Tukumbushane vituko vya mafundi...

Tukumbushane vituko vya mafundi...

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
5,433
Reaction score
6,825
Wiki hii imeanza kwa kishindo sana , huyu Gawio yule maduhuli basi tafrani.....
Moderators kama kichwa cha habari nimekosea basi naomba kurekebishwa.

Katika haya maisha tunayoishi binadamu hua tunapitia mambo mengi sana,wengine tumejenga mazoea kwamba unakua na kila aina ya fundi katika mfumo wako maisha,

Leo naomba tukumbushane vituko vya mafundi iwe fundi mwashi, kinyozi, fundi nguo (cherehani) , fundi viatu , fundi simu ,fundi rangi n.k....

1. Fundi /kinyozi
Ushawahi kusikia msemo wa waswahili " fundi mkweli ni kinyozi tuu " naam hapa waswahili wanamaanisha kinyozi hua halali na deni hata siku moja, Binafsi baada ya kujenga mazoea na kinyozi mitaa ya home basi nilimkabidhi kichwa changu kabisa nikifika saloon nasinzia tuu juu ya kiti jamaa anafanya yake, ikawa baada ya wiki 2 tuu naenda saloon kupunguza nywele si wajua tena ukiwa na kipilipili na alinijulia hasa maana vichwa vyetu wengine vina mabonde basi nywele hapunguzi zote,
Mara vuu akapata safari ya mkoa, kilichokuja kutokea wale vinyozi wengine wote waligoma kuninyoa kisa nabagua nikienda pale[emoji28]

2. Fundi Mwashi/ujenzi
Aisee hawa watu heshima kwao, kama unataka kujenga jitahidi sana ujue hata kidogo mahesabu ya ujenzi yanaendaje , wengine si waaminifu hata kidogo...
Wale wa site kubwa sasa hawapendi kukosolewa , nakumbuka kuna kijana katoka chuoni kaja field/training, kijana kafika tuu site kaanza kubomoresha mafundi ukuta maana ulikua umepinda , mafundi walifura kwa hasira sana, siku kama 3 mbele wakamshauri kijana ashuke chini kukagua ukuta kama umenyoka, fundi aliangusha karai la zege pale alipo , zege vuu kwenye macho , kijana kapatwa na uoni hafifu tena macho hayaoni vizuri, fundi mwashi[emoji21]

3.Fundi cherehani/nguo
Kati ya mafundi ambao ni maarufu kwa kule kwetu uswahilini ni hawa jamaa maana wanagusa kote wanaume na wanawake , tena ukute fundi wa kiume anampima mwanamke basi shida kweli kweli mara atamgeuza kama samaki... mara amshike kiuno, mara paja , mara hips ilimradi tuu apate vipimo vyake anavyohitaji

Binafsi nawaheshimu sana hawa watu maana wanatufanya tujistri na kupendeza pia , Ilifikia kipindi nikajenga mazoea na fundi nguo mmoja tuu, kila nikipata nguo au kitambaa namfuata yeye, siku moja nimeingia karume nikaopoa kadeti moja matata sana, break ya kwanza kwa fundi akanichukua vipimo vyote, ajabu iliyoje suruali haikufaa tena kuvaliwa na pesa nishamlipa , siku ya pili kitambaa cha suruali ya shule baada ya kujichanga nikanunua kitambaa ili akishone, suruali ilinibana kuanzia mapaja mpaka miguuni haikufaa tena
Tukio la 3, Kuna rafiki yangu alikua anaoa hivyo akaniomba niwe mpambe wake , kutokana na majukumu ya kazi basi fundi alishauri aje kazini kwangu kunichukua vipimo ili ashone suti, nikaona poa tuu...
Siku ya pili tuu fundi nguo huyo yupo getini kibaruani kwangu ananichukua vipimo, fundi alikuja na mbwembwe kibao mara kuna watu maarufu kawashonea suti mara anataja majina fulani, fulani ,Mimi nikaona leo nimepata fundi[emoji119]....

Siku ya harusi imefika nimevaa suti mikono mipana mnoo, suruali ni bwanga ukitembea linarukaruka nikaona leo duuh[emoji58], nikajipa moyo Mimi si bwana harusi hivyo watu macho yote yatakua kwa bwana harusi, ajabu kuna wadada tena nawafahamu walinicheka sana kwa suti ile tena kicheko hasa nikavunga tuu macho makavu sina haya wala soni , nikaonekana mzee, sijui kuvaa, sio modern guy ,old fashion...
Baada ya kuisha harusi ile suti sijavaa tena ipo kabatini miaka 2 sasa[emoji21]...

Kwahiyo kama una kituko au vituko vyovyote basi share hapa
Nawasilisha....
 
Hapa mtaani kwetu kuna fundi nguo n bonge la msahaulifu, yan anakupima bega akija kwenye kifua au achukue daftar aandke ashasahau vipimo vya bega, yan akipma inabd wewe ndo ukariri la sivyo utashonewa shati kama la Marehemu Pepekale kama si le mutuz
 
Jamaa anakuja SAA kumi mafundi washa nawa ila hela anatoa SAA moja au SAA mbili usiku muda mwingi ana onekana kuongea na simu. Mara apande juu golofani ashuke Ndio atoe hela.siku ya sikukuu watu wana taka hella ana lipa saa saba wakati alipaswa kulipa siku mbili kabla. na cite kuiba ilikuwa msala. Watu wakatia sabuni kwenye maji kesho yake zege akishika linapukutika tu.
 
Back
Top Bottom