Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,218
- 10,729
Kwenye pita pita zangu katika makarasi ya mzee nikakutana na hili tangazo, tangazo za sigara ambazo sikufahamu kuwa zilikuwa ni sehemu kubwa ya maisha ya watu enzi hizo.
Kwa wale wahenga nadhani wanafahamu na walipata uhondo wa sinema za bure katika viwanja mbalimbali huku wakiweka kila siku filamu mpya karibu mwezi mzima. Ni tangazo ambalo nyakati hizo lilitosha kuwafanya watu wawe wavuta sigara haswa.
Nimepata kuwauliza watu walidai kuwa tangazo hili liliambatana na wimbo ambao ulikuwa ukitia nakshi haswa, Wimbo unaimba sigara maalumu kwa kukuburudisha vuta sportsman! basi katika watu 10 lazma watu 6 watakuwa wavutaji.
Wapo wazee ambao miaka hiyo walivyokuwa vijana walikariri kuwa tarehe 10 ndo siku ya tukio. Hivyo kila tarehe 10 ya mwezi ilikuwa siku ya EAST AFRICA FACTUAL CINEMA.
Kabla ya kuitwa Portsman basi mwanzo watu walivuta sana Sportsman ama kwa kifupi Sports na kitu mbaya wakati huo ilikuwa ni nadra kukutana na lile onyo la:
UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO.