Tulianza kwa kumchukia mama wa kambo, na sasa ni zamu ya shemeji. Nini tatizo?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,523
27,017
Salamu waungwana.

Nianze kwa kujipigia mstari [to declare interest], natarajia kuingia ndoani muda wowote hata sasa punde tu ubavu sahihi ukipatikana.

Katika hatua za ukuaji tunaanza tukiwa watoto wadogo, kipindi hiki mtoto hana maamuzi wala uchaguzi wa kipi cha kumfaa na kipi kisichofaa, hutegemea mzazi au mlezi kumfanyia maamuzi kwa kadri ya mapenzi yao.

Kuna wale wamebahatika kulelewa na mama wa kambo, wengi wao wana kumbukumbu mbaya, na wote tunajua kuna ule msemo kuwa “Mama wa kambo si mama”.

Sasa kumeibuka kundi lingine la kuchukiwa, nalo ni mashemeji, nafikiri ni pande zote mbili.

Kuna imani kuwa shemeji wa kike [mawifi] ni wachonganishi, hawafai kuishi nao la sivyo watakuvunjia ndoa yako. Hawa ni wale wadada kwenda kuishi kwa kaka yao aliyeoa, na hii hasa sio habari ya uzi huu.

Kundi lengwa hapa ni shemeji wa kiume, kwenda kuishi kwa dada yake aliyeolewa, imeonekana ni kitendo cha fedheha sana na kinapigwa vita kila leo [hata hapa JF mtu akiambiwa “unaishi kwa shemeji” ni tusi kubwa].

Tukiacha mapungufu ya mtu mmoja mmoja ambayo kila mtu anayo yake, nini hoja ya ujumla inayohalalisha ‘ubaya’ wa kijana kuishi kwa shemeji..?

Sikuwahi kulipa umuhimu suala hili, ukizingatia upendo wangu kuishi na watu, na nikioa nilitamani ikitokea shemeji anakuja kuishi kwangu awe huru na mwenye furaha.

Hebu tuambizane, tukiacha hiyo mnaita fedheha [ambayo kwa kijana anayejitafuta hapaswi kuijali sana], nini hasa msingi wa hoja yetu ya kuchukia kuishi kwa shemeji..?

Nawasilisha.
 
Wanasema wanakula sanaaa hawafanyi kazi
Wanamjazia Choo Sasa sijui hataki mtu akila asiende hajaa kutoa mabaki??

Juzi hapa mtaani mmoja amepigwa na manati kisa ameficha ugali mvunguni mwa kitanda eti shemeji asile
Pumbavu kabsaa tulimwambia mzee sepa rudi kijiji ukale maombo
Bora lawana kuliko fedhehaa
Jamaa alipiga manati za hatari kisa tuu ugali tembele daah haya maisha???
Alishonwa nyuzi tatu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa ni competition ya affection kwa mume.
Bila kupendelea kokote most of ndugu wa mume hujiona wao ndio wenye ukaribu saana kuliko mke, na mke usipokuwa mjanja hujikuta akianza kucompete nao ili wakuone wewe ndio mama la mama, mama mwenye nyumba, mama mjengo.

Ila kuna waliozaliwa na ujanja unakaa pembeni unawacheki tu panda shuka zao wanachoka na sarakasi zao hawakuoni kama threat tena.Hapa ujanja ni kujifanya huoni! Kula na vipofu.
 
Juzi hapa mtaani mmoja amepigwa na manati kisa ameficha ugali mvunguni mwa kitanda eti shemeji asile
Pumbavu kabsaa tulimwambia mzee sepa rudi kijiji ukale maombo
Bora lawana kuliko fedhehaa
Jamaa alipiga manati za hatari kisa tuu ugali tembele daah haya maisha???
Alishonwa nyuzi tatu.

Nimecheka kinyama kwa huu mkasa japo nahisi sijaelewa vizuri, aliyepigwa manati ni yupi..?
 
client3
Mkuu nimekupata vema, sema umedadavua kwa upande mmoja tu ‘ndugu wa mume’.... vipi hawa ndugu wa mke mbona imekuwa ikichukuliwa fedheha..?
 
