Tuko tayari kuingia uchaguzi 2015 bila katiba mpya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuko tayari kuingia uchaguzi 2015 bila katiba mpya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ndamo emmanuel, Mar 1, 2011.

 1. n

  ndamo emmanuel Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 12, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu nina hakika zaidi ya 500%, kuwa katiba tunayoitaka Wananchi haiwezi kukamilika haraka, kama Ratiba ilivyo sasa kuwa kufikia 2014 tuwe tumepata katiba mpya!

  Kukimbizwa mbio mbio mchakato huu kutaacha masuala muhimu ya Msingi ya wananchi kuingia kwenye katiba, hivyo kulazimika kuweka viraka elfu kidogo mara tu tupatapo hiyo katiba mpya 2014.

  Kwa maoni yangu, Mwanasiasa yeyote atakayeunga mkono marekebisho ya katiba hii iliyopo ili kuruhusu Tume huru ya Uchaguzi pekee ili tuingie katika uchaguzi na kupata Rais Mwingine ili aendeleze mchakato wa katiba mpya ni UROHO WA MADARAKA!

  Tukiruhusu Mabadiliko au Marekebisho ya Tume ya Uchaguzi na Tukapata Tume huru ya Uchaguzi na Tukaingia Uchaguzi mkuu 2015 huku tukiacha mchakato wa katiba uendelee chini ya Usimamizi wa Rais huyo mpya tutakuwa tumefuata matakwa yenye mlengo wa kisiasa zaidi na sio wenye kulenga kusikiliza matakwa ya mtanzania wa kawaida maskini kwa sababu zifuatazo:

  1.Lengo kuu la vyama vya Siasa ni kushika Dola tofauti na malengo ya wapiga kura na wananchi ya kutimiziwa matakwa yao na kupata mgao sawa wa raslimali na mrejesho kodi wanazolipa Serikalini kupitia huduma za jamii!

  2. Kupata Rais wa nchi 2015 bila katiba mpya hakutaleta ahueni yeyote kwa mtanzania wa kawaida bila kujali kuwa ni CUF,CDM, MAGEUZI,C.C.M au UDP kitachoshika Dola.

  3. Kuruhusu nchi iingie ktk uchaguzi bila katiba mpya kutamfanya Rais atayeingia madarakani 2015 kutengeneza mazingira ya kujilinda kama alivyofanya Mwai Kibaki nchini Kenya na kusababisha muda wa upatikanaji wa katiba mpya uwe mrefu zaidi!

  4. Tunahitaji tuvidhibiti vyama vya Siasa ili viwe na Sera moja juu ya Uchumi, utamaduni, siasa usiokuwa tegemezi. Vyama hivyo vitofautiane tu jinsi ya kutekeleza Sera hizo.

  5.Hakuna madhara yoyote kwa wananchi kuahirisha Uchaguzi 2015 wakitumia muda huo kushiriki kikamilifu bila shinikizo la muda kutengeneza katiba nzuri yenye maslahi yao na baada ya kupata katiba mpya ndipo tuingie kwenye uchaguzi

  6. Chama, mtu au kikundi chochote kitachoshinikiza tuingie Uchaguzi mkuu 2015 bila katiba mpya ni Wabinafsi na WAROHO wa Madaraka kwa maoni yangu! Wenye Uchu wa Madaraka ndo unawasikia wanaanza kujadili nani atakuwa Rais wa 2015 wakati hata Robo ya Ilani yao ya uchaguzi bado kukamilisha!

  TUKIPATA KATIBA ILIYOKAMILIKA NDIPO TUKAINGIA KWENYE UCHAGUZI TUTAFIKIA YAFUATAYO:
  1. Tutaweza kutengeneza mfumo mzuri wa vyama vyetu vyote vya Siasa viwe vyenye kutokana na wananchi wenyewe bila shinikizo kutoka mataifa ya kibepari.

  2. Tutaweza kudhibiti mfumuko wa Bei na kupandisha thamani ya Sarafu yetu.

  3. Tutaondokana na Sera za Kinyonyaji zenye kuzuia Serikali yetu kuanzisha Viwanda na kuvisimamia ili kuleta ajira kwa Wananchi wake.

  4. Tutadhibiti Rushwa kwa kujenga maadili ya kitaifa na kuruhusu mfumo huru wa kuzuia na kupambana na Rushwa.

  5. Haki itapatikana katika vyombo vitoavyo haki na ‘’Wananchi wenye hasira kali’’ watabadilika kuwa ‘’Wananchi wenye upendo madhubuti’’

  6. Uchumi utarudi mikononi mwa wengi na tutapata mgao wa Dhahabu, Almasi, Tanzanite zetu na Raslimali zetu kwa ujumla.

  7. Tutarudia utamaduni wetu mzuri wenye staha, heshima, kuvumiliana na upendo tele.

  8. Tutaendeleza ndoto za Mwalimu Nyerere za kuiunganisha Afrika kuwa moja.

  Ni maoni yangu kuwa nia ya dhati ya kupata katiba mpya iliyoridhiwa na Rais Kwa matakwa ya wananchi wengi, iendelee hadi kukamilishwa ili mradi tu tusiingie uchaguzi mwingine na katiba hii nzee!

