa kurud nyuma. Mara ooh cc ni nchi tajir ni dono country mara mabeberu mara cjui nini. Na ukiangalia vizur ni kama vile wazir mkuu na serikali yake hawakaubalian na Rais ni hawana jins tu ya kufanya. Sasa walituambia tuombe cku 3. Hapo hapo tutumie miti shamba halafu hapo hapo wanapika data za uongo. Hiv mnajua Mungu hadhihakiw. Ukipandacho ndicho utakachovuna. Mi naona kama mh ameamua kuidhalilisha hii nchi tu. Kwamba ionekane hii nchi inaamin miujiza katika kutatua jambo mambo ya zama za kinjikitile ngwale. Hiv kweli Rais hajui yeye ndio baba yetu. Kwa hili ameonyesha kushindwa kabisa uongoz aisee kuwa mkweli tu. Na by the way hiv unajua usichukua hatua ukiwa na muda ukaendelea kusubir muda uje ukuamulie tutakuwa tumekwisha?. Na masikin hata awe amechoka vip mzee akiumwa lazima watu wajifunge atibiwe. Hii nchi yetu sote tumezaliwa huko machakan kula mara moja kwa siku tunashindwa vip kuvumilia huo mwez mmoja wa lockdown?
twende taratibu.maana wabongo kwa maneno hamjambo.

funga dsm,funga mwanza,funga arusha.upate watu milioni 15,toa watu milioni 3 wanaojiweza,wabaki milioni 12 wanaohitaji msaada.

bila kusahau factor no moja,kwamba uzalisha hamna baada shughuli za uzalishaji kufungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh...!, kumbe siku hizi humu jf kuna muongozo wa namna ya kuchangia?!, mtu akipandisha bandiko lina hoja kumi lazima uzijibu hoja zote 10?. Uki zero in kwenye eneo fulani unaulizwa kwanini hukuchangia kuhusu hili na lile?.

Bandiko lilikuwa na hoja nyingi mimi nika zero in eneo ninaloweza kuchangia, sasa kumbe nilitakiwa kuchangia kuhusu
  1. biashara kariakoo kwa kuijengea sepcials zones
  2. wilaya zote na kuwa na utaratibu maalum wa nyakayi za biashara na kupunguza sababu za kila mtu kwenda kariakoo
  3. Mass testing
  4. Case identification kupitia local authorities
  5. na namna ya kusaidiana kupitia watendaji
Asante nikitulia nitachangia tena uzi huu.
P
Hahahahaaaa

Naona all in arms

Your standards preceded you

I expected more... Lakini naona you are caught between a rock and a hard surface

Haya mzee baba nasubiri uchangie

Unitag please
 
Mkuu Barafu, kwanza pole sana kwa kufiwa na rafiki rubani wa Tanapa. Pia kwa incident ya kifo cha Mzee wa jirani aliyekosa huduma hadi kupoteza maisha na familia yake kuingizwa karantini.

Tangu kuingia kwa janga la Corona, elimu ya kinga imeenezwa sana, ila kwa upande wa msimamo na kauli za rais wetu, kuna watu hawajamwelewa ukiwemo wewe.

Watanzania tuko wa aina tatu
1. Kundi la kipato cha juu na watumishi wa umma, matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili ndilo kundi pekee ambalo wanaweza kuishi kwenye lockdown. Hawa wako wachache nchi ikiamua kufanya lockdown, wataendelea kulipwa even by doing nothing, na wataninua mahitaji yao yote na kujifungia ndani. Hawa ni watu wenye magari yao na wanaweza kununua mahitaji yote supermarkets. Kwenye kundi hili, they've made money and now, they use money work for them.
Yaani wanapesa ambapo wanaweza kukaa na kuitumia pesa kuwafanyia kazi. Kati ya watu milioni 50 ya Watanzania, kundi hili lina watu 10% ambao ni watu milioni 5.

2. Kundi la pili ni watu wa kipato cha kati, the working class, hawa ni wafanyakazi waajiriwa, wazalishaji mali na wafabiashara wa kati. Hawa wanafanya kazi, wanatoka jasho ndipo wapate pesa. Ikitokea lockdown hawa uzalishaji utasimama, biashara zitasimama, uchumi utatikisika na the working class watapoteza kazi, hivyo hawawezi ku survive kwenye lockdown. Hawa they work for money to live, yaani wanafanya kazi na kuvuja jasho kutafuta pesa ili waitumie hiyo pesa kuishi na kuendesha maisha yao. Ikitokea lockdown hawawezi kufanya kazi na hawawezi kupata pesa hivyo hawawezi kuishi. Kundi hili lina 20% ya Watanzania ambao ni watu milioni 10.

3. Kundi la mwisho ni kundi la watu wenye kipato cha chini, hawa they live hand to mouth, kundi hili ni kundi la wakulima, wafugaji, wavuvi na wafabiashara wadogo ambao ili waishi lazima wawahudumie, makundi yale mawili, kukitokea lockdown, kundi hili ndio most hit, watakufa njaa inabidi wagawiwe chakula, kundi hili lina 70% ya watu milioni 50, ambao ni watu milioni 35. Hawa they don't make any money, they only struggle to survive.

Uamuzi wa rais Magufuli wa no lockdown una lengo la kuzuia kuporomoka kwa uchumi wetu sio ili to make money but kuzuia watu wetu wasife njaa, kama ni kufa kwa kakolona heri wachache wafe kwa Corona, kuliko kufanya lockdown na kuua wengi kwa njaa.

P
Pascal Mayalla hoja zako zina mashiko ila takwimu zina upotoshaji mkubwa.
Kundi la kwanza ina maana unajumuisha "mabilionea wa Kitanzania" na viongozi wa juu wa makampuni, taasis, serikali na mashirika ya umma ambo umekisia ni 5,000,000. Idadi hii ni kubwa sana; tunazungumzia bilionea hata faida yake anayopata ni mabilioni hivyo kodi anazolipa serikalini ni mabilioni, sasa kama kwenye hiyo takwimu 4,000,000 watakuwa ni wafanyabiashara na wakalipoa kodi isiyopungua TZS 1,000,000,000 kwa mwaka kila mmoja, ninapata hesabu ambayo haisomi kwenye calculator yangu. Hivyo kundi la kwanza Tanzania haina idadi hiyo ya watu 5,000,000 wa kipato cha juu.

Kundi la pili umeweka watu wa kipato cha kati kuwa ni 10,000,000. Tuchukulie tuu hao ni watu wa kipato cha TZS 2,000,000 kwa mwezi hivyo kodi yao ni TZS 600,000 sawa na TZS 7,200,000; ukichukua hiyo idadi ya waty ukizidisha na TZS 7,200,000 napata jibu ambalo kwenye mashine yangu haliingii. Hivyo Tanzania haina watu wa kipato cha kati wanaofikia idadi hiyo ya 10,000,000

Kundi la tatu natumaini unajumuisha huko watoto, wanafunzi na wazee, kwa mtazamo wangu ni zaidi ya idadi uliyotoa mfano mimi nafanya kazi nyuma yangu nina mke, watoto watano wangu, watoto wawili wa marehemu kaka zangu, mtoto wa marehemu dada yangu sawa na 1: 9 yaani wasio na kipato ni 9/10 X 100 = 90% kwa mujibu wa familia yangu.

Pitia upya takwimu zako, kundi la kwanza na la pili lingekuwa na idadi hiyo ya watu, wale wasio na ajira wangekuwa walipwa na serikali kutokana na makusanyo makubwa ya kodi.
 
Mkuu Barafu, kwanza pole sana kwa kufiwa na rafiki rubani wa Tanapa. Pia kwa incident ya kifo cha Mzee wa jirani aliyekosa huduma hadi kupoteza maisha na familia yake kuingizwa karantini.

Tangu kuingia kwa janga la Corona, elimu ya kinga imeenezwa sana, ila kwa upande wa msimamo na kauli za rais wetu, kuna watu hawajamwelewa ukiwemo wewe.

Watanzania tuko wa aina tatu
1. Kundi la kipato cha juu na watumishi wa umma, matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili ndilo kundi pekee ambalo wanaweza kuishi kwenye lockdown. Hawa wako wachache nchi ikiamua kufanya lockdown, wataendelea kulipwa even by doing nothing, na wataninua mahitaji yao yote na kujifungia ndani. Hawa ni watu wenye magari yao na wanaweza kununua mahitaji yote supermarkets. Kwenye kundi hili, they've made money and now, they use money work for them.
Yaani wanapesa ambapo wanaweza kukaa na kuitumia pesa kuwafanyia kazi. Kati ya watu milioni 50 ya Watanzania, kundi hili lina watu 10% ambao ni watu milioni 5.

