Mambo ya kuishi na masela ni ya kijinga sana.
Kuna jamaa wawili niliwahifadhi ghetto kwangu kwa kama miezi 6 hivi, Wanakula, vyombo vinakaa hata wiki hawaoshi hadi nioshe mimi, Ndani vumbi linajaa, michanga wanakaa tu, hamna wa kujishughulisha nna Usafi isipokuwa mimi. Ilikua inanikera sana.
Watu wanabeba Viepe wanakula wanaacha mifuko na makaratasi juu ya meza, maganda ya ndizi.
Nilivumilia nikashindwa, siku moja nikawatolea uvivu, ila nikaonekana nawanyanyasa na kuwababaisha kisa wanaishi kwangu. Nikawaambia kama hawawezi kubadilika wasepe, Baada ya muda Wakasepa. Hivi sasa naishi mwenyewe mambo safi.