Tukumbushane vituko vya COVID - 19

jerrybanks

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
3,544
2,000
Leo nmejikuta nacheka mwenyewe.

Nakumbuka nilikuwa najisomea mwenyewe humu humu kuhusu Covid 19 wakat huo ikiwa iko China na kuhesabia ni gonjwa la wenzetu tu kwetu halitofika.

Ghafla siku isiyokuwa na jina ndo mgonjwa wa kwanza akatangazwa hali ikaanza kuwa tete watu full kuvaa mabarakoa. Mimi kiukweli zilinishinda na nkasema kuwa kamwe sitokuja kwenda quarantine ila Mungu akanambia mimi ndo mpangaji siyo wewe.

Nikiwa hospital moja ya Aga Khan bwana wakati naenda kupima vipimo nikawa naskia kuwa kuna semina ya manesi mle kwa ajili ya jinsi ya kujikinga na Corona na jinsi ya kuhudumia wagonjwa wa Covid 19, basi nikafanya kila njia na mimi nikaingia kumbe jana yake kuna mgonjwa walimgundua ana Corona Serikali ikamfuata then wakaambiwa wauguzi wote waliomhudumia yule mgonjwa wa Corona watafanyiwa semina.

Basi na mimi kufosi fosi ile nikawa mmoja wapo, walikuwa wauguzi wote, kumbe ilikuwa danganya toto kilichofata hapo wote nikiwemo na mimi kupelekwa quarantine.

Asikwambie mtu hakuna kitu kinachoweza kumuua binadamu kama hofu. Nashukuru Mungu wote tulipona na kuruhusiwa kurudi nyumbani japo wengi walikuwa hawana.

Baada ya kurudi nyumbani ndani ya week 2, nikaanza dalili zote za Corona kwenda kupima nikakutwa nina corona hivyo nikawekwa quarantine nyumbani kwangu nashukuru Mungu kwa kunipa mke mwenye nguvu ambae mbali na hofu zote za wakati huo kuhusu corona lakini alikuwa akinilisha na kulala na mimi nyumba na chumba kimoja ndani ya shuka moja hali ya kuwa ndugu zangu tu walikuwa wananikimbia.

Mtu wa mwisho ni bosi wangu ambae kila tukionana lazima acheke sana maana leo nimeenda kupima nikakutwa na corona jana yake nilishinda nae kutwa nzima baada ya kumwambia bosi nina corona kwenye simu alilia sana nakumbuka kauli yake moja tu "Jerry umeniua jerry nimekufa mimi"

Tupeane vituko vya Corona kwa upande wako
 

Marrryline

Member
Mar 27, 2019
89
150
Acha kabisa Mkuu niliumwa wiki mbili sitoki nje Yaani unajua maana Yakuumwa ikifika jioni mwili unachemka nikaishia kunywa tangawiz kujifukiza hospitali sijakanyaga hata nilikuwa naogoooopa balaa nilihis Covid lkn mbona alliyekuwa ananiuguza hakuumwa hata kichwa,mwisho nilipona vizuri tu.kiukweli kabisa Hiko kipindi sitaki hata kukumbuka ila Mungu mkubwa sana jamani.
 

jerrybanks

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
3,544
2,000
Acha kabisa Mkuu niliumwa wiki mbili sitoki nje Yaani unajua maana Yakuumwa ikifika jioni mwili unachemka nikaishia kunywa tangawiz kujifukiza hospitali sijakanyaga hata nilikuwa naogoooopa balaa nilihis Covid lkn mbona alliyekuwa ananiuguza hakuumwa hata kichwa,mwisho nilipona vizuri tu.kiukweli kabisa Hiko kipindi sitaki hata kukumbuka ila Mungu mkubwa sana jamani
Mie hospitali niligoma kabisa kwenda nikasema bora nifie nyumbani maana ilikuwa kwenda hospital ni kama kufata tiket ya kifo.
 

Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
3,876
2,000
Nakumbuka wakati korona imekolea nikaibuka kijijini kuwasabahi wazee. watu wakawa wananishangaa. kumbe huko waliambiana hii ngoma ni kimjinimjini zaidi, hivyo kulikuwa na kauoga. nashukuru nilisalimia na kurudi sa;lama.
 

rr3

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,910
2,000
Bwana bwana.

Acha mchezo na hofu, ishu ilivyochanganya nilipata kitripu cha Mombo basi nikaenda nikakaa wiki moja.

Ile kurudi hali si hali, kubanwa kifua , baridi n.k....... Acha ninywe malimao , tangawizi na kitunguu saumu .... Sikuwahi kujua kuwa malimao ukiyasaga na maganda na mbegu zake yanapita kooni.....yalipita.

Nilikuwa na gogo nne za grevilia nilipanga kumpa mtu apasue, nikachana mwenyewe ndani ya wiki...... Mchakamchaka, kichura push-up s........ Mtu ukifikiria kufa unaogopa sana.

Lakini hata hivyo vijana naona wanashukuru kuwa huu mchanganyiko wa malimao, tangawizi na vitunguu saumu umerudisha kwa kiasi chake heshima ya ndoa as kitandani performance imepanda kidogo.
 

Ulweso

JF-Expert Member
May 24, 2016
18,529
2,000
Ulikimbilia posho haaa haaa quarantine haaa haaa , siku mtu wakwanza kupatikana nilikuwa hosp basi wafanyakazi waliingia mule kwa Dr wote wamevaa barakoa mie na Dr tukabaki tunawashangaa vipi jamani? Eti tayari duu nilipopata tiba ni nyumbani moja kwa moja , mtu wangu alikuwa na bidii na na malimao vitunguu Swaumu jamani tulikunywa kwa lazima
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom