‘Tukope kwa ajili ya maendeleo’

‘Tukope kwa ajili ya maendeleo’

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
MHADHIRI Mwanadamizi mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azavery Lwaitama, ameeleza kushangazwa na mzigo mkubwa wadeni la taifa, akisema kuwa kwa kuendelea kukopa bila kufanya mambo ya maendeleo kutaifanya nchi kuwa mtumwa.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu juzi, Lwaitama alisema endapo nchi inazidisha kukopa itakuwa mtumwa kwa hao wanaodai na matokeo yake wataingia nchini na kuhodhi rasilimali za Watanzania.
Dk. Lwaitama alisema kuwa lingekuwa jambo zuri kama fedha hizo zinakopwa halafu zinaimarisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara na reli lakini zilizopo kwa sasa si za kutegemea kufanya hayo.
“Nakumbuka kuna wakati mmoja katika utawala wa Rais Mkapa deni hili lilikuwa mzigo na tuliingia kwenye matatizo na matokeo yake tukasamehewa hii ni hatari sana.
“Lakini bila kuwa na woga tunatakiwa kujihakikishia kuwa hizo fedha zinatumika kiusahihi au zinatumika kwa njia ya ufisaidi?” alihoji.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, deni la taifa linazidi kuongezeka kwa asilimia 38 kutoka sh trilioni 10.5 mwaka 2009 /2010 hadi sh trilioni 14.4 mwaka 2010\2011.
Hadi Juni 30 mwaka 2012, deni hilo limefikia sh trilioni 16.9 ukilinganisha na mwaka 2011 ambapo lilikuwa sh trilioni 14.4.
Katika deni la sh trilioni 16 kiasi cha sh trilioni 12, sawa na asilimia 73 ni deni la nje na ndani ni sh trilioni 4.5 sawa na asilimia 27.

CHANZO: TANZANIA DAIMA
 
Back
Top Bottom