Tulia Ackson ni nani, CV yake ipoje?

Tulia Ackson ni nani, CV yake ipoje?

tuache waonea wivu kina hasheem thabeet.. mbwana samatta, diamond platnum at their 20s tu wanashika mabilion tena kwa kujiajiri wenyewe tumuonee wivu tulia ambaye income yake haifiki hata milion 20 per month na ni mtumwa wa aliyemwajiri...

au kina home shopping futari tu wanatoa zawadi za I phone... kina bakhressa, mafuruki, dewji, raphael, hao ndio wa kuwaonea wivu income ya tulia ya maisha yake yote hadi astaafu wao wanaipata kwa siku tu..


Nilichokigundua ni kwamba hizi kelele zote dhidi ya Naibu Spika wetu Tulia (PhD) hazina uhusiano wowote ule na kazi yake kama Naibu Spika bali ni mafanikio yake, hilo ndiyo tatizo kubwa, na niseme ukweli kabisa hili siyo kwa chadema/ukawa tu hata kwa wale watu wa kawaida kabisa na wasio na vyama wengi wana wivu dhidi huyu dada!

Kwa maana nimeongea na watu mbalimbali na wengi wao husema kwamba ni mdogo sana, sasa hupima jinsi wao walivyosota kwa miaka kibao wakisaga lami kwanza kuja tu kupata masters na wengine miaka tena kupata PhD halafu wamesota kazini mpaka walipofikia karibia umri wa kustaafu ndiyo labda anafikia cheo kikubwa, lkn dada Tulia(PhD) amezaliwa mwaka 1976 amesoma mfululizo Bsc-Msc-PhD, mwaka 2009 akawa Dean (associate) wa Sheria hapo UDSM, mwaka 2014 akateuliwa na raisi wa JMTZ kwenye uundwaji wa Katiba ya JMTZ, akateuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu, baadaye akateuliwa kuwa Mbunge na Raisi wa V wa JMTZ na mwishowe kuwa Naibu Spika wa Bunge la JMTZ!

Sasa huyo ni dada aliyezaliwa mwaka 1976 na kufikia hapo alipofika leo hii na hii ni kwa merit tu, kwa mafanikio kama haya, kwa nini asipate maadui? Watu kama Tundu, Mbowe,Msigwa, Mbatia &Co. wameshaarchive nini academically? Kwa nini wasimchukie? Wote tunakumbuka Shuleni wale wanafunzi vipanga yaani wenye akili walikuwa wanachukiwa na wanafunzi wengine hasa wale wavivu na v.ilaza!

Na hapo ndipo shida kubwa ilipo na ndiyo maana unaona chuki walionayo ni binafsi na wameilekezea kwa dada Tulia Mwansasu(PhD) na siyo Bunge linaloongozwa na CCM, kwani ukweli ni kwamba hata kama Spika Ndugai au Mwenyekiti yoyote yule wa Bunge akiongoza Bunge leo hii bado kwa chadema/ukawa hakuna kitakachobadilika kwa maana CCM ndiyo wengi Bungeni na hili tumeliona vipindi vyote vya Bunge kuanzia akina Sita, mama Makinda ingawaje wote hawa walitukanwa na chadema lkn kulikuwa hakuna chuki binafsi kama anazopewa dada Tulia!

Hivyo naweza kusema Dada Tulia Mwansasu(PhD) ni victim of her own success, kama wasemavyo Wazungu na kikubwa hapo ni wivu tu watu wanajilinganisha naye wanashindwa kuonisha lkn wanasahau kwamba Dunia ya leo haiendeshwi na Umri tena bali intelligence kama una Intelligence kama ya Msigwa au Mbowe unategemea ufike wapi Dunia ya leo? Mambo ya kubabaisha sijui kudanganya watu wewe mchungaji yameisha!

Tuwe wakweli na nafsi zetu watu kama Mbowe ukiondoa fedha ambazo ni za urithi hivyo hapo jitihada binafsi ni 0, au Lisu, Msigwa, Sugu wanaweza kupata kazi wapi Dunia hii mbali na yale ya utapeli wanayaoyafanya hapa Tanzania?
Dada Tulia Mwansasu(PhD) ana uwezo kutuma CV yake na kupata kazi popote pale Dunia hii, na hapo ndipo shida ilipo, wanaona wivu sema wanashindwa kusema tu na kuliattack hilo mafanikio makubwa kwenye umri mdogo wa dada Tulia wanaamua kumuattack lkn indirectly!
 
tuache waonea wivu kina hasheem thabeet.. mbwana samatta, diamond platnum at their 20s tu wanashika mabilion tena kwa kujiajiri wenyewe tumuonee wivu tulia ambaye income yake haifiki hata milion 20 per month na ni mtumwa wa aliyemwajiri...

au kina home shopping futari tu wanatoa zawadi za I phone... kina bakhressa, mafuruki, dewji, raphael, hao ndio wa kuwaonea wivu income ya tulia ya maisha yake yote hadi astaafu wao wanaipata kwa siku tu..


Na hapo ndipo unapokosea hakuna nilipo oanisha mafanikio ya Dada Tulia na fedha, kama ni hivyo ningemtaja Mbowe ambaye amekulia kwenye utajiri tangu mtoto na hajui dhiki ni nini, ningemuweka kwenye watu wenye mafanikio makubwa tangu watoto, na isitoshe hawo uliowataka akina Hashimu, Mbwana hawako Bungeni na wala hawako kwenye Siasa, hivyo mifano yako ingekuwa na maana tu kama ungeleta Mwanasiasa wa upinzani ambaye anaweza kuonyesha mafanikio kama ya dada Tulia kwa umri huwo ...
 
Ameshaanza kulazimisha ubunge Mbeya mjini
 
Back
Top Bottom