Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Mister T ( r.i.p )
mr-t.jpeg


Mr.-T.jpg

Ndani ya Dtv
 
Katika matangazo nilokuwa nayapenda moja wapo la revola.
'Tueleze siri ya mafanikio,
Sio siri, ni revola,
Revola pekeyake?
Ndio, kwani marashi yake ni tulivu na huniweka fresh mchana kutwaa.
Yalikuwa kama matatu tofauti, ila me nilikuwa nalipenda la yule mdada alokuwa anafanya mazoezi, ile lafudhi yake ilikuwa tamu na mbwembww zake.
Jengine la maji ya kilimanjaro.
'Maji safi kilimanjaroooo'
Tangazo la colgate la watoto, na tangazo la fanta la watoto pia.
Tamthilia nilokuwa naipenda ni Acapulco bay.

Kwani marashi yake ni tulivu na huniweka fresh, mchana kutwa. Alafu anatoa tabasamu moja lainiii na nyororo mithili ya sufi hadi leo nalikumbukaaaa
 
Tamthiliya ya haina na hasani ya wakenya ilikua inaoneshwa itv wakapotea msituni wakawa wanatafutwa utoto nilikua najua kweli
 
Kuna tamthilia ilikuwa inaitwa SUNSET BEACH balaaa saaana mpaka shule kwetu enzi hizo Forodhani ya kina Munira,Hemed Kavu,Hamisi Makaveli ilikuwa moto.....tukapatunga sehemu karibu na geti etiii SUNSET BEACH

Kuna dada mmoja alikuwa anaitwa Fina ana figure namba 8 hadi leo cjaona mfano wake
 
Dah aisee hizo memories zimenibamba kinyama.Enzi Mr.T na the A Team.Love thy neighbour ile tamthiria kijamaa kina upara kinaruka kamba na watoto.Police Academy.

Miziki ya west Africa kina Yossou Ndou,Angelica kidjo.

Kuna the roots ya kina kunta kinte.

Kale katoto kaliimba "Tanzania eeh nakupenda... alichanganya na kijapan.

Football enzi za kina babayalo,uche ukochuku hiyo Atlanta olympic 1996.pia enzi za kina Mc Fish yaani nilikuwa nimebandika stickers zao nyuma ya mlango.

Bafana bafana 96 hio nadhani, Mac Fish, Dr Khumalo, Ladebe
 
Tamthilia ya The passion, nmemkumbuka timmy, bibi mchawi tabitha, kay, miguel, simone
Pia The crow


Mr julian crane na mkewe ivy(ivy alizaa nje ya ndoa mtoto aliyeitwa ethan crane) ethan na gwen baadae akamuoa theresa,Whitney na simon watoto wa doctor Russell (eve), chad mtoto wa julian na dct Russell, tabitha na tim, charity, kay, sam, sheridan na luis, pastor kipofu, pawler mama yao (luis, theresa, david na miguel) mrs hotchkis mama yke gwen, dah, ilikuwa hatari sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom