Maisha ya sasa ya Dar es salaam na ya zamani.

Tomahawk

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
232
217
Dar es salaam ni mji unaokuwa kwa kasi mno katika bara la Africa.
Katika pilika pilika za maisha mji wa Dar es salaam upokea wageni wengi pengine kuliko jiji lolote hapa Tanzania.
Miaka ya 2000, Jiji la Dar es salaam lilikuwa na idadi ndogo ya watu isiyozidi hata million tano naimani kwa sasa jiji ili lina watu zaidi ya million tano.
Hapa najaribu kukumbuka baadhi ya mambo ambayo nayakumbuka mno miaka iyo ya nyuma.
Television maarufu ya wakati uo ilikuwa ni ITV na ilikuwa na vipindi vizuri na vya kuvutia, hata matangazo yake ya biashara yalikuwa ni ya kuvutia mno kwa mfano Tangazo la sabuni ya revola, sweet heart lotion na binafsi matangazo yaliyokuwa yakinivutia zaidi ni ya sigara aina ya sweet menthol (SM) na la Air Tanzania.
Wakati uo hakukuwa na foleni kama ilivyo sasa nilikuwa naishi kimara wakati shule niliyokuwa nasoma ilikuwa iko mbagala, sikuwa napata sana changamoto ya usafiri kwakuwa hakukuwa na foleni wala watu hawakuwa wakijazana kwenye mabus ya usafiri kama ilivyo sasa.
Nauli kwa wanafunzi ilikuwa kwanza tsh 25 ikaja 30 na baadae tsh 50.
Kulikuwa na bus la UDA mfano ya mwendo kasi wa sasa lililokuwa likifanya safari ya mbagala kuelekea kivukoni lilikuwa refu na tulikuwa tukiliita sisi wanafunzi kama bus train na wala halikuwa na ubaguzi unapanda na unakaa kwenye siti bila kubughuziwa ivyo wanafunzi wengi tulilipenda ilo bus, kwa kizazi kile hatushangai mwendo kasi kwakuwa tulishalipanda sana.
Television ya vijana ilijulikana kama ITV 2 ambayo kwa sasa ni EATV.
Bongo flavour ndo ilikuwa kwenye peak kwenye miaka ya 1999 na 2000.
Billicanas ndo ilikuwa club pekee ya music ivyo kwa sisi wakazi wa kimara ilitupasa kusafiri umbali mrefu kwenda Club iyo iliyokuwa katikati ya jiji kwakuwa hakukuwa na club nyingine maarufu hapa jijini, ivyo bila usafiri inakuwia vigumu kwenda club bilicanas.
Starlet ndo zilikuwa gari maarufu za vijana kwa wakati uo.
Nakumbuka miaka ya 2000 zikajaga izi offices za kuitwa internet cafe, binafsi nili isi ndani ya izi offices wanauza chai na kahawa kwakuwa zilikuwa na jina la cafe.
Na internet ndo ikawa maarufu kwa sisi watoto wa shule wa wakati uo ivyo mchezo wa kufungua email ndo ulikuwa ujanja wenyewe kama hauna email basi waonekana mshamba tuuu, na tukienda internet cafe mda wote unaolipia ni kuangalia porno tu.
Mimi binafsi nilikuwa natumia umbali mrefu kufuata internet cafe, nilikuwa natoka kimara mpaka pale kitega uchumi, kulikuwa na internet pale sikumbuki ghorofa ya ngapi vile au nakwenda sea boys internet cafe pale magomeni au opposite na sea boys kulikuwa na cafe nyingine ikiitwa virus cyber cafe, kwakweli technology ilinitesa kuitafuta ila sikuchoka kwakuwa nilikuwa naipenda.
Maisha yalikuwa ya utulivu bila mvulugano.
Vipindi maarufu vya tv kwa wakati uo ni Days of our lives (CTN), Mambo ayo na Tausi (ITV) izo unaoga mapema ili uwahi kiti cha mbele usawa wa tv uone vizuri.
Magari maarufu kwa kipindi icho yalikuwa ni Toyota chaser, vitara, surf na starlet kwa vijana.
Shule maarufu za secondary wakati uo zilikuwa Makongo, Jitegemehe, st anthony na kwa kimara kulikuwa na Midland, st peter na Moa maeneo ya kimara suca.
ITAENDELEA.........
 
kuhusu mabasi ya UDA hapo umetikisa macho haya maicarus yalikwepo miaka ya 8o na mwanzoni mwa miaka ya 90 ila miaka ya 70 kulikuwa na mabasi ya ghorofa mekundu moja bado lipo pale udsm estate office
 
Back
Top Bottom