Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 42,561
- 105,361
Nilitakiwa kingia kibaruani saa 18:00, na sikuhiyo pia nilikuwa ninamiadi ya kukutana na mdada m-moja niliekuwa nimemtingoza kwa muda wa kama miezi 3 mfululizo pasipo na mafanikio.
Siku mbili kabla mvua kuubwa ilikuwa imenyesha na kuendelea kudondosha manyunyu kwa masaa kadhaa, hali iliyo pelekea ardhi ya maeneo yale kutengeneza tope la kutisha na hali ya hewa kubadilika na kufanya baridi jembamba.
Muda wa kwenda kazini ulifika nilijiandaa na nikamuaga mpenziwangu tuliekuwa tukiishi pamoja nakwenda kazini. Nilipiofika sikuhiyo nilikuwa sina amani, mawazo yalinijaa huku nikiwaza nijinsigani nitaweza kuondoka kazini ili nirudi kwenye miadi ya kwenda ku.... na yule mdada niliekua nikimsotea kwamuda mrefu. Basi ndipo nilipo panga mkakati wa kudanganya boss kwamba ninamatatizo ya kifamilia, boss aliniruhusu na kufikia mida ya saa 21:00 nilikua tayari nimeshafika kwenye miadi na kukaribishwa ndani na yule dada.
Kwakuwa kile chumba hakikuwa na kiti ilibidi anikaribishe nikae kitandani, nami bila hiyana huyooo nikakaa huku nikijichekesha na kujitahidi kuonyesha upendo mkubwa juu yake, nae hakuwa mchache mdada akanikirimu kwa mabusu huku akonivua nguo (sare) za kazini, kwani zilikua zimeloa kwa mvua ilioninyeshea nikiwa njiani na nikabaki na kaptura tu.
Kabla hatuja fanya chochote, basi akaniomba nikaoge ili tuje tulale kwa raha zetu, akanipelekea maji bafuni, naye akajifinga kanga moja ili tukaogo pamoja.
Wakati tunaoga, ghafla tuliskia kishindo kikubwa sana na alipo mulika nje kutokea bafuni, tuliona nyumba yoote imeanguka.
Sikuweza kuoga tena, viatu pamoja na nguozangu, walet ikiwa na vitambulisho na kadi za benki zote zilikua zimefunikwa na udongo pamoja na mabati, ilinilazimu niondoke kwenda nilipokua nikiishi nikiwa na kaptura, sikuweza kusubiri watu wajae kwani walikuwa wananijua pamoja na mwanamke wangu, pia yule dada alikua ni mlokole nailikua inajulikana pale mtaani.
Hivyo ndivyo nilivyo koswa na kifo.