Tukumbushane mboga, matunda, vyakula na mapishi ya asili

Mwanza kuna mbute, mapalage, michembe, matobolwa na samaki kibao kama fulu, chengu, sato nghuyu, nembe, gogogo, ningu, kamongo nk
 
Iwe bojo,kuna kinywaji kinaitwa Omuramba,kuna chakura kinapikwa na kufungwa kitaalam kinaitwa Eibowa,kuna tundizi tutamu saaana tunaitwa Akanana,funga kazi ni pale mchumba anapokuzawadia Ensenene...nikiwa mjini haya yote nayamiss
 
Iringa kuna majani ya maboga unachanga na maua yake then unaunga na mbegu za bangi zilizo twangwa , na ugali wa kivelege na kuku wa kuchoma. Kinywaji komon mkangafu, ulanzi na togwa. Matunda kuna mapinigesi, mafyox, sasati, mapeasi dah!
 
Kwa kina Mura kure Tarime na Serengeti kuna ugari na vimoro, weee acha tu!
 
ukija pale moshi kuna vyakula kama kiburu,ng'ande,kitalolo ni balaa,kuna matunda kama kweme na viazi vikuu..dah home sweet home..
We Mushi tangu lini kweme zikawa matunda???Nwy umesahau mtori..machalari..kisusio...ugali wa ndizi...perege...miwa...zambarau...elimu...mbege...nzuga...
 
umenikumbusha Kule tabora kuna Mlenda, kihembe cha nsili, uyoga(bhobha), matobolwa, masangu ga mhande, dengu,
mzabagulwa, msosolwa, matembele, nswa, nsansa, mzubho na vingine vingi, bila kusahau maziwa, asali na viazi.
 
umenikumbusha Kule tabora kuna Mlenda, kihembe cha nsili, uyoga(bhobha), matobolwa, masangu ga mhande, dengu,
mzabagulwa, msosolwa, matembele, nswa, nsansa, mzubho na vingine vingi, bila kusahau maziwa, asali na viazi.
Nsansa, nswalu na matunda kama ntalali, ndanti, mantonga, makebhe oooh ...NOWORA
 
Kwetu Kiomboi,

kuna,

furu, sisai, zambarao, matunda ya nyani, kambare, kamongo, mbiluli, mabuyu, korosho, kau na bila ya kuisahau togwa
 
Jana Bujibuji kasema eti kijijini kwao huwa wanakula ugali kwa madafu.
 
Manyara kwa wa Iraqiw
kuna dansai, ugali mlaini unaitwa ugali
wa qwantai, pombe kama manguree na busa na wanzukia etc ..
 
Back
Top Bottom