Nimecheka kinyama kwa huu mkasa japo nahisi sijaelewa vizuri, aliyepigwa manati ni yupi..?
Shemeji mkuu ndiyo alikula manati
Kamnyima jamaa ugali tembele tuu
Usicheke aise maisha magumu Sana

Kaka yake alimfukuza dogo arudi kijiji
Dogo kamaliza form four mwaka Jana tuu

Ila yule dada alikoma yupo saiv anauguza kidonda chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasema wanakula sanaaa hawafanyi kazi
Wanamjazia Choo Sasa sijui hataki mtu akila asiende hajaa kutoa mabaki??

Juzi hapa mtaani mmoja amepigwa na manati kisa ameficha ugali mvunguni mwa kitanda eti shemeji asile
Pumbavu kabsaa tulimwambia mzee sepa rudi kijiji ukale maombo
Bora lawana kuliko fedhehaa
Jamaa alipiga manati za hatari kisa tuu ugali tembele daah haya maisha???
Alishonwa nyuzi tatu

Sent using Jamii Forums mobile app

Eti kaficha ugali mvunguni duuh, si bora kumfukuza tu
 
Mara nyingi tatizo huanza kwa kutaka special treatment.

Unaenda kwa mtu halafu hautaki kufanya kazi yoyote, unajaa kiburi na unakuwa chanzo cha ugomvi. Hapo hamwezi kuishi vizuri.

Ukienda kwa mtu usipeleke sheria zako, fuata sheria unazozikuta.
 
Nadhani huwa ni case chache sana kukuta ndugu wa mke hawapatani na shemeji yao, unajua kwa nini? huwa tunawafundisha tabia nzuri na kuwapa abcd za kuendana na mume na mashtaka huwa hatupeleki kwa mume tunaonyana na kumalizana kimyakimyaa hata liwe baya vipi ili tu kutojitukanisha kwa upande wa pili.

Ukikuta ndugu wa mke vimeo ujue hao kweli wamepinda for sure, matumizi ya vileo na bangi na mwingine kajishindikania tu

client3
Mkuu nimekupata vema, sema umedadavua kwa upande mmoja tu ‘ndugu wa mume’.... vipi hawa ndugu wa mke mbona imekuwa ikichukuliwa fedheha..?
 
Mkuu wewe unaweza kuvumilia usiku mzima unasikia sauti za dada yako, wakiwa wanafanyana na sio kimasihara?
 
Mkuu wewe unaweza kuvumilia usiku mzima unasikia sauti za dada yako, wakiwa wanafanyana na sio kimasihara?

Sio katika mazingira yote utaweza kusikia hizo sauti, unakuta nyumba ina nafasi tu na unapewa chumba cha kulala.... kama mazingira hayaruhusu ungeweza kuzisikia hata kama ni kwa ndugu au mtu mwingine yeyote.
 
client3
Na hapo sasa umeupata msingi wa hoja yangu, kweli ni nadra sana ndugu wa mke kuleta ujuaji kama ulivyoelezea hapo juu.... bali kuna huu mtazamo hasi wa kijamii.

Mfano zile kejeli kuwa unaishije kwa shemeji kwani mmeolewa wote, siku dada’ako ‘akitimuliwa’ mnafungasha wote.... na mengine mengi kama hayo.
 
Mara nyingi tatizo huanza kwa kutaka special treatment.

Unaenda kwa mtu halafu hautaki kufanya kazi yoyote, unajaa kiburi na unakuwa chanzo cha ugomvi. Hapo hamwezi kuishi vizuri.

Ukienda kwa mtu usipeleke sheria zako, fuata sheria unazozikuta.

Kwanini kwa shemeji, hata ukifanya yote hayo bado jamii itakuona kana kwamba unajipendekeza tu.... na utasikia kwani mmeolewa wote..?
 
Kwanini kwa shemeji, hata ukifanya yote hayo bado jamii itakuona kana kwamba unajipendekeza tu.... na utasikia kwani mmeolewa wote..?
Jamii inaamini mtoto wa kiume anatakiwa kupambana. Sasa ukiwa kwa shemeji inaamini vinginevyo.
 
Kuishi kwa mume wa dada yako kuna muda fedheha itazidi. Fikiria wakigombana mbele yako unajisikiaje, au dada yako akipewa talaka, utaishi wapi. Pia shida nyingine ni wasiwasi wa wewe kuzoeana na wifi za dada ako (kama wapo) unaweza kuanzisha nao mahusiano. Yangu ni hayo.
 