2. Kundi la pili ni watu wa kipato cha kati, the working class, hawa ni wafanyakazi waajiriwa, wazalishaji mali na wafabiashara wa kati. Hawa wanafanya kazi, wanatoka jasho ndipo wapate pesa. Ikitokea lockdown hawa uzalishaji utasimama, biashara zitasimama, uchumi utatikisika na the working class watapoteza kazi, hivyo hawawezi ku survive kwenye lockdown. Hawa they work for money to live, yaani wanafanya kazi na kuvuja jasho kutafuta pesa ili waitumie hiyo pesa kuishi na kuendesha maisha yao. Ikitokea lockdown hawawezi kufanya kazi na hawawezi kupata pesa hivyo hawawezi kuishi. Kundi hili lina 20% ya Watanzania ambao ni watu milioni 10.

3. Kundi la mwisho ni kundi la watu wenye kipato cha chini, hawa they live hand to mouth, kundi hili ni kundi la wakulima, wafugaji, wavuvi na wafabiashara wadogo ambao ili waishi lazima wawahudumie, makundi yale mawili, kukitokea lockdown, kundi hili ndio most hit, watakufa njaa inabidi wagawiwe chakula, kundi hili lina 70% ya watu milioni 50, ambao ni watu milioni 35. Hawa they don't make any money, they only struggle to survive.

Uamuzi wa rais Magufuli wa no lockdown una lengo la kuzuia kuporomoka kwa uchumi wetu sio ili to make money but kuzuia watu wetu wasife njaa, kama ni kufa kwa kakolona heri wachache wafe kwa Corona, kuliko kufanya lockdown na kuua wengi kwa njaa.

P
Kaka Pascal, nina hakika wewe ndio hujamuelewa mkuu Barafu; hajasema kwamba Dar iwe lock down na wakazi wake wafungiwe, pendekezo lake (ambalo ndio wengi wameshauri sana) ni kwamba ban only public transports, basi na Ndege za kuingia na kutoka Dar vipigwe stop, ruhusu only magari ya mizigo ambayo itakua inatoa mizigo Dar na kwenda huko kwingine including nje ya nchi na pia yalete vyakula na bidhaa nyingine Dar including vile vya kwenda nje ya nchi through bandari yetu but wakazi wa Dar wasisafiri kwenda nje ya Dar ambako inavyo onekana wanapeleka huo ugonjwa mikoani; hivi hilo lina shida gani? Mkuu Barafu ndicho alicho maanisha
 
Kaka Pascal, nina hakika wewe ndio hujamuelewa mkuu Barafu; hajasema kwamba Dar iwe lock down na wakazi wake wafungiwe, pendekezo lake (ambalo ndio wengi wameshauri sana) ni kwamba ban only pablic transports, basi na Ndege za kuingia na kutoka Dar vipigwe stop, ruhusu only magari ya mizigo ambayo itakua inatoa mizigo Dar na kwenda huko kwingine including nje ya nchi na pia yalete vyakula na bidhaa nyingine Dar including vile vya kwenda nje ya nchi through bandari yetu but wakazi wa Dar wasisafiri kwenda nje ya Dar ambako inavyo onekana wanapeleka huo ugonjwa mikoani; hivi hilo lina shida gani? Mkuu Barafu ndicho alicho maanisha

Unafikiri hawajui basi, bali wanafanya exaggeration makusudi ili kutake vitu out of context kwa malengo yao ya kuficha incompentence yao
 
Unafikiri hawajui basi, bali wanafanya exaggeration makusudi ili kutake vitu out of context kwa malengo yao ya kuficha incompentence yao
Kibaya Zaidi tunafanyia mzaha kwenye ugonjwa; mambo haya yamezungumzwa sana Bungeni, Lema aliongea kwa uchungu sana hadi aka predict kwamba in 3 weeks time mambo yatakua hadharani bungeni na wao wataanza kukimbiana, yale mavichwa maji ya bungeni kama kawaida yao yakazomea na kukejeri, leo wameanza kuogopana. Sijui hua kuna uhusiano gani wa UJINGA na ccm, sijui kwa kweli.
 