  Je mwana JF uko tayari kuingia Uhaguzi 2015 bila katiba mpya?

  Au uko tayari kuruhusu Uchaguzi mkuu usogezwe mbele hadi hapo tutakapopata katiba mpya kwa maslahi ya wananchi?
   
 2. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mh, mkubwa una ubavu wa kudefend hii post yako? subiri kidogo tu.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  LOL! Bora apewe ufalme kabisa wa kubaki mdarakani milele kisha watoto wake watakuwa wanarithi mmoja baada ya mwingine.
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  :A S 13:Katika watu wasio na akili wewe ndo kiranja!!!!
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Duh! Tunalingana mawazo mkuu. Nilifikiri hivyo hivyo, awe mfalme, au angalau apewe uraisi wa maisha.
   
 6. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wambadilishe cheo.....kwa kuwa katiba mpya inakuja....itabidi aitwe Field Malshal Jogoo La Kikwere KaKa wa Kaka Dakta Profesa Wa Ukweli Mgao Wa Umeme Mwiko Mfalme Wa Wafalme King Of the World The Main Explorer, General Kanali Head Of State Emperor JK
   
 7. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  President King and Emperor for Life
   
 8. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kumbe kuna watanzania wengine mna umaskini wa mawazo?
   
 9. Bless the 12

  Bless the 12 Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  That is non-sense post, kuna haja ya jamii forum kulimit watu wanaojiresta humu, maana wengine hawana hata tone ya mawazo muhimu.
   
 10. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ndo mawazo yake jamvini, WHERE WE DARE TO TALK OPENLY.
   
 11. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Jamani watu wengine hawajui matani, hawa jamaa wa Chama Cha Zamani wana numbers pale mjengoni, wakichungulia JF waone hii thread watadhania anakubalika wanaweza kuchakachua mjengoni kuongeza muda wa mshikaji..pls acha satires:rain:
   
 12. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Bora aongezewe muda atusaidie kuizika ccm.
   
 13. Mageuzi

  Mageuzi Member

  #13
  Sep 20, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muheshimiwa Raisi Dk.Kikwete kuongezewa muda Wa uraisi ,ili amalizie maswala ya katiba mpya kwa urahisi,pia na kutuwezesha watanzania kuelewa maana ya katiba na umuhimu wake.

  isitoshe magamba yatakuwa yemevuliwa yote,na pia kusimamia magamba mapya yakichipua vizuri.

  Raisi wa marekani aliwahi kuongeza muda wa kuwa madarakani ,Franklin Roosevelt .1933 to 1945 . source: Franklin D. Roosevelt - Wikipedia, the free encyclopedia
  tunajua USA ndio nchi inayojitangazia uimwenguni kuwa na Demokrasia,na isitoshe Dk.Jakaya kikwete ni Friends of USA,so haitakuwa mbaya akiongezewa muda,hiyo pia ni sehemu ya Demokrasia

  natimiza haki yangu kikatiba ,kwa kutoa maoni bila kuvunja sheria
   
 14. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  mi sipo!
   
 15. d

  dotto JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Una lako jambo. Kwanza unayemsema haijui katiba! Ndo maana hata DC igunga hajui sheria za Tanzania.
   
 16. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katiba kitu gani banaa...hiyo si inabadilishwa tu? CCM inao wabunge 75% wanatosha kupitisha hayo mabadiliko.

  JK FOR LIFE.
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Massanja vipi huko Ze Komedi freshi?????????????

   
 18. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimechoka kumsema vibaya JK. Mwache apumzike salama. Najua nia yako. Na hatumshambulii ng'o. Kwanza hata yeye mwenyewe akiongezewa hata wiki moja baada ya muda wake kwisha ( kama atafanikiwa kumaliza miaka minne iliyobaki salama) hataki kabisa huo ujinga wenu mnaouita urais.
   
 19. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Embu wazubutu ndo watajua nguvu ya umma
   
 20. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Roosevelt hakuongezewa muda, kama ambavyo huwezi kusema Nyerere aliongezewa muda. Haikuwa inazuiliwa kuchaguliwa zaidi ya mara mbili wakati wa FDR hivyo alichaguliwa mara nne katika chaguzi za kawaida. Term limits zimeanza baada ya FDR, katika mabadiliko ya 22 ya katiba yao.
   
Loading...