Sio katika mazingira yote utaweza kusikia hizo sauti, unakuta nyumba ina nafasi tu na unapewa chumba cha kulala.... kama mazingira hayaruhusu ungeweza kuzisikia hata kama ni kwa ndugu au mtu mwingine yeyote.
Sasa hapo wewe unajua kuwa husikii ila rafiki zako wote tunajua kuwa wewe jamaa ni mvumilivu.

Mara nyingi mtoto wa kiume kwa kaka yake sio ishu sana pia wa kike kwa dada yake sio ishu sana hasa kama wanajielewa na wanakua msaada.
Ila wa kiume kwa dada ni balaa na kike kwa kaka ni balaa kubwa zaidi.
Nafikiri kuna mvutano wa nguvu unaotokea kwa sababu mmoja atataka kumtetea dada ya kila wakati kama walivyokua wanakua mwengine atataka aringe kwa kaka yake na hatokubali kupelekeshwa
 
Tatizo ni watu kupenda kuhemea vya watu kwa kutokutaka kufanya kazi na kuwa na sehemu zao za kuishi. Kupenda vya bure mpaka wanaishia majungu fitina na umbeya.
Yote yanasababishwa na uvivu wa kazi uliopitiliza na uvivu wa kufikiri. Typical Tanzanians...kama alivyosema JPM...na asiyefanya kazi na asile...
 
client3
Na hapo sasa umeupata msingi wa hoja yangu, kweli ni nadra sana ndugu wa mke kuleta ujuaji kama ulivyoelezea hapo juu.... bali kuna huu mtazamo hasi wa kijamii.

Mfano zile kejeli kuwa unaishije kwa shemeji kwani mmeolewa wote, siku dada’ako ‘akitimuliwa’ mnafungasha wote.... na mengine mengi kama hayo.
Aaah sasa nimekuelewa mimi niliingia chocho vibaya sana, kumbe ulikusudia mtazamo anaotazamwa anayekaa kwa shemeji, kwa kweli inategemea sana umri wako na nini unafanya na nini unategemea kufanya.Kama umekaa tu huna ufanyacho ni aibu sana, kama ni issue za likizo, kusubiria michongo ya biashara huku na kule au post za ajira haina shida.

Ni aibu kwa nini?
1. Mara nyingi jamii zetu breadwinner ni mwanamme, yeye ndio anafanya kazi analeta chakula nyumbani familia inakuja ikiwamo huyu shemeji ndugu wa mke, sasa kwa shemeji huonekana kama kupe akitegemea mwanamme mwenzie ahenyeke yeye ale tu.
2.Anayeolewa ni dada sasa hutafsirika kama matusi kuwa unategemea k ya dada kuishi,kwamba asingekuwa dada kutoa k wewe huli huna pa kuishi.
3.Kwenye maisha kuna kuhitilafiana kwa mke na mume sasa nyakati hizi huwa ngumu sana kwa shemeji maana atakosa pa kuegemea kwa hiyo kumweka mbali na scenario kama hizi then shemeji is highly discouraged to live with the in-law.
4.Huwa ni mbinu tu za kumfanya mwanamme kutokubweteka asichukulie poa tu maisha ya kula kulala.
 
client3

4. “Huwa ni mbinu tu za kumfanya mwanamme kutokubweteka asichukulie poa tu maisha ya kula kulala”.

This is very positive, asante kwa hili.... naahidi nami nitakuwa namaanisha hivi ikitokea namchallenge mtu aishiye kwa shemeji.

Na hii ni kwa shemeji wa kiume, wale wa kike risk yao kubwa nadhani ni kuliwa na mume.... hawa mara nyingi mke inampasa awe makini sana na wadogo zake wa kike.
 
Kuishi kwa mume wa dada yako kuna muda fedheha itazidi. Fikiria wakigombana mbele yako unajisikiaje, au dada yako akipewa talaka, utaishi wapi. Pia shida nyingine ni wasiwasi wa wewe kuzoeana na wifi za dada ako (kama wapo) unaweza kuanzisha nao mahusiano. Yangu ni hayo.

Umesema vema mkuu, kwanini mtazamo ujengwe kwa misingi ya kutabiri [ikiwa wakigombana au talaka].?

Hiyo kuhusu kuzoeana na ‘mawifi’ sikuiwazia, ila nimeipata kwako na kweli matokeo yake sio mazuri ikitokea yamebuma... ila bado simwoni shemeji mkuu [mwenye nyumba] katika kosa lolote hadi hapo.
 
Back
Top Bottom