PreGE2025 Tulia Trust yatoa msaada wa masomo kwa walioshindwa kuendelea na elimu baada ya baba yao kufariki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Taasisi ya Tulia Trust Chini ya Mkurugenzi Wake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) Dkt. Tulia Ackson imewasaidia mahitaji watoto wa familia moja walioshindwa kuendelea na masomo kwa kukosa vifaa vya shule.

Tulia Trust imewasaidia vifaa vya shule ikiwa ni pamoja na daftari, begi, sare za shule, viatu pamoja na nguo za nyumbani Latifa Mengondele (12) anayesoma darasa la sita na mdogo wake Ivan Mengondele (7) aliyetakiwa kuanza masomo ya chekechea katika shule ya Msingi Hayanga iliyopo kata ya Isyesye jijini Mbeya.

Watoto hao walishindwa kuendelea na masomo kwa kukosa vifaa vya shule baada ya baba yao kufariki huku mama yao akiondoka nyumbani na kwenda kusikojulikana kabla hata ya kifo cha baba yao hivyo kwa sasa wanaishi kwenye nyumba iliyoachwa na baba yao huku wakipata msaada kutoka kwa shangazi yao ambaye hana uwezo.
 
This is too low for a speaker on National Asembly. Yaani kusaidia watoto wawili madaftari na ada ndiyo vitu vya kuwaanika kwenye mitandao??

Huu ni upuuzi wa siasa, msiwatumie wenye shida to build your persona egos
 
Back
Top Bottom