Mkuu Barafu, kwanza pole sana kwa kufiwa na rafiki rubani wa Tanapa. Pia kwa incident ya kifo cha Mzee wa jirani aliyekosa huduma hadi kupoteza maisha na familia yake kuingizwa karantini.

Tangu kuingia kwa janga la Corona, elimu ya kinga imeenezwa sana, ila kwa upande wa msimamo na kauli za rais wetu, kuna watu hawajamwelewa ukiwemo wewe.

Watanzania tuko wa aina tatu
1. Kundi la kipato cha juu na watumishi wa umma, matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili ndilo kundi pekee ambalo wanaweza kuishi kwenye lockdown. Hawa wako wachache nchi ikiamua kufanya lockdown, wataendelea kulipwa even by doing nothing, na wataninua mahitaji yao yote na kujifungia ndani. Hawa ni watu wenye magari yao na wanaweza kununua mahitaji yote supermarkets. Kwenye kundi hili, they've made money and now, they use money work for them.
Yaani wanapesa ambapo wanaweza kukaa na kuitumia pesa kuwafanyia kazi. Kati ya watu milioni 50 ya Watanzania, kundi hili lina watu 10% ambao ni watu milioni 5.

2. Kundi la pili ni watu wa kipato cha kati, the working class, hawa ni wafanyakazi waajiriwa, wazalishaji mali na wafabiashara wa kati. Hawa wanafanya kazi, wanatoka jasho ndipo wapate pesa. Ikitokea lockdown hawa uzalishaji utasimama, biashara zitasimama, uchumi utatikisika na the working class watapoteza kazi, hivyo hawawezi ku survive kwenye lockdown. Hawa they work for money to live, yaani wanafanya kazi na kuvuja jasho kutafuta pesa ili waitumie hiyo pesa kuishi na kuendesha maisha yao. Ikitokea lockdown hawawezi kufanya kazi na hawawezi kupata pesa hivyo hawawezi kuishi. Kundi hili lina 20% ya Watanzania ambao ni watu milioni 10.

3. Kundi la mwisho ni kundi la watu wenye kipato cha chini, hawa they live hand to mouth, kundi hili ni kundi la wakulima, wafugaji, wavuvi na wafabiashara wadogo ambao ili waishi lazima wawahudumie, makundi yale mawili, kukitokea lockdown, kundi hili ndio most hit, watakufa njaa inabidi wagawiwe chakula, kundi hili lina 70% ya watu milioni 50, ambao ni watu milioni 35. Hawa they don't make any money, they only struggle to survive.

Uamuzi wa rais Magufuli wa no lockdown una lengo la kuzuia kuporomoka kwa uchumi wetu sio ili to make money but kuzuia watu wetu wasife njaa, kama ni kufa kwa kakolona heri wachache wafe kwa Corona, kuliko kufanya lockdown na kuua wengi kwa njaa.

P

Wewe acha kutetea muuaji eti tuangalie uchumi kwanza huku mamilioni wakifa wewe unatokea wapi? Ni wale mliotumwa kumtetea mwenzenu kwa hali na mali? Africa kusini, Botswana, Namibia, Nigeria, Egypty, Kenya, ,etc wamefanya lockdown unafikiri hawa hawajui uchumi? Tulikosea mno kuchagua mtu kama huyu.
 
Nchi hii njaa imekuwepo mara nyingi. Na rais alishaonesha hajali habari ya njaa. Alishasema wilaya itakayokuwa na njaa watajua wenyewe.
Mbaya zaidi tumeuza chakula kutoka kwenye ghala na kila mwaka Zito alikuwa anaonesha akiba inavyopungua.
Leo wakisema haitakiwi lockdown kwa sababu kutakuwa na njaa ndiyo wakati mzuri wa kuwauliza tangu lini wanajali njaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni dhahiri kuwa kwa sasa Rais John Pombe Magufuli anajionyesha kuwa katika uongozi wake,suala la majanga na uhai wa wananchi wake hayana vipaumbele.Kwake ni pesa na kuona uchumi unakuwa.Rais wetu tofauti na matarajio yetu,amelinganisha uhai na thamani ya pumzi ya watu wake na uchumi wa nchi,kwake Uchumi kwanza uhai baadae.

