Tukumbushane ENZI ZA MDUNDIKO

Tukumbushane ENZI ZA MDUNDIKO

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,036
Reaction score
168,673
Enzi hizo mdundiko ukipita hata mtaa wa sita utalikisia tu timbili lake.
Mama anaacha sufuria jikoni anajitosa kwenye mdundiko.
Baba alikuwa chooni anakata gogo , kutokana na utamu wa mdundiko anatoka nduki kuufuata mdundiklo huku suari ikiwa magotini na mkononi ana kata ya kuchambia.
Watoto ndio usiseme, ukija kushtuka uko Gongo la Mboto wakati kwenu Tegeta.
Jamani mdundiko ulikuwa una raha yake. Nimezimiss sana zile zama za magoma moto ya MDUNDIKO
 
...huu ni utamaduni wa Wazaramo!
Kwetu kanda ya ziwa...
Tujuze mlivyo kuwa mnafanya wakati huo...
 
  • Thanks
Reactions: amu
Last edited by a moderator:
...huu ni utamaduni wa Wazaramo!
Kwetu kanda ya ziwa...
Tujuze mlivyo kuwa mnafanya wakati huo...

hapo ndo naposhindwaga nitawezaje kuishi huko wakati nimeshazoa mdundiko mieeeeeeeeeeeeeeeee
 
...huu ni utamaduni wa Wazaramo!
Kwetu kanda ya ziwa...
Tujuze mlivyo kuwa mnafanya wakati huo...

Kule ni mwendo wa kucheza mbina.
Mkivuna tu kila siku jioni vikundi mbalimbali hushindana kucheza ngoma na kushindana madawa
 
Last edited by a moderator:
Enzi hizo mdundiko ukipita hata mtaa wa sita utalikisia tu timbili lake.
Mama anaacha sufuria jikoni anajitosa kwenye mdundiko.
Baba alikuwa chooni anakata gogo , kutokana na utamu wa mdundiko anatoka nduki kuufuata mdundiklo huku suari ikiwa magotini na mkononi ana kata ya kuchambia.
Watoto ndio usiseme, ukija kushtuka uko Gongo la Mboto wakati kwenu Tegeta.
Jamani mdundiko ulikuwa una raha yake. Nimezimiss sana zile zama za magoma moto ya MDUNDIKO

teh teh teh Bujibuji umeniacha hoi
 
daaaa mdundiko bhana uwakute wale wanaojua kuzungusha nyonga hasa huku kwetu lindi weeeeee
 
hahahahahahaha Bujibuji me mbona nipo? alaf mdundiko hupo hadi leo huku kwetu lindi kila j.tano hapa kosi mdundiko.
mwambie amu akualike yeye ni mtaalamu wa kupiga ngoma na kucheza viduku.

yeye anakaa tegeta sijui boko mdundiko atausikia wapi jamaniii?
aje huku kwetu aone wapi tunavyoburudika tukikupongeza ukiolewa lazima tukuletee na mdundiko, tukikualika shughuli lazima tuutembeze mdundiko nyumba hadi nyumba tukigombana na kufuta urafiki lazima nikuletee mmdundiko nikukuomba umama wa hiyariii lazima nikuletee mdundiko usiombe unichimbe maana nitakuchamba kwa matarumbeta
 
hahahahahaha alaf wake za watu wanatoroka nyumba zao wana kimbilia mdundiko alaf kinacho nishangaza watu huwa hawachoki.
 
...huu ni utamaduni wa Wazaramo!
Kwetu kanda ya ziwa...
Tujuze mlivyo kuwa mnafanya wakati huo...

Lemie lemie punguza. dududududu dududu dududududu wa x2 he e he e dududududu dududu dududududu wa, nakabombonya wa
 
hahahahahaha alaf wake za watu wanatoroka nyumba zao wana kimbilia mdundiko alaf kinacho nishangaza watu huwa hawachoki.
full kuunguza mboga na watoto kupotea.
Nakumbuka nliunguza maharage kisa kuusindikiza mdundiko kupeleka sanduku weeee nlichezeaje kichapo nliporudi home
Tulivyokuwa wadogo mdundiko ukipita tunafungiwa ili tusipotee
cc: Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Binafsi enzi hizo miaka ya 1997 nilikuwa tunaishi vingunguti na mdundko ulinifanya nkapotea na kupatikana jioni kabisa.
 
full kuunguza mboga na watoto kupotea.
Nakumbuka nliunguza maharage kisa kuusindikiza mdundiko kupeleka sanduku weeee nlichezeaje kichapo nliporudi home
Tulivyokuwa wadogo mdundiko ukipita tunafungiwa ili tusipotee
cc: Mtambuzi

hahahahahahaha inabidi umpe shule Bujibuji kila nikiona mdundiko naangalia kama nitakuona hhahahahaha
 
Last edited by a moderator:
Wapiga ngoma wa mdundiko wamegegeda sana dada zetu.
Yaani ile ngoma kama ina uchawi vile.
Binti anamkataa afisa wa BOT anataka mpiga ngoma wake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom