Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Ibra Mgumia yule aliyesomaga Kitete primary school mwenye sauti nyembamba flani hivi au?

Amefariki Yule mshikaji? Kulikoni??
Wewe utakuwa na undungu na kijana alikuwa anaitwa Ibrahim Mgumia (Ibra), amefariki hivi karibuni. Alikuwa mwanajeshi, lakini baadae sijui ikawaje akarudi Mboka kwao.

Dr. Kisenge, kuweka record sawa hapo juu. Huyu Daktari alikuwa na Watoto karibu wote wa Kiume ambao walisumbua sana pale Uhazili. Mmoja wa mtoto wake ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo (Cardiovascular) hapo JK - Muhimbili.
 
Bundala na Kanyaboya walikuwepo Boyzia had 2005 kama ulipita T boys naamini story za Tukutuku utakua nazo nyingi sana
Ha ha ha ha nimepita hapo 2007/2009 Bundala alikuwepo, alikuwa anatufundisha soka, ha ha ha ha, mtaoga matusi hadi kesho!
 
Ni Majubwa sio Majugwa. Kimbembe kilikuwa hatari Sana miaka hiyo. Mimi ni Alumni wa Milambo wanaume pia wa kipindi cha Majubwa late 90's to early 2000's
Nimesoma huu uzi, umenikumbusha mbali sana. Majubwa alikuwa Head Master kipindi hicho. Nimekulia hiyo mitaa, marehemu mzee wangu Mwl Kwigeza akifundisha Milambo miaka hiyo.
 
Nani alikuwepo pia siku tuliyokwenda kwa mkuu wa shule kufanya fujo kilichotokea kwa kuku wake aliofuga bandani11? na tulivyokwenda kumwaga ki..esi T.G?

GO EAST,GO WEST,MILAMBO IS THE BEST...haya maandishi unayakuta juu ya ubao darasani..
Kwa mwalimu MAJUBWA au?
 
MILAMBO SHULE YANGU NAIPENDAAAAAAAAA
IKO TABORA MJINI,MKOANI TABORAAAAAAA
KANDA YA MAGHARIBIIIIIII
MOTTO WETU SIKU ZOTEEEE
ELIMU NI AMANA,PIA NI UFUNGUO
HULETA UFANISI
HAHAHAHAHAHAH Wimbo wa shule huo nimeusahau jamani ulikuwa unanisisimua sana enzi hizo aisee
 
Nakumbuka siku moja tulienda disco Tabora Girls sasa muda wa kurudi shuleni kwetu Milambo,tukarushiwa sana mawe njiani tukiwa kwenye lori la shule mpaka vioo vikapasuka vya pembeni.Tukafika mbele tukapaki tukajidiliana namna ya kuwashawishi wahuni ili waje turudishe majibu(maana tulienda wachache kulingana na mwaliko tuliopewa)Ikabidi mimi nishuke kwenye lori tulivyokaribia shule halafu wale waliobaki wakaenda kutangaza kwamba mimi nimetekwa(Maana nilikuwa popular pale shule).Asikwambie mtu MILAMBO walikuwa na umoja balaa,muda huohuo ikafunguliwa stoo ya majembe,makwanja na kila mtu akajipatia la kwake safari ikaanza kuelekea Tabora boys "kunikomboa mateka mimi" Ilikuwa noma walipewa kichapo na kuibiwa vitabu na madaftari yao kwenye maloka yao maana walifuatwa mpaka mabwenini kwao bila hata mlinzi wao kujua.Ile MILAMBO ndio maana ilikuwa inaitwa MEN SCHOOL aisee ilikuwa na vichwa hatari sana.
 
Nimesoma huu uzi, umenikumbusha mbali sana. Majubwa alikuwa Head Master kipindi hicho. Nimekulia hiyo mitaa, marehemu mzee wangu Mwl Kwigeza akifundisha Milambo miaka hiyo.
Wee! Mwl Kwigeza alifariki? Poleni sana mkuu! Mwl Kwigeza amenifundisha Chemistry form four pale Milambo. Alikuwa mwalimu mzuri sana hasa kwenye practicals na alinisaidia sana kwenye ufaulu wangu form four sitakaa nimsahau. Poleni sana aisee
 
Wee! Mwl Kwigeza alifariki? Poleni sana mkuu! Mwl Kwigeza amenifundisha Chemistry form four pale Milambo. Alikuwa mwalimu mzuri sana hasa kwenye practicals na alinisaidia sana kwenye ufaulu wangu form four sitakaa nimsahau. Poleni sana aisee
Asante sana, nami alinifundisha Chemistry hapo Milambo miaka hiyo ya early 2000s. Amefariki mwaka jana, mimi ni first born wake.
 
Back
Top Bottom