Tulia Ackson ni nani, CV yake ipoje?

Tulia Ackson ni nani, CV yake ipoje?

Aiseee nakumbuka enzi za mama makinda walikuwa wanampelekesha mama wa watu mpaka huruma sasa kaletwa Tulia watu wanasusa shida nini?
 
Nilichokigundua ni kwamba hizi kelele zote dhidi ya Naibu Spika wetu Tulia (PhD) hazina uhusiano wowote ule na kazi yake kama Naibu Spika bali ni mafanikio yake, hilo ndiyo tatizo kubwa, na niseme ukweli kabisa hili siyo kwa chadema/ukawa tu hata kwa wale watu wa kawaida kabisa na wasio na vyama wengi wana wivu dhidi huyu dada!

Kwa maana nimeongea na watu mbalimbali na wengi wao husema kwamba ni mdogo sana, sasa hupima jinsi wao walivyosota kwa miaka kibao wakisaga lami kwanza kuja tu kupata masters na wengine miaka tena kupata PhD halafu wamesota kazini mpaka walipofikia karibia umri wa kustaafu ndiyo labda anafikia cheo kikubwa, lkn dada Tulia(PhD) amezaliwa mwaka 1976 amesoma mfululizo Bsc-Msc-PhD, mwaka 2009 akawa Dean (associate) wa Sheria hapo UDSM, mwaka 2014 akateuliwa na raisi wa JMTZ kwenye uundwaji wa Katiba ya JMTZ, akateuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu, baadaye akateuliwa kuwa Mbunge na Raisi wa V wa JMTZ na mwishowe kuwa Naibu Spika wa Bunge la JMTZ!

Sasa huyo ni dada aliyezaliwa mwaka 1976 na kufikia hapo alipofika leo hii na hii ni kwa merit tu, kwa mafanikio kama haya, kwa nini asipate maadui? Watu kama Tundu, Mbowe,Msigwa, Mbatia &Co. wameshaarchive nini academically? Kwa nini wasimchukie? Wote tunakumbuka Shuleni wale wanafunzi vipanga yaani wenye akili walikuwa wanachukiwa na wanafunzi wengine hasa wale wavivu na v.ilaza!

Na hapo ndipo shida kubwa ilipo na ndiyo maana unaona chuki walionayo ni binafsi na wameilekezea kwa dada Tulia Mwansasu(PhD) na siyo Bunge linaloongozwa na CCM, kwani ukweli ni kwamba hata kama Spika Ndugai au Mwenyekiti yoyote yule wa Bunge akiongoza Bunge leo hii bado kwa chadema/ukawa hakuna kitakachobadilika kwa maana CCM ndiyo wengi Bungeni na hili tumeliona vipindi vyote vya Bunge kuanzia akina Sita, mama Makinda ingawaje wote hawa walitukanwa na chadema lkn kulikuwa hakuna chuki binafsi kama anazopewa dada Tulia!

Hivyo naweza kusema Dada Tulia Mwansasu(PhD) ni victim of her own success, kama wasemavyo Wazungu na kikubwa hapo ni wivu tu watu wanajilinganisha naye wanashindwa kuonisha lkn wanasahau kwamba Dunia ya leo haiendeshwi na Umri tena bali intelligence kama una Intelligence kama ya Msigwa au Mbowe unategemea ufike wapi Dunia ya leo? Mambo ya kubabaisha sijui kudanganya watu wewe mchungaji yameisha!

Tuwe wakweli na nafsi zetu watu kama Mbowe ukiondoa fedha ambazo ni za urithi hivyo hapo jitihada binafsi ni 0, au Lisu, Msigwa, Sugu wanaweza kupata kazi wapi Dunia hii mbali na yale ya utapeli wanayaoyafanya hapa Tanzania?
Dada Tulia Mwansasu(PhD) ana uwezo kutuma CV yake na kupata kazi popote pale Dunia hii, na hapo ndipo shida ilipo, wanaona wivu sema wanashindwa kusema tu na kuliattack hilo mafanikio makubwa kwenye umri mdogo wa dada Tulia wanaamua kumuattack lkn indirectly!
 
wivu..!

ngoja system imtumie alafu imteme kama big g isiyo na ladha..
 
hii nchi in hasara mtu ana PHd hata kujielezea kipindi anaomba kura za unaibu hawezi kashindwa na sakaya sasa nini maana ya usomi wake
 
Mkuu,umetumia kigezo gani kunijiridhisha na hayo uyasemayo? Maana hakuna asiye na mapungufu duniani hata ajikusanyie PhD 200.Na ni kwa nini wamchukie kiwango hicho?
 
Mkuu,umetumia kigezo gani kunijiridhisha na hayo uyasemayo? Maana hakuna asiye na mapungufu duniani hata ajikusanyie PhD 200.Na ni kwa nini wamchukie kiwango hicho?


Wivu dhidi ya mafanikio yake!
 
Mafanikio ni Elimu?
As we human beings we search for ultimate goals but only education with virtue leads to ultimate goal(s)that is happiness, love& dignity.
Kinachofanywa na UKAWA sio hawajui ila ni sehem ya mazoea ya siasa za Tanzania. Labda hawajui nini cha kufanya kwa xaxa
ili kuendana na Rais wa sasa.
 
Wewe mwenyewe umeleta hoja kishabiki tu...unsongelea miaka kuzaliwa sio kuongelea utendaji..kama issue ni elimu kubwa ina maana tungesema Maprof pekee waende kuwa wabunge na viongozi wa serikali maeneo yote...elimu na kaarama ya uongozi ni vitu viwili tofauti...hivi Nyerere alikua Prof? Mbona alikua PM na miaka 39 kwasababu alikua na karama...acha ushabiki wa ajabu
 
Yeye ni wa kwanza kufanikiwa Tanzania?


Hilo swali inabidi uwaulize ukawa/chadema, kwa maana wanaolewa kuhusu mafanikio yanayotokana na jitihada binafsi wanamkubali na kumpenda sana Dada Tulia!
 
Back
Top Bottom