Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,656
- 27,320
Salamu waungwana.
Nianze kwa kujipigia mstari [to declare interest], natarajia kuingia ndoani muda wowote hata sasa punde tu ubavu sahihi ukipatikana.
Katika hatua za ukuaji tunaanza tukiwa watoto wadogo, kipindi hiki mtoto hana maamuzi wala uchaguzi wa kipi cha kumfaa na kipi kisichofaa, hutegemea mzazi au mlezi kumfanyia maamuzi kwa kadri ya mapenzi yao.
Kuna wale wamebahatika kulelewa na mama wa kambo, wengi wao wana kumbukumbu mbaya, na wote tunajua kuna ule msemo kuwa “Mama wa kambo si mama”.
Sasa kumeibuka kundi lingine la kuchukiwa, nalo ni mashemeji, nafikiri ni pande zote mbili.
Kuna imani kuwa shemeji wa kike [mawifi] ni wachonganishi, hawafai kuishi nao la sivyo watakuvunjia ndoa yako. Hawa ni wale wadada kwenda kuishi kwa kaka yao aliyeoa, na hii hasa sio habari ya uzi huu.
Kundi lengwa hapa ni shemeji wa kiume, kwenda kuishi kwa dada yake aliyeolewa, imeonekana ni kitendo cha fedheha sana na kinapigwa vita kila leo [hata hapa JF mtu akiambiwa “unaishi kwa shemeji” ni tusi kubwa].
Tukiacha mapungufu ya mtu mmoja mmoja ambayo kila mtu anayo yake, nini hoja ya ujumla inayohalalisha ‘ubaya’ wa kijana kuishi kwa shemeji..?
Sikuwahi kulipa umuhimu suala hili, ukizingatia upendo wangu kuishi na watu, na nikioa nilitamani ikitokea shemeji anakuja kuishi kwangu awe huru na mwenye furaha.
Hebu tuambizane, tukiacha hiyo mnaita fedheha [ambayo kwa kijana anayejitafuta hapaswi kuijali sana], nini hasa msingi wa hoja yetu ya kuchukia kuishi kwa shemeji..?
Nawasilisha.