Huyu sio Rais ambaye kwa sasa unaweza kutoka mbele ya wafiwa na wahanga wa corona na kuwaeleza kuwa ni Rais wa wanyonge, hata mara maja, abadani haitawezekana kwa sasa. Ni kama mkubwa wetu huyu kayaweka maisha ya watu wake rehani na kuutazama kwanza uchumi na pesa.

Kuna malalamiko mengi juu ya ubovu wa huduma za afya katika sehemu walizotengewa wagonjwa wa COVID-19,anatumia mpaka magazeti ya serikali kueneza propaganda kuwa vifaa tiba vimejaa kila mahali, ukweli ni kuwa, huko Mnazi Mmoja, Amana na Mwananyamala wahudumu wa afya ni kweli wanawakimbia wagonjwa sababu na wao wanaokoa maisha yao kwa kukosa PPE.

Watu wanakufa,watu wanaambukizana na kwa kweli wengine wanaangamia kwa sababu ya kauli za Rais na matendo yake.Hali ni mbaya ndugu zangu,tusisikilize propaganda.

Sasa bila shaka kila mtaa umeanza kukumbwa na vifo vya Corona,juma la jana,familia ya rafiki yangu waliuguliwa na mzee wao kwa ugonjwa wa Corona,wakatoka nyumbani kwenda hospitali ya jirani ya Palestina,huko wakawaambia waende Amana,kufika hapo wakaambiwa wanatakiwa kwenda Buguruni kwa Mnyamani ndio kuna kituo kinashughilikia,kufika Buguruni wakaambiwa waende Mloganzila maana ndio watapata haduma.

Safari yote hiyo mgonjwa hana huduma yoyote,walipofika Mloganzila wakaambiwa hawana huduma yoyote,katikati ya bumbuwazi mgonjwa akafariki bila matibabu,na baadae serikali kuuchukua mwili na kuuzika kwa madai kuwa wamechukua sampuli za maiti na kuona maambukizi,familia nzima sasa ipo karantini.

Ummy Mwalimu na Serikali,iseme sasa,na iseme tena,kwanini kila mahali wagonjwa wanakataliwa??Wagonjwa wetu tupeleke wapi?

Habari mbaya kwangu,na ngumu sana,ni kumpoteza rafiki yangu wa muda mrefu,mwanafunzi wangu na comrade wangu mcheshi,huyu alikuwa rubani wa ndege za TANAPA ambaye amepoteza maisha kwa janga la corona na hayupo hata katika kundi la watu waliotangazwa kuwa wamekufa na ugonjwa huu.Huyu ameondoka na watu kadhaa nyuma yake ambao walimbukizana.Na hao watu wameambukiza wengine...Hali ni mbaya na bado serikali inashindwa kutoa sauti ya kimamlaka kuonyesha kuwa hali ni mbaya.

Marehemu huyu(nahifadhi jina lake) siku kadhaa nyuma tuliwasiliana akienda kuhuisha mambo yake ya leseni za urubani na vibali kadhaa pale mamlaka ya Usafiri wa Anga,na baadae kuwa na training nje ya jiji la Dsm wakiwa na mwenzake na watumishi kadhaa wa mamlaka,maanake alikutana na watumishi hapo mahali,hao watumishi wana familia zao,na hao sehemu ya familia wana jamaa zao wengine makazini na mitaani.

Naambiwa sehemu ya ofisi za Mamlaka hizo watumishi wapo karantini sababu waligusana au kuchangamana na marehemu rafiki mpendwa na mwenzake.

Kwa hali hii,bado serikali imejaa vitisho,haizuii misongamano,haiuzuiii mjii wa Dsm kusongamana katika bars,kumbi za starehe na mikusanyiko mingi.Mji upo wazi kusambaza magonjwa mikoani kwa jina la "Kukuza Uchumi".Huu ni unyama gani?Tunawaza pesa juu ya uhai?

