Tulio na madigrii tunaaibishwa sana na failures aisee! Nini maoni yako?

Lazima watu waelewe kinachofanya mafanikio sio degree ya MTU au masters ya MTU ila ni akili ya MTU binafsi...

Niliwai kuambiwa Na Mzungu Mmoja kuwa Shule inafundisha MTU kuzungumza lugha flani kama ni engineer utazungumza lugha ya kiingineer lakini si kwa sababu umesoma basi uwe unagundua gundua vitu kila mara...

Nilichogundua vyuo vyetu Tanzania vinaua watu wote wenye akili ata kama MTU alikuwa mtundu vipi baada ya CHUO akili azipo tena utamuona Na bahasha anazunguka..

Mfano Mdogo tu uwa najiuliga wakati tuko CHUO tunaambiwa lazima tuwe tofauti Na watu wasio soma...wakati nje unaambiwa ujichanganye ili kuongeza ufanisi Na akili yako bila kujali kitu chochote au kudharau MTU....
 
Hao baada ya kurudi mtaani wamefanya nin labda
duh mkuu una maswali magumu hadi sijui nikujibu vp..!!Mimi mwenyewe nilikuwa siamini kama wewe nikaamua kufanya utafiti wangu binafsi kwa kutembelea viwanda vya madawa n.k,unaweza kuona tuu jinsi ambavyo ni vigumu kujua mtu anafanya nini kwa sasa mtaani kwa sababu ni wengi,siku zote wasomi hufanya mambo si kwa ajili yao binafsi wanafanya mambo kwa ajili ya jamii,anaweza asiwe bilionea lakini mchango wake kwa jamii ukawa ni mkubwa sana..
 
Nakuelewa mkuu!

Kuhusu kupokea hela manually za wateja stendi ni katika kudharau business process za huyu mpuuzi.Ni kwamba kwa process hiyo huwezi kukusanya hela katika enterprise level ukapata turnover ya billions kwa mwaka.Huwezi!

Kwa njia hiyo,hiyo biashara ni uchuuzi!

Sema una mabasi elfu moja,utaweza kweli kukusanya manually?Kuna limit hapo tayari!Hiyo biashara ni kweli ya watu wa lasaba!Ndio level yake!

Angefanya innovation ya payment system kuweza kufacilitate large number of buses bila mtu kuiba then angefanikiwa!

Jinga jinga tu hilo puuzi.Level zake ni biashara za kichuuzi tupu!
Haya mkuu nimekupata!! Though Musukuma kasema ukweli ambao wengi wetu wasomi hatupendi kuusikia
 
hivi hao wamiliki wa viwanda bila ya watu walioelimika hizo mashine wangezipata wapi??
ni mtanzania mjinga asiyeweza kuuona umuhimu wa elimu!
mambo yote ya sayansi na teknolojia yanayoonekana leo hii ni matokeo ya mapinduzi ya elimu duniani!!hivyo maendeleo ni teknolojia na sayansi ambayo msingi wake ni elimu..
yeye kasema wao wa darasa la saba wanaajiri magraduate, kweli si kweli? Hivi Mo ana digrii ngapi? Bakhresa je? Msukuma? Wale wakinga pale kariakoo
 
Ni kweli kwa sababu msomi wa degree hawezi kwenda Makete kwa mganga wa kienyeji kutafuta ndago ya utajiri..
 
Una tatizo. Technology inayotumika kujenga na kumaintain viwanda (vya Tanzania) haitokani na wasomi wa Tanzania. Inatoka nje ya nchi.

Kwahiyo alichosema msukuma ni ukweli mchungu wasomi wa Tanzania hawapendi kusikia.

Pole msomi.
Kweli mkuu.
 
tatizo lenu mnazungumzia vitu jumlajumla,kwani we unawajua maprofesa wote wa Tanzania na ishu zao??au unadhani kila mtu anapenda kujionesha vitu au miradi anayomiliki??haya nitajie program ya kompyuta iliyogunduliwa na mtu ambaye hakuenda shule??
Kazi ya wasomi wa Tanzania ni Ku complicate nadharia ya maarifa ili watese watu kwenye mitihani.
Niliwahi kusema kuwa,ukiwapa wasomi wabobezi wa michezo watengeneze mtaala wa mpira wa miguu,halafu ukampa Messi asome,lazima atapata zero,au umpe diamond mtihani wa somo la muziki,atapata alama 2%! Sasa ukija kwa wasomi wetu wa kitanzania,Muziki ana A,ila hakuna chochote alichofanya kuhusu muziki,ukitoa paper ya michezo watu watakuwa na A nyingi ila nenda kwenye soka lenyewe.Hao ndio wasomi tulio nao.
Elimu yao imebaki kuwa silaha ya kutukania na kutambia wasio na elimu.Ndio maana kuna misamiati mingi inayoonyesha kitu chochote cha kipumbavu,hata kama kimefanywa na msomi mwenye PhD, kinanasbishwa na mtu asiyesoma.
Msukuma anayo sababu ya kuwananga wasomi kutokana na tabia na maamuzi yao yasiyoonyesha umuhimu wa wao kuwa wasomi na kwamba wengi wao ndio wanao create matatizo badala ya kuleta suluhu
 
