Ni ujinga kuisifia Serikali wakati nchi inapita kwenye janga la ukosefu wa nishati

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,566
41,085
Lazima uwe punguani hasa kuamini kuwa nchi inaweza kupata maendeleo bila nishati ya uhakika ya umeme.

Kwa sasa, nchi nzima haina nishati ya umeme wa uhakika. Hakuna mkoa hata mmoja unaoweza kupata umeme masaa 24 angalao kwa siku 4 mfululizo.

Kama nchi ingekuwa na Serikali inayojua uchumi, na wananchi wanaojielewa, sasa hivi ilitakiwa kuwepo na tangazo la nchi kuwepo kwenye janga kuu la linalosababisha ujenzi wa uchumi kudorora kutokana na kukosekana kwa nishati ya umeme.

Kwa sasa hakuna kiwanda kinachoweza kufanya uzalishaji wowote kwa faida.

Fikiria, kama una kampuni ina wafanyakazi 1,000. Halafu katika wiki umeme unakatika kwa masaa 12 kwa siku 4. Kwa mwezi, hii ni sawa na:

12×4×30×1000= 1,440,000 workman hours lost. Kama kwa wastani kila mfanyakazi analipwa sh 500,000 kwa mwezi na anafanya kazi kwa masaa 8 kwa siku, kwa siku 26 kwa mwezi; ina maana kwa saa 1, mfanyakazi analipwa sh 2,403 kwa saa.

Kwa masaa hayo 1,440,000; ina maana kupitia tu mishahara, kiwanda kinapata hasara ya sh 1,440,000×2,403= 3,460,320,000. Hii ni katika mishahara pekee yake, bado gharama nyingine. Hicho ni kiwanda kimoja. Fikiria kama kuna viwanda 100 au zaidi.

Hapa unaongelea viwanda tu, bado migodi, biashara mbalimbali kubwa na ndogo. Fikiria pia huduma kama afya, ambazo zinazotegemea nishati ya umeme.

Jambo la kusikitisha sana ni kuwa wakati haya yanatokea, watawala na baadhi ya watu fulani wajinga wanafiki wanaisifia Serikali eti inafanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kutokea. Nadhani hawa watu, labda wanamaanisha kuwa Serikali inafanya mambo makubwa kwenye matumbo yao kwa kiasi ambacho hakijawahi kutokea tangu nchi hii ipate uhuru.

Wananchi, tuweke kumbukumbu ya viongozi wote wajinga wanafiki wanaoisifia sana Serikali wakati wananchi wakipita kwenye lindi la moto na mateso ya uchumi na huduma, kutokana na ukosefu wa nishati ya umeme. Hawa wanaoisifia Serikali katikati ya mateso kwa wananchi watambulike kuwa ni maadui wa wananchi na Taifa.

Tungekuwa na viongozi wazalendo, wanaoguswa na matatizo ya wananchi, sahizi nchi nzima tungekuwa tunasikia sauti za viongozi kuikumbusha na kuitaka Serikali itoe majibu kwa janga hili la Taifa la kukosekana kwa nishati ya umeme baada ya uwongo mwingi wa Waziri wa Nishati.

Lakini bahati mbaya tunao viongozi wanafiki, waongo, wanaojali sana manufaa yao binafsi kuliko kushughulika na matatizo ya umma, hatusikii chochote zaidi ya sifa kwa anayewafanya waendelee kuneemeka katikati ya mateso ya wananchi.
 
Sifa zimepitiliza kwa sasa hakuna mtanzania mwenye mawazo yenye tija. Viongozi wote ni kushindana kusifia tu. Mipango ya maendeleo hupangwa na bunge kupitisha, uchawa unasema ni maono ya raisi hapa ndipo ujinga ulipoanzia
 
Kuna siku Hadi kujisaidia utakuja kuita Janga.Jifunze matumizi ya maneno kabla ya kuropoka.
 
