Tuko tayari kuingia uchaguzi 2015 bila katiba mpya?

Nimechoka kumsema vibaya JK. Mwache apumzike salama. Najua nia yako. Na hatumshambulii ng'o. Kwanza hata yeye mwenyewe akiongezewa hata wiki moja baada ya muda wake kwisha ( kama atafanikiwa kumaliza miaka minne iliyobaki salama) hataki kabisa huo ujinga wenu mnaouita urais.

hahahaa,if u cant beat him, then....!!
 
Muheshimiwa Raisi Dk.Kikwete kuongezewa muda Wa uraisi ,ili amalizie maswala ya katiba mpya kwa urahisi,pia na kutuwezesha watanzania kuelewa maana ya katiba na umuhimu wake.

isitoshe magamba yatakuwa yemevuliwa yote,na pia kusimamia magamba mapya yakichipua vizuri.

Raisi wa marekani aliwahi kuongeza muda wa kuwa madarakani ,Franklin Roosevelt .1933 to 1945 . source: Franklin D. Roosevelt - Wikipedia, the free encyclopedia
tunajua USA ndio nchi inayojitangazia uimwenguni kuwa na Demokrasia,na isitoshe Dk.Jakaya kikwete ni Friends of USA,so haitakuwa mbaya akiongezewa muda,hiyo pia ni sehemu ya Demokrasia

natimiza haki yangu kikatiba ,kwa kutoa maoni bila kuvunja sheria

Kikwete kuongezewa muda?? dhubutu, sasa hivi anaomba muda wake wa urais uishe haraka yasije yakamkuta ya Misri halafu wewe unasema kuongezewa muda!!!
 
Akitaka tutamuongeza ili tukome. Kwani bado hatujatosheka na haka tulikokapata. Ila mimi simo nyie mpeni kwa vile hakuna watu wenye uwezo au?
 
Muheshimiwa Raisi Dk.Kikwete kuongezewa muda Wa uraisi ,ili amalizie maswala ya katiba mpya kwa urahisi,pia na kutuwezesha watanzania kuelewa maana ya katiba na umuhimu wake.

isitoshe magamba yatakuwa yemevuliwa yote,na pia kusimamia magamba mapya yakichipua vizuri.

Raisi wa marekani aliwahi kuongeza muda wa kuwa madarakani ,Franklin Roosevelt .1933 to 1945 . source: Franklin D. Roosevelt - Wikipedia, the free encyclopedia
tunajua USA ndio nchi inayojitangazia uimwenguni kuwa na Demokrasia,na isitoshe Dk.Jakaya kikwete ni Friends of USA,so haitakuwa mbaya akiongezewa muda,hiyo pia ni sehemu ya Demokrasia

natimiza haki yangu kikatiba ,kwa kutoa maoni bila kuvunja sheria

Wala hahitaji muda zaidi

Amefanya mengi kwa muda tunamshukuru

Atastaafu timely..ccm hatuna utamadun huo mkuu usiwe na hofu...

Haya mambo watafanya kina Lyatonga na Slaa siyo CCM..no chance
 
Awamu ya kwanza alipokuwa anazindua kampeni pale jangwani alianguka!
Awamu ya pili nayo akaanguka!
Sasa mdau unamuombea heri kweli wewe?! Wewe unafikiri akiongeza awamu ya tatu nini KItatokea Jangwani?????????????????
 
Neno Tanzania toka lianze kutumika alijatimiza miaka 48, hiyo 50 inatoka wapi?
 
kama nani aongezewe muda????? lakini unaweza muongezea kichwani mwako!!! akutawale mwenyewe
 
Binafsi sipo tayari kuona madudu ya NEC and the likes, madudu ni mengi mno yanayoruhusu unfair competetion, ni bora muda wa uchaguzi ukasogezwa mbele ili nchi tuweze kupata katiba mpya. Mwamko ni mkubwa mno kwa watanzania kushiriki katika chaguzi zozote zile, isipokuwa system ya uendeshaji imejaa ualakini mwingi ambapo hata mtoto mdogo anajua. Chukulia wakuu wa wilaya, mikoa achilia mbali wenyeviti wa vitongoji! utakuta hawa wote kama ni chama fulani wanakuwa hawako tayari kuona wanafanya kile wanachotakiwa hata kama kinaumiza chama chao!
 
Kufanya uchaguzi 2015 bila katiba mpya ni kukubali kuendeleza matatizo yaliyopelekea ulazima wa kutaka katiba mpya. Kusogeza uchaguzi mbele ni suala la kikatiba na tukifika hapo itaangaliwa katiba ilipo sasa ambapo suala hilo litakuwa uvunjifu wa katiba.

Kama itabidi kusogeza mbele uchaguzi mkuu ili kutoa muda zaidi kupata katiba mpya madhubuti basi itapasa kulipeleka suala hilo bungeni ambako nina hofu kufanikiwa kwake.

Tujenge imani na tujitokeze kwa wingi kutoa maoni ya marekebisho ya katiba ili kuhakikisha haitakuwa ni kanzu ile ile chakavu iliyoshonewa viraka bali tuwe tumeshona kanzu mpya itakayo tusitiri vyema 2015 na kwa kipindi kirefu kwa maslahi ya wananchi wote.
 
kama mnasoma alama za nyakati kwa muundo wa bunge la katiba na kwa fukuto lililopo huku visiwani la kutaka mamlaka kamili hatutaweza kupenya kwenye kura ya maoni kirahisi labda nasema tena labda lisitumike daftari la kupiga kura na mbadala wake vitambulisho vtumike kura ziongezwe kwenye makambi ya jeshi na tume ichakachue matokeo huku znz ndo tunaweza kupenya.
 
Nchi hii inaweza kuendeshwa bila ya kuwa hata na Katiba. Tumeambiwa kuwa watu wengi sana hawajaisoma au kuiona Katiba ya sasa; kwa maana hiyo chombo chochote kikiifinyanga Katiba, hakuna mtu ambaye anaweza kuhoji! Tulishazoea kuwa na Katiba yenye viraka kuanzia Uhuru.
 
Mwisho wa kikwete ni 2015 hizo sababu mnazojenga hazimsaidii yeye na ccm 2015 they must go with their ccm.hata kama katiba haitakamilika kuunda tume huru ya uchaguzi hakutupishida.
 
Tume huru ya uchaguzi itaunda na uchaguzi utafanyika.mkataba wa kikwete ni miaka 5 tu.zaidi ya hapo hapana
 
kama mnasoma alama za nyakati kwa muundo wa bunge la katiba na kwa fukuto lililopo huku visiwani la kutaka mamlaka kamili hatutaweza kupenya kwenye kura ya maoni kirahisi labda nasema tena labda lisitumike daftari la kupiga kura na mbadala wake vitambulisho vtumike kura ziongezwe kwenye makambi ya jeshi na tume ichakachue matokeo huku znz ndo tunaweza kupenya.

Katiba mpya inawezekana tu CCM itakapotoka ikulu
 
Tunaandika katiba mpya sababu kuu ikiwa kwamba iliyopo ina viraka vingi, Iwapo tumefika 2015 na haijakamilika, Tutaweka kiraka kingine cha kuruhusu tume huru ya uchaguzi? au tutakubali kuingia uchaguzi 2015 kwa katiba hii hii yenye kutambua Tume ya uchaguzi iliyo chini ya Rais? Lipi gumu lisiloeleweka hapo ndugu zangu!
 
Back
Top Bottom