Obimbo
Member
- Nov 17, 2020
- 35
- 36
Amani ya Bwana iwe nanyi,
Tunamshukuru Muumba kwani nchi yetu imejaaliwa kuwa na mito mingi mikubwa kwa midogo, ile ya msimu na isiyo ya msimu. Mito hii licha ya kupendezesha sura ya nchi imeleta pia changamoto za usafiri tokea upande mmoja kwenda upande mwingine.
Nilipokuwa kijana mdogo nlikuwa nikuvutiwa kusikiliza sana story. Ndipo siku moja mama yangu alinisimulia walivyokuwa wakienda shule kwa mabasi ya serikali, hakusita kuniambia adha ya Usafiri hasa kuvuka mto Mara kwa Panton kwani alikua akitokea Tarime kwenda shuleni kwao Weruweru.
Ikumbukwe kuwa eneo hilo ni mahali ambapo mto hukutana na ziwa hivo kasi ya maji inakuwa kubwa, hivyo iliwalazimu manahodha wa Panton kuwa makini japo changamoto hazikuisha, kunanyakati nyingine malori kwa mabasi yalitumbukia katika eneo lile na kupelekea upotevu wa mali pamoja na ndugu zetu.
Kama eneo lile lionekanavyo limezungukwa kwa matete mengi hivo samaki hupenda kuzaliana maeneo hayo vile vile na majoka makubwa pia hayakosi kwani hujipatia kitoweo chao katika mazingira hayo. Siku moja wakiwa tayar wameshaingia ndani ya Panton na nahodha akiwa anajiandaa kukivusha chombo ghafla joka kubwa lilitokea katika matete na kuelekea kuingia katika Panton, taharuki ilikuwa kubwa ilopelekea watu kutaka kujirusha majini lakini kwa namna ya ajabu Muumba aliwaokoa watu wake kwani joka lile lilikaa pale kwa muda na Kisha kurudi majini lenyewe.
Karibu tupeane visa katika kuvuka mito korofi