Tukumbushane haya..

Hicho kibatari nilikitumia sana ila tatizo lake ni kamasi jeusiiii asubuhi. Dah! Umenikumbusha mbali sana ila kiliniwezesha kupaa O level
 
Hizo taa zimetusevu sana enzi hizo, ila nilikuwa nachukia process za kutoa utambi ukitumbukia kwenye chemli au kibatali.
 
Hiyo taa ya chemli nikiangaliaga hapo kwenye unapotokezea utambi dah..huwa nawaza sana vitu vya kiutuuzima
 
Enzi za "maaaafuuuta ya taaaaaaa" kipindi cha ubrazamen wetu
 
vijana wa kanda maalum haya sio mabomu tasavali
 
Umenikumbusha mbali sana, taa ya chemli nimesoma nayo shule ya msingi mpaka nimeingia University. Nakumbuka nikiwa secondary mambo ya msuli tembo kusoma mpaka usiku wa manane, siku moja mama akaniambia taa ya chemli ikipata moto ukigusa na maji inapasuka basi mm usiku hivi kwenye saa 6 nikiwa nasoma nikaamua kufanya jaribio. nikaweka kidole mdomoni nikagusa taa nikasika paaah taa imepasuka alafu ndo hiyo hiyo inategemewa aisee. Wachaaa kabisa sad enough mama aliyenipigania nikapata elimu hajafahidi hata matunda ya elimu ya mwanae kifo hichi jamani.....!
 
Pole sana.
 
pole sana mkuu, apumzike mahali pema bi mkubwa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…