Hii mada ni kwaajili ya watu wenye akili timamu na wenye uelewa mkubwa. Wewe pumzika, usichangie chochote. Unajitesa kuchangia kitu kinachozidi uwezo wa akili yako.

Changia mambo ambayo yanaendana na uwezo wa akili yako.
 
Lazima uwe punguani hasa kuamini kuwa nchi inaweza kupata maendeleo bila nishati ya uhakika ya umeme.

Kwa sasa, nchi nzima haina nishati ya umeme wa uhakika. Hakuna mkoa hata mmoja unaoweza kupata umeme masaa 24 angalao kwa siku 4 mfululizo.

Kama nchi ingekuwa na Serikali inayojua uchumi, na wananchi wanaojielewa, sasa hivi ilitakiwa kuwepo na tangazo la nchi kuwepo kwenye janga kuu la linalosababisha ujenzi wa uchumi kudorora kutokana na kukosekana kwa nishati ya umeme.

Kwa sasa hakuna kiwanda kinachoweza kufanya uzalishaji wowote kwa faida.

Fikiria, kama una kampuni ina wafanyakazi 1,000. Halafu katika wiki umeme unakatika kwa masaa 12 kwa siku 4. Kwa mwezi, hii ni sawa na:

12×4×30×1000= 1,440,000 workman hours lost. Kama kwa wastani kila mfanyakazi analipwa sh 500,000 kwa mwezi na anafanya kazi kwa masaa 8 kwa siku, kwa siku 26 kwa mwezi; ina maana kwa saa 1, mfanyakazi analipwa sh 2,403 kwa saa.

Kwa masaa hayo 1,440,000; ina maana kupitia tu mishahara, kiwanda kinapata hasara ya sh 1,440,000×2,403= 3,460,320,000. Hii ni katika mishahara pekee yake, bado gharama nyingine. Hicho ni kiwanda kimoja. Fikiria kama kuna viwanda 100 au zaidi.

Hapa unaongelea viwanda tu, bado migodi, biashara mbalimbali kubwa na ndogo. Fikiria pia huduma kama afya, ambazo zinazotegemea nishati ya umeme.

Jambo la kusikitisha sana ni kuwa wakati haya yanatokea, watawala na baadhi ya watu fulani wajinga wanafiki wanaisifia Serikali eti inafanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kutokea. Nadhani hawa watu, labda wanamaanisha kuwa Serikali inafanya mambo makubwa kwenye matumbo yao kwa kiasi ambacho hakijawahi kutokea tangu nchi hii ipate uhuru.

Wananchi, tuweke kumbukumbu ya viongozi wote wajinga wanafiki wanaoisifia sana Serikali wakati wananchi wakipita kwenye lindi la moto na mateso ya uchumi na huduma, kutokana na ukosefu wa nishati ya umeme. Hawa wanaoisifia Serikali katikati ya mateso kwa wananchi watambulike kuwa ni maadui wa wananchi na Taifa.

Tungekuwa na viongozi wazalendo, wanaoguswa na matatizo ya wananchi, sahizi nchi nzima tungekuwa tunasikia sauti za viongozi kuikumbusha na kuitaka Serikali itoe majibu kwa janga hili la Taifa la kukosekana kwa nishati ya umeme baada ya uwongo mwingi wa Waziri wa Nishati.

Lakini bahati mbaya tunao viongozi wanafiki, waongo, wanaojali sana manufaa yao binafsi kuliko kushughulika na matatizo ya umma, hatusikii chochote zaidi ya sifa kwa anayewafanya waendelee kuneemeka katikati ya mateso ya wananchi.
Mkweeeeee!!!
Screenshot_20230918_104017.jpg
 
absolutely,mimi dispensary kwangu nalazimika kuwasha jenereta,umeme ukirudi hata hauhna ngugvu stabilizer inasoma 150V in put kwa kujitahidi,hauweizi kusukuma baadhi ya mashine
 
Back
Top Bottom