Mgonjwa mmoja wapo kule Rukwa,alitokea Dsm kwa njia ya ndege ya ATCL,akapanda ndege mpaka Mpanda na akasogea mpaka Sumbawanga,hapo kaacha ugonjwa kuanzia kwenye ndege,Mpanda hadi Sumbawanga,maanake alichangamana na abiria wengine,alioambukiza ndio wenye dalili na walio hoi,maanake tamaa za uchumi na pesa,zinafanya tunarusha ndege toka Dsm kwenda Mpanda ili ipeleke ugonjwa ukasambae vijijini kwa masikini na wanyonge.Hao Emirates na wengine walifunga safari sio kwamba hawajui pesa,wanajali uhai wa watu wao.

Hizi ni dalili mbaya za kiuongozi,huu ni uuwaji usiokuwa wa moja kwa moja au ni tuseme wa moja kwa moja.Ni ukosefu wa utu na upendo kwa watu ulioapa kuwalinda ukiwa na katiba kuume na kitabu cha dini kushoto.Wewe baba badilika,okoa watu wako...hiyo ndio kazi tuliokupa kwa njia ya kura.

Sasa ni kama hata data zinapikwa,watu wengi wanakufa,tumeanza kupoteza hata wahudumu wa afya ambao ni askari wetu wa mstari wa mbele...Watumishi wa afya wameanza kufa kwa maambukizi ya kukosa PPE!

Serikali ipo,inaaminisha tutapona kwa mvuke,ni labda kweli,lakini kwanza ilipaswa tuwaambie watu wetu kuwa hali ni mbaya,kukiri kuzidiwa na ugonjwa huu sio udhaifu wa kiuongozi bali ni uimara wa kiuongozi,hii ni kwasababu unawapa watu wako taarifa iliyo kamili na bora.

Sasa barakoa zilizothibitishwa na mamlaka za viwango zinakosa wateja,sababu Rais kaongea hadharani kuwa haziaminiki sababu zinaweza kuwa na virusi.Kazi hii sasa imeachiwa kwa machinga na mafundi cherehani,ambao sasa wanachonga barakoa zisizo thibitishwa ubora wake na mamlaka yoyote.

Si mbaya kuwa na barakoa ya kitambaa,lkn ni hakika kuwa wataalamu wanaeleza kuwa haizuii virusi kwa kiwango hicho zaidi ya kuzuia vumbi tu,lkn haya yote ni sababu ya kauli ya Rais ambayo ina mamlaka ndani yake.

Katika masoko,makanisani na misikitini bado watu wanajazana...Hali ni mbaya,na kwa sababu kwa siku kadhaa serikali imeanza kutaja tu wanaopona kwa idadi kubwa,hatutaji tena vifo,tukidhani kifo ni aubu,kumbe kwa mantiki ya ugonjwa huu wanaopona hata wakiwa 1000,lazima tulie na aliyekufa mmoja,sababu uhai na utu wa mtu una thamani isiyofananishika.Kila mahali sasa watu wamelegeza kufuata kanuni za afya na kujikinga wakiona kuwa wataugua na kupona.

Kuusema ukweli juu ya ugonjwa huu si kuleta hofu,ni kuelezea ukweli na uhalisia wa madhara ya gonjwa hili.Kuficha data sio sifa za uongozi bora,bali ni sifa za uongozi mbovu unaouwa watu wake kwa kufanya "Massaging of data"

Toka mafichoni Rais,wewe ni Amiri Jeshi mkuu,kaa mstari wa mbele...Umekuwa ukivaa magwanda kuonyesha u mwanajeshi,sasa onyesha kwa vitendo...Njoo mbele baba njoo,wasisitize watu wako kuwa hali ni mbaya.

Mikoa iliyoathirika kama Dsm,si lazima uifunge,ruhusu magari ya mizigo na chakula kuingiza na kutoa bidhaa kupeleka mikoani.Hii itasaidia kupunguza maambukizi.

Huwezi kuelewa bandiko hili,mpaka sehemu ya ndugu au jamaa yako afe kwa ugonjwa huu katika mazingira ambayo kuna uzembe mkubwa kutoka kwa watu tuliowapa dhamana...Hii ni ujinga,ni ajabu sana kwanini watu wanashindwa thamini maisha ya watu na wanaona pesa ni bora zaidi.

Zile tambo zote na mikakati mliyotutambia kuwa hii ni serikali mpya,mbana zimefifia??Okoa maisha ya watu wako,pesa makaratasi.
Uhai na watu havina Kiki Kama vitu.Hata tv ya ccm uonyesha vitu sio watu.
 
Back
Top Bottom