Mkuu ninaamini mungu alitaka kunionyesha upendo alionao juu yangu
Kuna jamaa, sasa ni marehemu, alikuwa ameoa na ana watoto. SIku hiyo alikuwa anaingia kazini zamu ya usiku, kiwanda cha saruji wazo hill.
Ilipofika jioni, alimwambia mwenzake kwamba "amsainie" hatokwenda kazini anakwenda outing na mchuchu (mke wa mtu). Kweli, rafiki kaenda kamsainia kazi ikaanza.
Huyu jamaa mume wa mtu akaenda zake na mke wa mtu huku akiwa anaendesha gari lake. Wakaenda baa ya Kapongo, maarufu sana Tegeta. Hii habari ilitolewa kwenye vyombo vya habari, kama sikosei.
Jamaa kaenda kula bata weee, mpaka asubuhi. Saa kumi na moja asubuhi walitoka hao mdogomdogo na gari yao.
Kuingia tu barabara kuu pale Tegeta, walivamia kwa nyuma lori la sementi. Walifariki pale pale.
Ishu ilikuwa kazini, jamaa kazini kaulizwa Fulani alikuja kazini? Alisema ndiyo (wakati hakwenda). Jamaa anakuja kujua mshikaji alishapotea kwenye ajali.
Unadhani yale mazingira yangeelezekaje?
Inasemekana mke wa mtu yule alofariki, alimuaga mumewe kwamba anaenda kwa ndugu yake sijui wapi.