Mzurulaji
JF-Expert Member
- Sep 25, 2021
- 284
- 564
Habari zenu wakuu natumai mu wazima wa Afya.
Wakati tunaendelea kupambana na Uchumi wa kati.
Tujikumbushe tuliowahi kunusurika na Kifo.
Binafsi hii imenikuta mwaka juzi tu hapa. 2020.
Nilipata mualiko wa kwenda kwenye harusi ya ndugu yangu mtoto wa Mamkubwa wangu alikuwa akiolewa.
Binafsi siku hiyo sikuwa na ratiba yoyote ya kutoka lakini kwa sababu ni ndugu yangu na hilo alipingiki. Nilijiandaa kikamilifu. Na kufika eneno husika kwa shughuli hiyo. Hakukuwa mbali na napoishi, nilijongea mpaka eneo husika kwaajili ya kuifurahia shughuli ile. Ukumbuke hapo nilipokuwa nikiishi nilikuwa nimepanga hivyo hata wakati wa kuondoka niliondoka peke yangu.
Shughuli iliendelea kuwa bora na iliotaliwa na uchangamfu mpaka panapo majira ya saa nane usiku.
Wakati wa kuondoka sikuwa peke yangu nilikuwa na vijana wenzangu wengine tunaofahamiana na wote tulikutana eneo husika hii ilitufanya tusiwe na hofu kabisa. Sasa wakati tukiwa njiani kila mtu apate kuifikia nyumba anayoishi ilitubidi tugawane ili kila mtu aende zake kwa maana tulikuwa hatuishi pamoja.
Wakati nikiwa peke yangu huku yakiwa yametimia majira ya saa tisa usiku, nilifika hatua ambayo ni karibu na nyumbani nilichotakiwa kufanya ni kuvuka barabara iliotaliwa na kijigiza hafifu ili niweze kuingia ndani.
Hakika kwa hofu niliokuwa nayo kabla ya kuvuka barabara ilinibidi nitazame upande wa juu wa barabara hiyo kwa usalama wangu. Daah sikuamini macho yangu mtu nisiomfahamu alikuwa akija nilipo kwa kasi sana huku akionekana amedhamiria kunikamata. Nilianza timua mbio na kufanikiwa kufika sehemu ambayo najua nikijitosa navuka ukuta na kuingia nyumbani.
Kupitia kujitosa kule kwa kupanda ukute ule. Nilifanikiwa kuingia ndani ila wakati wa kushuka chini nilianguka vibaya sana. Nilikuja kushtuka ni majira ya saa kumi na moja nipo pale pale huku nikihisi maumivu makali kwenye kichwa changu.
Nyumbani nilifanikiwa kuwapa taarifa na huo ukawa mwisho wangu wa kutoka usiku.
Nawe tiririka na yako ndugu mwana JF. Ahsanteni pia.