Labda nitoe ufafanuzi kuhusu wazo la elimu.

Inapaswa tujue kwamba kuna aina mbili za elimu.
Ya kwanza ni elimu rasmi
Ya pili ni elimu isiyo rasmi.

Katika Jamii ya kitanzania umetokea utamaduni wa wale walioelimika kupitia mfumo usio rasmi kusema hawana elimu wakiamini mwenye elimu ni yule tu alìyeanza darasa la kwanza hadi kufika chuo kikuu.

NB: Watanzania tubadilike
noted
 
sababu ni moja wewe utatumia miaka zaidi ya 20 ili kuipata degree. Yeye muda huo alienda moja kwa kwenue biashara ama kilimo.

Ila kutokana na wingi wa walioenda kwenye biashara/kilimo wenye mafanikio ya wastani kiasilimia ni wachache sana kulingana na wale wenye degree.

Bila elimu hata yeye asingejua kuna kitu gari wala hivyo viwanda. Kazi zote za kiufundi zinaitaji elimu hivyo mawazo ya hivyo kudharau wenye shule kichwani yako cheap sana.
 
Kazi ya wasomi wa Tanzania ni Ku complicate nadharia ya maarifa ili watese watu kwenye mitihani.
Niliwahi kusema kuwa,ukiwapa wasomi wabobezi wa michezo watengeneze mtaala wa mpira wa miguu,halafu ukampa Messi asome,lazima atapata zero,au umpe diamond mtihani wa somo la muziki,atapata alama 2%! Sasa ukija kwa wasomi wetu wa kitanzania,Muziki ana A,ila hakuna chochote alichofanya kuhusu muziki,ukitoa paper ya michezo watu watakuwa na A nyingi ila nenda kwenye soka lenyewe.Hao ndio wasomi tulio nao.
Elimu yao imebaki kuwa silaha ya kutukania na kutambia wasio na elimu.Ndio maana kuna misamiati mingi inayoonyesha kitu chochote cha kipumbavu,hata kama kimefanywa na msomi mwenye PhD, kinanasbishwa na mtu asiyesoma.
Msukuma anayo sababu ya kuwananga wasomi kutokana na tabia na maamuzi yao yasiyoonyesha umuhimu wa wao kuwa wasomi na kwamba wengi wao ndio wanao create matatizo badala ya kuleta suluhu
Ni kweli kabisa ndugu!
 
Swali ni je katika watu ambao hawajaenda shule kuna kina bakhresa wangapi
kwani walioenda shule, wapo wangapi waliofikia walau nusu ya kina bahresa, usiende mbali. binafsi nina kamasters tu na nategemea niitwe dr someday. lakini still kuna watu hawana hata degree lakin uwezo wao kibiashara na kiuongozi ni mzuri sana, na ndio hao wanaomiliki viwonder!hahaha
 
Boss fanya tathmini japo sitabase zaid kwenye viwanda na biashara kwa ujumla deep
Fanya random sampling kwa idadi ya ya walioenda shule na wasioenda shule then compare kundi lipi lina watu wenye unafuu Wa kujikimu kimaisha kuliko jingine ,elimu ina nafasi Kubwa sana
kwa kukusaidia, ulishawahi kuona wapi profesa tajiri? wengi ni middle class tu na hela waliyonayo huwa inawafaidisha kizazi chake cha kwanza, kile cha pili cha wajukuu hawafaidi chochote zimeshaliwa na kizazi cha kwanza.
 
Labda degree, we usomee PhD. hicho kiwanda utaanzisha saa ngapi
kwanza maswali ya kuthubutu yanakuwa mengi, hauamini kama utafanikiwa, na unaleta theory nyingiiii, unapiga mahesabu mengii mwishowe unakata tamaa unaaza kusubiria mshahara wa kuajiriwa na PHD yako.
 
Back
Top Bottom